Hiki hutokeaga kwangu hasa nikichanganya sheli. Mara nyingi huwa naweka Total nikiwa mjini ila siku za safari huwa naweka wese la Lake oil full tank.Duh leo nimetenda dhambi roho imeniuma sana. Nilikuwa na gari sijaizoe. Taa ya mafuta imewaka range inanionesha nina km20 tu. Nikaamua niweke mafuta ya kunifikisha home tu nikaweka 10,000 nilijua itaongeza range hadi km60 hivi. Baada ya kuweka mshale haukusogea wala range haikubadilika. Nikaenda ninapoenda range inashuka.
Kurudi nikapita njia ile ile range iko 14, nikapita pale kituo cha mafuta nikamwambia Yule dada nimeweka mafuta hapa kwako lakini gauge haikupanda wala kuonesha kuna mafuta yameingia, umeniibia! Dada Yule akasema sijakuibia nimekuwekea hela ulionipa nikamwambia haiwezekani kusiwe na mabadiliko kwenye gauge, ikabidi niende kituo kingine nikaweka 10, aisee gauge ikakurupuka ikapanda sana na range ikaja kwenye 110km. Hapo nikajua ni kweli aliweka mafuta nimemsingizia tu. Nimejisikia vibaya sana.
Good RRONDO. Knowledge is power.Labda tusiseme kubishana, tuseme kueleweshana. Wakati vuguvugu la zebra limeshika kasi mmoja alinisimamisha akataka kuniandikia kisa sikusimama kwenye zebra na hakuna mtu anavuka. Eti hata kama hamna mtu inabidi usimame uwashe hazard(wengi walipigwa faini) wakati sio kweli Sheria haisemi hivyo. Baadae polisi wenyewe wakatoa ufafanuzi kwenye zebra unasimama iwapo kuna watu wanataka kuvuka.
Hilo la tochi kituo A unasimamishwa kituo B bado linaendelea. Kuna siku maeneo karibia na Msata nilisimamishwa eti kwenye 50kph nimepita na 70kph. Nilikuwa na abiria na kila 50zone nilikuwa napita na 50. Wakanionesha picha. Ile picha inaonesha kibao kinachomaliza 50kph zone, nikamwambia nioneshe kibao cha 50kph zone ambako nimepita,hana picha. Nikamwambia mmetoa makusudi kibao cha kuanza 50kph ili watu wasikione halafu mnawapiga picha watu mkitumia kibao cha kumaliza 50kph mkiwatuhumu wako ndani ya 50kph zone na speed kubwa! Jamaa akawa mdogo akaniambia basi braza nenda.Na hata hapa bongo ndo inapaswa kuwa hvyo kwa utaratibu wa sheria. Mh.Kangi amebadilisha sana mambo mengi-Nitaongelea mifano michache,Alipiga vita sana mtu kupigwa tochi za nyuma ya gari na kusema ni kinyume cha utaratibu.Akasema pia ni marufuku kupiga picha kwa kuvizia au kupiga picha kituo A ili ukakamatwe kituo B.Akaenda mbali kusema kama Traffic kaangalia tairi la gari limekutwa kipara,kioo kina crack,taa imepasuka yote hayo ni makosa ya ubovu wa gari na ni kosa moja hvyo halitazid 30'000.
Mzee baba unaishi bongo kweli?Kiuhalisia ni kwamba Traffic hapaswi kutafuta kosa kwenye gari-Anapaswa kujua kwa nn anakusimamishia na siyo kuibua problems kichwani kwa kuhisi.Wabongo shida yetu ni kwamba hatujui wajibu wetu na haki zetu hasa tunaposimamishwa na traffic & appropriate channels za ku escalate mambo yetu pale tunaposhindwa kuafikiana.Hon. Kangi Lugola alitufumbua sana macho wananchi juu ya haki zetu pamoja na wajibu wa traffic na ndiyo maana hawa jamaa wa wa usalama barabarani hawakumpenda hata kidogo.
Naongelea sheria na miongozo ya nchi hii kaka na siyo hisia binafsi.Mzee baba unaishi bongo kweli?
Hizo unazosema ni theories tu,mimi kipindi kile cha lugola amesema( sijui ukikutwa na kosa la taa ni mbovu,side mirror mbovu,rangi imeisha hilo ni kosa 1 tu la uchakavu na sio makosa matatu) nilikamatwa kule Tegeta nikiwa na kosa la taa 1 mbovu nikakuta traffic wamemshikilia jamaa mmoja ana harrier old model yuko anabishana nao huku amewatolea simu wale maafande kwamba Lugola anasema hivi na bla bla blah kibao.
Mimi walivyonifata nikawaambia ni kweli afande taa yangu kweli ni mbovu lkn kwa sasa siko njema mfukoni lkn w/end hii salary itaingizwa nitatengeneza afande,nikaomba samahani.
Afande akaniambia jitahidi uitengeneze na sikutoa hata senti,yule jamaa aliyekua anabishana nao mambo ya Lugola akaandikiwa makosa mawili na akaambiwa mpige huyo Lugola mwambie tumekuandikia na pia na No. ya RTO hii hapa mpigie huko mbele ya safari mueleze tumekuandikia kibabe maana tunapendaga wajuaji kama nyie.
😀😀😀😀... tutapambana tu maisha, kuyaogopa ni sawa na ku fail😁 😁 😁 Duh! Be careful with your choices manake awamu hii na mambo ya CC kubwa siyo rafiki kabisa mkuu.
Hivi kumbe ni yule Kuhani mwenyewe?😃😃😃😃😃Unaijua hii yenye engjne ya VQ35 😀😀😀😀 au jesta.. ila nataka inayo anzia 2013.. kabei kake kazuri hasa zenye URS engine zenye UZS bei ipo chini ila sijazipenda.. ! Bado kidogo kibubu kifumuke..
Hii walinibutua wale wa kagomeni mwembe chai pale... zebra haikuwa na mtu wala mnyama.. nikasema sawa andika.. roho iliniuma sana.. najua naonewa.. ila kwakua nilikuwa nimeisha kasirika sikuta hata kujieleza nikasema andika tu.Labda tusiseme kubishana, tuseme kueleweshana. Wakati vuguvugu la zebra limeshika kasi mmoja alinisimamisha akataka kuniandikia kisa sikusimama kwenye zebra na hakuna mtu anavuka. Eti hata kama hamna mtu inabidi usimame uwashe hazard(wengi walipigwa faini) wakati sio kweli Sheria haisemi hivyo. Baadae polisi wenyewe wakatoa ufafanuzi kwenye zebra unasimama iwapo kuna watu wanataka kuvuka.
😃😃😃😃😃Hivi kumbe ni yule Kuhani mwenyewe?😃😃😃😃😃
Na hizo sheria na miongozo ndio jamaa wanapendaga watu wa dizaini hizo mzee.Naongelea sheria na miongozo ya nchi hii kaka na siyo hisia binafsi.
Hapa 80..100..120...130! Nalegeza mguu kidogo kulinda RPM zisivuke 3! 😝😝😝Bongo hii hiiView attachment 1678852
Sometimes unaepusha mengi kukubali kuonewa. Usiombe upewe kosa la kumzuia askari kufanya kazi yake!Hii walinibutua wale wa kagomeni mwembe chai pale... zebra haikuwa na mtu wala mnyama.. nikasema sawa andika.. roho iliniuma sana.. najua naonewa.. ila kwakua nilikuwa nimeisha kasirika sikuta hata kujieleza nikasema andika tu.
Mtoto ulimkosha sana hapa lazima ulinyakua point 3 za ujentromeni😂Nimerudi tena kuweka mafuta pale pale,yafuatayo ndio mazunguzo yangu na Yule dada
Mimi:Mambo
Yeye😛oa
Mimi:Niwekee 15,000 (huku nampa20,000)
Yeye:Naomba uangalie kabla sijaanza kuweka nishakukariri
Nikatabasamu na yeye akacheka
Yeye:Siku ile mshale ulipanda
Mimi:Ulipanda ni kweli uliniwekea mafuta
Yeye:Ulijisikiaje
Mimi: Nilijisikia vibaya sana ndio maana leo nimekuja tena kwako nikuombe msamaha
Yeye:Mimi nimekusamehe (huku akinirudishia chenji 5,000)
Mimi:Asante hio chenji kaa nayo ni sehemu ya msamaha wangu.
Nilimuacha ametabasamu na roho yangu imetulia.
Changamoto hii kwa sehemu kubwa huchangiwa na shape ya tank la mafuta ya gari.Tank la gari naweza lifananisha na bakuli-nusu ya chini huwa inajaa haraha sana,lakini kadri unavyozidi kujaza upandaji wake kwanzia katikati kuja juu huhitaji kimiminika kingi zaid kujaa kuliko ile second half ya chini.Ndiyo maana kwenye baadhi ya magari Tank likizid half tunaonaga linachelewa kushuka kufika half,lakin likiwa chini ya half hushuka haraka sana.Hiki hutokeaga kwangu hasa nikichanganya sheli. Mara nyingi huwa naweka Total nikiwa mjini ila siku za safari huwa naweka wese la Lake oil full tank.
Sasa mara chache hutokea nataka niweke mafuta katika zone ambayo hamna total. Huwa sipendi kutembelea gari inayowaka taa ya mafuta hivyo nalazimika kuweka mafuta kwenye visheli uchwara kama Oilcom, Meru n.k Hapo ndio mziki sasa.
Gari yangu hunionyesha mabadiliko kwenye gauge after 1.5km distance maana nina katabia ka ku reset trip meter kila nikitoka sheli. Ikitokea haijafanya hivyo huwa nafadhaika sana na kuisi nimeibiwa hela bure.
Ni kweli kabisa, maana na mie nilivyo ona nimekasirika nikaona hapa nipo kwenye danger zone.. najielewa. Nikakubali ila roho inauma sana.. nikachapwa mkeka safi, nika u clear hapo hapo alafu nikasepa zanguSometimes unaepusha mengi kukubali kuonewa. Usiombe upewe kosa la kumzuia askari kufanya kazi yake!
Hahah mara moja moja itupie mpk 5 to 6 Rpm kupunguza carbon buildup mzee.Hapa 80..100..120...130! Nalegeza mguu kidogo kulinda RPM zisivuke 3! 😝😝😝
Alafu kwenye vituo vya mafuta ma manager wao huwa ni ma pisi kali.. tu.. hasa kama kituo flani.. nisikitaje .. muhusuki akawapo humu.. nikahamisha kambi bure 😀😀😀Mtoto ulimkosha sana hapa lazima ulinyakua point 3 za ujentromeni😂
RRONDO angeshalipa basi hiyo faini ya tochi aliyoambiwa kapigwa 😁 😁 😁 .Woga wako ni hasara yako-Pambania haki yako kwa hoja na siyo woga usio na msingi.Kama umeamua kuwa mkimya unapoonewa it's fine ni wewe,ila viongozi wa nchi wamesema hiyo hapana.Ukiona haki yako inakanyagwa waziwazi wametoa hotline upige and sometimes for freee.Na hizo sheria na miongozo ndio jamaa wanapendaga watu wa dizaini hizo mzee.