Wazee wa Pixel: Google wamezindua Pixel 10 Series!

Hivi Tensor ni in-house zao tu kama A series za iPhones?
Tofauti na Apple ambayo hutengeneza in-house A-series chips zake kwa undani sana, chips za Google Tensor zinatengenezwa kwa ushirikiano.

Apple hufanya kila kitu kwenye chips zake. Kuanzia uundaji wa CPU (Central Processing Unit) na GPU (Graphics Processing Unit), hadi uzalishaji.

Chips za Google Tensor ni tofauti. Zimekuwa designed na Google, lakini hazijatengenezwa kabisa in-house. Google wana manufacture Tensor zao kwa ushirikiano na Samsung. Kwa hiyo, Tensor SoC (System-on-a-Chip) inatumia baadhi ya main components za Samsung Exynos, hasa CPU na GPU. Hata hivyo, Google inaongezaga component zake muhimu kama vile Tensor Processing Unit (TPU).
Tensor Processing Unit (TPU): Hii ndiyo sehemu muhimu zaidi kwenye chip ya Tensor. TPU imeundwa mahususi na Google kwa ajili ya kujifunza machine learning na AI. Inasaidia kufanya kazi kama vile Computer imagery, Magic Eraser, na data processing kwa haraka kwenye simu

Hivi karibuni Google imeanza kujitenga zaidi na Samsung. Kuanzia na chip ya Tensor G5 (ambayo inatarajiwa kutumiwa kwenye Pixel 10) Google imeanza kushirikiana na kampuni ya TSMC (Taiwan Semiconductor Manufacturing Company) kwa ajili ya uzalishaji.

Kwa kifupi, Tensor za awali zilikuwa na ushirikiano na Samsung, lakini Tensor zijazo zinatarajiwa kuwa miundo ya Google pekee inayotengenezwa na TSMC. Hii inazifanya ziwe kama in-house, lakini sio inhouse kabisa kama "Apple" ambao wao huunda kila kitu peke yao bila msaada kutoka nje kwa baadhi ya vipengele.
 
Kwa nini unataka kuhama Samsung?

Ninapenda gadgets na wala si sababu nyingine yeyote...

Nimekuwa nikitumia Samsung tangu 2012 hapo hadi sasa...

Pixel za mwanzo zilivyotoka sikuwa nimeguswa sana na muonekano wake, lakini kuanzia toleo la 9 na sasa hili la 10 zinashawishi kujaribu kuwa nayo...

Features nyingine za ndani nadhani hazipishani na Samsung sababu zote ni android OS...
 
Zote ni Android lakini Samsung wameweka One UI. Zina vitu vingi sana kuliko Pixel na zinatofautiana
Pixel software yake inawapendeza watu wanaopenda simplicity na minimalistic design, hawataki mambo mengi.
Samsung wao wamebase kila kona, kuanzia features, customization, AI nk. Software yao ina kila kitu
Ila kama umetumia Samsung tangu 2012, basi naelewa kwa nini unataka uhame
 
Tofauti na Apple ambayo hutengeneza in-house A-series chips zake kwa undani sana, chips za Google Tensor zinatengenezwa kwa ushirikiano.

Apple hufanya kila kitu kwenye chips zake. Kuanzia uundaji wa CPU (Central Processing Unit) na GPU (Graphics Processing Unit), hadi uzalishaji.

Chips za Google Tensor ni tofauti. Zimekuwa designed na Google, lakini hazijatengenezwa kabisa in-house. Google wana manufacture Tensor zao kwa ushirikiano na Samsung. Kwa hiyo, Tensor SoC (System-on-a-Chip) inatumia baadhi ya main components za Samsung Exynos, hasa CPU na GPU. Hata hivyo, Google inaongezaga component zake muhimu kama vile Tensor Processing Unit (TPU).
Tensor Processing Unit (TPU): Hii ndiyo sehemu muhimu zaidi kwenye chip ya Tensor. TPU imeundwa mahususi na Google kwa ajili ya kujifunza machine learning na AI. Inasaidia kufanya kazi kama vile Computer imagery, Magic Eraser, na data processing kwa haraka kwenye simu

Hivi karibuni Google imeanza kujitenga zaidi na Samsung. Kuanzia na chip ya Tensor G5 (ambayo inatarajiwa kutumiwa kwenye Pixel 10) Google imeanza kushirikiana na kampuni ya TSMC (Taiwan Semiconductor Manufacturing Company) kwa ajili ya uzalishaji.

Kwa kifupi, Tensor za awali zilikuwa na ushirikiano na Samsung, lakini Tensor zijazo zinatarajiwa kuwa miundo ya Google pekee inayotengenezwa na TSMC. Hii inazifanya ziwe kama in-house, lakini sio inhouse kabisa kama "Apple" ambao wao huunda kila kitu peke yao bila msaada kutoka nje kwa baadhi ya vipengele.
Man than deep. Shukrani sana.
 
Back
Top Bottom