Wazee wa Etihad, nini kifanyike kesho tutoboe UEFA?

Boutafrica

JF-Expert Member
Dec 11, 2014
948
2,037
Hali tete sana .... kama una la kumshauri Guadiola hebu weka maoni yako hapa huenda kuna mtu akayaona akampelekea ili ayafanyie kazi kesho.
 
Yaani kitendo cha kupigwa 3 bila ni kosa kubwa sana. Cha msingi akafunguke acheze mpira haswaaa maana hana sababu ya kujilinda.

Kwenye mpira yote yanawezekana na kuhakikisha hilo PSG analijua hilo
 
Waache kupaki basi....cha msingi ni kuuchambua mpira...pass za kutosha...na bila kusahau waongeze efficiency ya kufunga magoli. All the best!! Ingawa chance ya kupenya ni ndogo, chance bado mnayo ukichukulia Captain wa majogoo ataikosa hiyo mechi mhimu!
 
AKUMBUKE MACHUNGU ALIYOMFANYIA ARSENAL.. GADIOLA OUT

Waache kupaki basi....cha msingi ni kuuchambua mpira...pass za kutosha...na bila kusahau waongeze efficiency ya kufunga magoli. All the best!! Ingawa chance ya kupenya ni ndogo, chance bado mnayo ukichukulia Captain wa majogoo ataikosa hiyo mechi mhimu!
 
Labda waje kumuazima Okwi wanaweza kutoboa ila kwa wale strikers wao uchwara, hawataweza kutoboa.
 
city ana uwezo wa kupita hatua ya nusu fainali kama tu rate yao ya kubadili nafasi kuwa magoli itakuwa kubwa na la msingi wasiruhusu goli pale etihad
 
Nachoweza kumshauri Guardiola ni kuwa aingie kama mechi nyingine tu asije na tatctic kama alizotumia juzi za kumjazia dogo Alexander Arnold wale wakali wake akina Sane, KDB na Silva akidhani kuwa ndio weak link ya defense ya Liverpool matokeo yake mbinu imemtia aibu.

Ajaribu kucheza mchezo balanced ana amwanzishe chura sterling ili tuone anavyopewa vitasa na Robertson

Pili mwambie sasa hivi Liverpool imepata kiranja pale nyuma anaitwa vVD hivyo akumbuke first leg hawakupiga hata shot moja on target. Wajaribu kupiga za mbali.

Pia waambie wasifanye fitna kwa mashabiki wa Liverpool na wasinaribu kuiga walichokifanya mashabiki wa Liverpool kwenye kuzipokea team maana wale ni wahuni haijawahi kutokea.

Man City akishinda labda atapata draw. Liverpool anashinda kwa mbembwe zote. Kama unaweka mkeka weka hata mke au nyumba
 
Siku ile île Guardiola aliomba PDF za notice wslizotumia Barca kuwang'oa PSG. akaziprint kwa vile anaamini katika hardcopy.

Kaniambia Ijuma ndio alimaliza kupitia kwa Mara y'a pili wakaifanyia mazoezi ila wakahofu kuitumia mechi y'a mtani kwa sababu kuwa majogoo wataogopa n'a kuwa Makini.

Mwenyewe Kaniambia Jurgen atatukanwa sana
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom