PostGE2025 Wazee wa Dar es Salaam wampongeza Rais Samia kwa ushindi mkubwa

PostGE2025 Wazee wa Dar es Salaam wampongeza Rais Samia kwa ushindi mkubwa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Mwenyekiti wa Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Salum Matimbwa amesema Wazee wa mkoa huo wanaungana na Watanzania lkumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushindi wa kishindo alioupata katika uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.

Mzee Matimbwa akizungumza katika Mkutano wa Wazee hao na Rais Samia amesema ushindi huo ni ishara ya imani kubwa ya Watanzania kwa Dkt. Samia, kwamba ni kiongozi mahiri na makini

Hata hivyo, Mzee Matimbwa ameeleza kuwa wanatambua kampeni zilifanyika kwa utulivu mkubwa na hata uchaguzi mkuu mpaka pale vurugu zilipojitokeza.

Ameongeza kuwa kadhia hiyo imewafadhaisha kwa sababu vifo vimetokea, mali zimeharibiwa, miundombinu imeathiriwa n.k.



 
Unaweza ku comment UKA AMBIWA HAUNA MALEZI YA PANDE MBILI...

Ngoja ninyamaze...

Hapa nasikiliza ngoma za BOBBY WINE..
 
Hahahaha hawa ndio hazina ya taifa?....Yeye mwenyewe anajua hakupigiwa kura.....
Gen Z kazi mnayo na wazee wenu hawa....Matimbwaaaa
 
Back
Top Bottom