petrinamwana
JF-Expert Member
- Dec 9, 2011
- 901
- 345
Hahaha nmhh mbona mambo
Maofisa mbalimbali wa Mamlaka ya Bandari Tanzania wamepania kumwonyesha Waziri Mteule wa Uchukuzi,Dr.(PhD) Harrison Mwakyembe,kilichowashinda watangulizi wake: Omari Nundu na Athuman Mfutakamba.Wakiongea nami jana katika nyakati tofauti juu ya vipi watampokea Waziri 'mpya',wazee hao wa Bndari walitamba kuwa hawataacha kilichozoeleka Bandarini hapo.'Tunajua Rais anatupima ubavu kwa kutuletea Mwakyembe.Na aje tumwonyeshe mfupa mgumu hapa Bandarini.Hatutaacha mazoea yetu'. alitamba mmoja wa wazee wa Bandari. Mwakyembe ataisafisha Bandari yetu?
Mamlaka ya bandari ya mkusanyiko wa wazee fulani waswahili swahili kiasi kwamba wamekuwa ni watu wa kuendekeza ushirikina tu na ndio maana wengi wao licha ya kufanya kazi bandarini miaka mingi na kipato kizuri lakini wako duni kabisa. So hilo la kumuonyesha Mwakyembe mfupa uliowashinda watangulizi wake ndio muendelezo wa ule ujinga wao...lakini tatizo ni kuwalea na kuwaogopa ndiko kunakowapata kiburi. Kuna jamaa yangu ndugu yake alipata kazi ya udereve pale temporary kwa muda wa miezi miwili tu jamaa aliambiwa kuwa kuendesha gari iliyokuwa ikiendeshwa na yule mzee inabidi awe mgumu jamaa hakujali lakini siku ya 5 tu akaomba kuacha kazi......:eek2:
Hapa inawezekana kuna mtu mkubwa anaogopeka hapa..ni nani? na kuna kipindi mkulu alisema kuwa anawajua watu wote wa bandari pale na matendo yao...
Kweli tz tuna hali mbaya! Presidaa anaelewa kila kitu ila haelewi afanye nini! Thats why huwa anaenda abroad maana hawezi fanya lolote zaidi ya unafiki hilo ni pro yakeMkuu hakuna statement inayoudhi kama hiyo hasa toka kwa mkuu! Anawajua wauza unga wote, anawajua majambazi sugu, anawajua wezi wa halmashauri, anawajua walaji wa bandari, lakini hajui kwanini Tanzania ni maskini! Lol, Tanzania ina kila sababu ya kuingia ktk historia kwa kuwa na raisi wa kipekee