Wazazi wamkataa mchumba wangu kisa mahari ni ndogo

USHAURI KAMA HUU WA WATU WASIO NA DINI NA HOFU YA MOLA WAO USIUZINGATIE... MCHE MOLA WAKO... TARATIBU ZA KIISLAAM ZA KUFUATA ZIPO... KAMA BABA ANAENDEKEZA UJINGA... ANAACHWA TU... NA NDOA ITAFUNGWA KWA USIMAMIZI WA MAWALII WENGINE...

KWA SABABU UKIFANYA ZINAA HUTOMKOMOA MTU BALI UTAJIKOMOA MWENYEWE...
beba mimba ya mwamba game over
Muhusika usijaribu kabisa huu ujinga. Tulizana kwa mzee ukule raha cha msingi mtu wakukuoelekea moto yupo basi hamna shida genye zikidizi unampelekea jamaa anakugegeda

Mwambie jamaa akutoroshe akupangie sehemu ubebe mimba yake na ugome kabisa kurudi kwenu ikwezekana ubadilishe na namba zako za simu.

Baada ya muda wazazi wako watapata uchungu wa uzazi watakuja kukuomba msamaha na kurudisha mahusiano na wewe.
 
Mkipata wa kuwaoa tena pana kizuizi nyumbani sijui mahari wengine wanauliza Elimu wakati wao hawana...hatari sana kwa kweli Mzee kakosea maana wapo wanaoenda bila hata kulipiwa chochote baadae utasikia wahuni wanakuja kujitambulisha sema Mzee inatakiwa wazee wa busara wakae nae wamuelekeze hayo maisha anayoyataka ayapo na pia kinachotakiwa ni kuwatakia maisha mema tuu maana Mahali sio ubora wa ndoa na ndoa inaweza ikawa bora na isiyo na migogoro na wahuni wakawa walilipa kidogo tuu..
 
USHAURI KAMA HUU WA WATU WASIO NA DINI NA HOFU YA MOLA WAO USIUZINGATIE... MCHE MOLA WAKO... TARATIBU ZA KIISLAAM ZA KUFUATA ZIPO... KAMA BABA ANAENDEKEZA UJINGA... ANAACHWA TU... NA NDOA ITAFUNGWA KWA USIMAMIZI WA MAWALII WENGINE...

KWA SABABU UKIFANYA ZINAA HUTOMKOMOA MTU BALI UTAJIKOMOA MWENYEWE...
Sasa wee kwani hapo alipo unahuhakika gani kwamba apelekewi moto
 
huyo babaako aache akili za kivuta bangi, mwanaume utaishi nae wewe sasa yeye anatia kauzibe ya nini? mahari 10m kwamba anakuuza au? wazazi kama hao ndio hua wanafanya wanaume wanakua na hasira hadi wanaua wake zao kwa kosa dogo tuu... mwambie ameniudhi sana.
 
Tunapaswa kuwaheshi baba na mama, hii ni amri tuliyopewa na Muumba, lakini naamini kwa hili hata huyo shetani mtenda maovu ameuficha uso wake maana ni kituko cha mwaka.

Baba yako ni KENGE, tena ni bonge la kenge, kama huyo bro anakupenda kwa dhati alipe hizo 3M then m-focus na maisha yenu ndugu sometimes wana lostisha.

Wahusishe viongozi wa dini kulingana na imani yako, hebu muulize alimuoa mama yako mahali kiasi gani. Wewe dada kuwa na makini usipoangalia utakuwa single mother.
 
Habari zenu wana JF,

Bila kuwachosha naenda moja kwa moja kwenye point. Nilikuwa na mchumba wangu tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka sasa. Kwa hiyo mwaka huu huyo kaka nilimwambia aje home kujitambulisha, akasema haina shida.

Niliwataarifu wazazi wangu tarehe ambayo aliniambia anakuja wakasema aje kwetu.

Kama kawaida huyo kaka alikuja na mshenga wake pamoja na mjomba wake. Baba yangu alialika wenzake kama 6 hivi ili kujadiliana mahari. Kwa kweli ilikuwa tafrani, kwasababu baba yangu mzazi alishauriana na wenzake mahali iwe 10.5M kitu ambacho kilinishangaza sana.

Mjomba wake akasema hiyo hela hawana kwani hawanunui kiwanja. Baadae mjomba akasema wao wanaweza toa 2.5M baba akasema iongezeke japo 3M kwa shingo upande, kwamba hataki mahari ndogo akidai watakuja wengine.

Jioni yake akaniita mimi na mama akaanza kunifokea. Akaniambia mimi namdhalilisha kuleta mtu masikini na haeleweki kwa hiyo niachane naye, na nisipoachana naye mimi nitakuwa siyo mtoto wake na nikikubali kuolewa naye nisije kukanyaga kwake mpaka kaburi lake nisije kulisogelea.

Hakuishia hapo akaanza kunilinganisha na kabati ambalo anadai limenizidi, kwamba yeye alilinunua kwa bei kubwa kuliko mahali yangu. Nililia sana maana hata mama yangu alikuwa upande wa baba kwa hiyo sikuwa na support yoyote.

Aibu naipata mimi mtaani, naogopa hata kutoka kwenda sehemu kwa ajili ya wazazi wangu kunisambazia doa kubwa.

Naombeni ushauri katika huu wakati mgumu, kushauriwa kumuacha mtu uliyependana naye mkaendana siyo kitu rahisi. Japo huyo kaka hajaonesha dalili zozote za kuniacha, anawasiliana na mimi kama kawaida.

Ahsanteni sana. Napitia maoni yenu, wote nawakaribisha.
KAMA UNAMPENDA MWAMBIE HUYO MWAMBA AKUTIE MIMBA KWANZA,HIYO NDIO TECHNIC NILIYOTUMIA MIMI MZEE WA CUBA,MWENYEWE AKANYOOKA HUYO BABA MKWE
 
Kazi ya kueleweka anayo..N mhandisi wa masuala ya umeme.Lkn kwa sas mwenyez mungu hajajalia kupata kazi kwa ivo anajishikiza kweny mishe mbali mbali hata hio mahali hamna mtu kamchangia.
Kama mnapendana komaa nae tu ndo rizki yako achana na miruzi ya wazazi ..mahari kitu gani wakati jamaa anakuhudumia miaka kibao mbele..Hyo ndo rizki yako .
 
Habari zenu wana JF,

Bila kuwachosha naenda moja kwa moja kwenye point. Nilikuwa na mchumba wangu tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka sasa. Kwa hiyo mwaka huu huyo kaka nilimwambia aje home kujitambulisha, akasema haina shida.

Niliwataarifu wazazi wangu tarehe ambayo aliniambia anakuja wakasema aje kwetu.

Kama kawaida huyo kaka alikuja na mshenga wake pamoja na mjomba wake. Baba yangu alialika wenzake kama 6 hivi ili kujadiliana mahari. Kwa kweli ilikuwa tafrani, kwasababu baba yangu mzazi alishauriana na wenzake mahali iwe 10.5M kitu ambacho kilinishangaza sana.

Mjomba wake akasema hiyo hela hawana kwani hawanunui kiwanja. Baadae mjomba akasema wao wanaweza toa 2.5M baba akasema iongezeke japo 3M kwa shingo upande, kwamba hataki mahari ndogo akidai watakuja wengine.

Jioni yake akaniita mimi na mama akaanza kunifokea. Akaniambia mimi namdhalilisha kuleta mtu masikini na haeleweki kwa hiyo niachane naye, na nisipoachana naye mimi nitakuwa siyo mtoto wake na nikikubali kuolewa naye nisije kukanyaga kwake mpaka kaburi lake nisije kulisogelea.

Hakuishia hapo akaanza kunilinganisha na kabati ambalo anadai limenizidi, kwamba yeye alilinunua kwa bei kubwa kuliko mahali yangu. Nililia sana maana hata mama yangu alikuwa upande wa baba kwa hiyo sikuwa na support yoyote.

Aibu naipata mimi mtaani, naogopa hata kutoka kwenda sehemu kwa ajili ya wazazi wangu kunisambazia doa kubwa.

Naombeni ushauri katika huu wakati mgumu, kushauriwa kumuacha mtu uliyependana naye mkaendana siyo kitu rahisi. Japo huyo kaka hajaonesha dalili zozote za kuniacha, anawasiliana na mimi kama kawaida.

Ahsanteni sana. Napitia maoni yenu, wote nawakaribisha.
muulize anafanya biashara haramu ya binadam?
 
kwa io imeandikwa baba akuchagulie mume..Kama huna ushauri tulia

Nionyeshe ni wapi iliandikwa baba anaweza kukutafutia mume..Tumieni vizur maandiko sio kupotosha watu
Ni kawaida kwa Binadamu kupingana na Maandiko ya MUNGU.
Nimekuambia soma katika Biblia kitabu cha KUTOKA 22:16-17 kisha tafakari nini maana ya maagizo hayo.

Ukitafakari kwa makini baada ya kusoma kifungu hicho, na ukiwa na akili timamu kichwani utaona kuwa baba wa binti amepewa mamlaka ya kuamua nani amwoe binti yake na kiwango kipi cha mahari.

Lakini kwa sababu ya "ukaidi" na "shingo ngumu" wanadamu wamekuwa wakipuuza maagizo ya MUNGU.
 
Ni wapi nimetumia Maandiko vibaya???
Ni sawa ulivyosema mtoto anatakiwa kutii wazazi wake, lakini sio kila kitu unachoambiwa hata kama kitakuletea athara ni kukukubali tu.

Kuna muda wazazi huwa wanatukosea sana, suala la mapenzi halitakiwi kuingiliwa kama watu wamependana waachwe sio wazazi mnaanza kuwawekea obstacles kwa kuwa hamjapendezewa kumuona huyo mtu anaoa au anaolewa katika familia yenu, na kuna wazazi wengine wanafanya vitu vibaya kwa makusudi ili apate sababu ya kukuachia LAANA na RADHI

Mfano kwako mzazi wako akuambie "mwanangu hebu kula hayo mavi hapo" je utatii na kula hayo mavi kwasababu kwenye biblia wameandika utii wazazi wako?

Muda mwingine huwa tunatumia maandiko vibaya kwa kukurupuka tu bila kutafakari na kutumia hekima, mwisho wa yote tunatakiwa sawa kutii wazazi wetu lakini sio kwa kila kitu utakachoambiwa wewe ni kufata tu mkumbo ili uwafaidishe watu pasipo kujiangalia na wewe
 
Tunapaswa kuwaheshi baba na mama, hii ni amri tuliyopewa na Muumba, lakini naamini kwa hili hata huyo shetani mtenda maovu ameuficha uso wake maana ni kituko cha mwaka.

Baba yako ni KENGE, tena ni bonge la kenge, kama huyo bro anakupenda kwa dhati alipe hizo 3M then m-focus na maisha yenu ndugu sometimes wana lostisha.

Wahusishe viongozi wa dini kulingana na imani yako, hebu muulize alimuoa mama yako mahali kiasi gani. Wewe dada kuwa na makini usipoangalia utakuwa single mother.
Kitendo cha kumwita mzazi wako "KENGE" ni dhambi kubwa, adhabu yake ni kifo. Tena imeandikwa, "amelaaniwa amdharauye baba yake au mama yake.

Mwenye masikio na asikie!
 
Wavulana naona mnatokwa povu ila hakuna mzazi anayefurahia mwanae kuolewa na mwanaume asiye na kipato. Subirini nanyi muwe baba mtafanya the same.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom