Baadhi ya wazazi wamemuomba Waziri wa Elimu kuingilia kati suala la wanafunzi kufukuzwa kiholela katika shule hiyo baada ya bodi ya shule chini ya shinikizo la Mkuu wa Shule hiyo anayefahamika kwa jina la Kandoro kuwafukuza shule tarehe 03/06/2023.
Wazazi wanadai watoto hao walifanya makosa ya utovu wa Nidhamu ambayo hayastahili watoto hao kufukuzwa shule. Pia, wazazi wanalalamika kuwa watoto hao wamekuwa wakijeruhiwa kwa kupigwa vichwani, kwenye nyayo na migongoni na wanadai ushahidi wanao.
Wazazi wanamuomba Waziri wa Elimu kushughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo kwani wamechoshwa na mkuu huyo ambaye anadai anaweza kufanya lolote na hakuna wa kumtisha kwakuwa kuna mtu mzito anamtegemea Serikalini.