Wazazi wa kisasa kwenye kusomesha Watoto shule wanafanana na wauza maduka wa sinza

Wazazi wa kisasa kwenye kusomesha Watoto shule wanafanana na wauza maduka wa sinza

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,437
Reaction score
35,963
Wazazi wa kisasa kwenye kusomesha watoto shule wanafanana na wauza maduka wa sinza.

Duka la sinza fremu kodi milioni, decorations za duka zinatumika milioni 10.

Halafu mtaji wa bidhaa za kuuzwa dukani thamani yake laki 7 tu.

Hivyo hivyo kwa wazazi. Mtoto primary analipiwa ada kwa mwaka milioni 3. na chekechea ada milioni 2

Kwa miaka saba mpaka anamaliza la saba imetumika zaidi ya milioni 20.

Sekondari mtoto anapelekwa tena private school ada milioni 5, mpaka anamaliza form 4 inatumika jumla milioni 20.

A level tena shule nyingine ada mamilioni, chuo tena hapati mkopo analipiwa ada milioni kazaa kila mwaka.

Mtoto anahitimu chuo anarudi nyumbani hana ajira. Sababu hana ajira hivyo mtoto huyo anamuomba mzazi mtaji ili ajiajiri. Mzazi anampa mtaji mdogo chini ya milioni tano, ambao unatosha kufungua banda la chips tu ama duka la mangi la kawaida.

Imagine

Mzazi katumia zaidi ya milioni 50 kumsomesha tu mtoto mmoja. Ila mzazi huyo huyo hana uwezo wa kumpa mwanae mtaji wa kueleweka pale mtoto anapomaliza chuo na kukosa ajira. Ama mzazi hawezi kumpa mtoto wake urithi wa biashara ya kueleweka kama kina Mo dewji walivyopewa na baba zao.

Yaani elimu ya private school inalipiwa hela nyingi. Huku ni kama decorations ya duka, halafu kwenye kujiajiri mtoto huyo huyo mtaji anapewa mdogooo , ama hapewi mtaji kabisa anabaki anahangaika tu.

wazazi tubadilike,
 
Hapo ujazungumzia mshahara ikiwa huyo mtoto atajiiriwa.

Gharama zote hizo mshahara ni kuanzia laki 7 mpaka milioni 3.
 
Kumbuka hiyo ada hajatoa kwa mkupuo ametoa kidogo kidogo kwa mda wa miaka 12

Lakn mtaj u atakiwa utolewe kwa pamoja n ngumu kupata kias kikubwa kama hicho kwa wakat mmoja

Ushaur kwa waazaz kwa hal ya sasa ilivyo wakat vijana wanasoma wakirud likizo wapate muda wa kujifunza na stad nyingne za maisha kama useremala welding makanika au kama una biashara mshirikishe apate uzoefu badala ya kuwaza tuishen
 
Back
Top Bottom