Wazazi kuweni makini sana na hawa Mabeki tatu angalia walivyoharibu maisha ya Zungu

jooohs

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
2,067
8,595
Natumai wote muu wazima, pia tusisahau kuchukua tahadhari
juu ya covid 19.

Ok ,leo wakati naendelea na harakati zangu za kutafuta ugali wa kila siku, ghafla nikaono ujumbe kwenye simu yangu, bro huku kijijini life limekuwa gumu naomba nisaidie elfu tano nitashukuru sana.

Hapo mawazo yakanirudusha mbali sana nikiwa mdogo wakati ninakuwa kulikuwa na jamaa mtaani watu wanamwita zungu, katika kijiji kile jamaa alikuwa tofauti na kila mtu, kuanzia rangi, muonekano wengine walikuwa wanamwita albino, wengine mzungu ndio chanzo cha jina hilo zungu.

Kipindi hiko nilikuwa mdogo sana lakini kadri siku zilivyokuwa zinasogea nikaanza kujiuliza maswali mbona huyu jamaa ni mzungu kabisa wakati mama yake ni Mtanzania tena mweusi kabisa, kwa weupe jamaa aliokuwa nao alikuwa ni kaburu pure.

Pia nyumbani kwao alikuwa hana cha kaka wala dada alikuwa anaishi yeye na huyo mama yake mtanzania, maisha yenyewe waliokuwa wanaishi yaani ni shida tupu, kuanzia chakula, elimu, hata nyumba waliokuwa wanakaa.

Jamaa tulikuwa tukienda kwenye vibanda umiza vilivyokuwa vinatumia generator kucheki movies za kina rambo na van damme ndio kama maskani yake.

Sasa kuna siku nilikaa nikamuuliza mama yangu mzazi, baba yake zungu ni mtu wa wapi mbona zungu yeye yuko tofauti sana halafu tumesha zoea watu weupe mambo mazuri mbona yeye yupo yupo tu.

Ndio nikaanza kupewa kisa cha mama yake na zungu kuwa toka kitambo alikuwa ni mtu wa kuolewa na kuachika, kwanini alikuwa anaachwa na kila mwanaume sababu ni kuwa alikuwa hazai soo aliamua kukimbia Tanzania enzi za East Africa kabla mipaka haijafungwa akaenda kutafuta kazi huko Nairobi.

Alifanya kazi za ndani kwa miaka kadhaa ndio akapata kibarua kwa wazungu fulani waliokuwa wanafanya kazi kwenye mashirika makubwa, wengine wanasema UN, wengine UNDP wengine WHO, wengine UNICEF kila mtu anazungumza analoweza kuzungumza.
Bahati mbaya hao mabeberu wakapata mtoto ambae inasemekana ndio huyo zungu, sasa kwa kuwa huyo beki tatu alikuwa hana mtoto alitokea kumpenda sana zungu na hao mabeberu walikuwa ni watu wa safari safari ikabidi huyo beki tatu apange njama atoroke na zungu akiwa na miezi kadhaa kujanae mpaka bongo.

Zungu baada ya kuwa mkubwa marafiki zake walikuwa wanamtania yaani unapigwa msoto hapa bongo na wazazi wako wako Ulaya wanakula bata, kuna siku alipandwa na hasira akamkaba mama yake, ikabidi mama yake amwambie sijui baba yake alikuwa anakaa wetsland nairobi mara riverside

Mpaka leo maisha ya zungu yameharibika ndio huyo alikuwa ananiomba nimsaidie elfu 5000, Tuweni makini na hawa mabeki tatu wakuokota okota sehemu nyingine beki tatu anachukuliwa taarifa za muhimu hadi anapimwa afya.
 
Mama naye alikupiga fix tu, mzungu sio mtu wa kupoteza mtoto kirahisi namna hiyo.

Kwanza utoroke na mtoto mzungu kutoka Kenya mpaka Tanzania? Hiyo haiwezekani hata kwa dawa, utakamatiwa boda tu.
 
Mama naye alikupiga fix tuu, mzungu sio mtu wa kupoteza mtoto kirahisi namna hiyo.

Kwanza utoroke na mtoto mzungu kutoka Kenya mpaka Tanzania? Hiyo haiwezekani hata kwa dawa, utakamatiwa boda tuu.
Ndio inawezekana maana hakuna majibu ya moja kwa moja kuhusu huyo jamaaa
 
Huyo zungu hajapata nafasi tu ya kugundua kipaji chake, hakutakiwa kusota kijiji, huku arusha wapo hao mixed race na akijitambua life inanyooka. Ni wapambanaji wa ukweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom