NADHARIA Wazazi hawatakiwi kukutana kimwili mtoto wao akifanyiwa tohara?

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Source #1
View Source #1
Wadau habari zenu!

Tumemfanyia tohara Jana mtoto wetu wa miaka 2. Mbaba mdogo akanipigia akaniambia tuache kushiriki/kukutana na mke wangu hadi watoto wapone.

Ni mwiko kabisa.

Je, ni kweli wadau?

Screenshot_20230622-151507_1.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwa na uvumi kutoka baadhi ya watu wa Jamii ukidai kuwa Wazazi hawatakiwi kufanya mapenzi baada ya kufanyia tohara mtoto wao wa kiume mpaka kidonda chake kipone. Uvumi huo unaeleza kuwa ikiwa wazazi watakutana kimwili itapelekea kidonda cha tohara cha mtoto wao kutopona kwa haraka.

Uvumi huu umeenea katika jamii mbalimbali nchini kiasi cha kufikia kuletwa mpaka kwenye Majukwaa ya JamiiForums

Mfano: Mnamo Julai 22, 2015 Mwanachama wa Jamiiforums Vkeisy2006 alikuja na andiko lake akiuliza:
Naomba niulize, juzi juzi nimetairi watoto wangu wawili (vidume vya mbegu), lakini ma mkwe akatuita chemba na katuonya haturuhusiwi kudinyanya wenyewe wala kuchepuka mpaka watoto wapone kabisa.

Hivi kuna uhusiano gani kutairi mtoto na Kufanya mapenzi baba na mama au mama na mtu mwingine na baba na mtu mwingine na mtoto kuchelewa kupona?
Hata hivyo katika andiko hilo 99% ya walitoa maoni yao walipinga jambo hilo na kulihusisha na imani potofu. Mfano: Mwanachama Heargy da Best alieleza:

Hizo ni fikra potofu, hapana tatizo lolote. Unaweza kustarehe na mtu wako bila tatizo lolote.

Je, upi ukweli hasa wa jambo hili?
JamiiForums imefanya jitihada za kuwatafuta baadhi ya wataalamu wa Afya ili kupata ufafanuzi wa kitaalamu kujua ukweli wa jambo hili ambapo tumepata maoni yafuatayo:

Mtaalaumu wa Afya Daktari Isimbula Mnalimuka anakanusha uvumi huu kwa kusema:

"Hakuna uhusiano wowote kati ya kidonda cha tohara cha mtoto na wazazi wake. Wazazi kukutana kimwili haiathiri chochote kwenye maendeleo ya kidonda cha mtoto. Hivyo, hoja ya wazazi kutotakiwa kufanya mapenzi baada ya mtoto wao kufanyiwa tohara zinabaki kuwa ni imani za kijamii zisizo na uthibitisho wa kisayansi."

"Daktari Isimbula anaongeza kuwa, kidonda cha tohara cha mtoto ni sawa na kidonda kingine kinachoweza kutokea kwenye mwili wa mtoto ambapo hakina uhusiano wowote na wzazi wake. Kuchelewa au kuwahi kupona kwa kidonda hicho itategemea mazingira ambayo mtoto anashinda na namna kidonda hicho kinavyohudumiwa kwa kufuata ushauri wa Wataalamu."

Naye, Daktari Godfrey Chale mtaalaum wa magonjwa ya Wanawake na uzazi hatofautiani na Dakati Isimbula ambapo yeye anasema:

Jambo hili sio kweli na ni Imani tu. Hakuna uhusiano wowote wa kisayansi kuhusu jambo Hilo.

Hivyo kutokana na ufafanuzi wa Wataalam hao juu JamiiForums inaona kuwa hoja ya wazazi kutotakiwa kukutana kimwili baada ya mtoto wao kufanyiwa tohara ni nadharia tu ambayo haina ushahidi wa kisayansi.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom