tremendous
JF-Expert Member
- Aug 12, 2016
- 3,237
- 5,313
Habari wana JF
Kama tujuavyo mtoto huzaliwa akiwa hajui chochote ila anajifunza kadri anavyo interact ktk mazingira yake.
Katika kujifunza mtoto huchukua mazuri na mabaya kutoka ktk jamii inayomzunguka kwahiyo ni kazi kwa mzazi kuhakikisha mtoto anakuwa na maadili yenye kukubalika ktk jamii.
Ktk kuwaadhibu watoto wao baadhi ya wazazi hutoa adhabu ambazo hazilengi kuwafunza watoto bali kukomoa kama hizi hapa:
Kumfukuza mtoto nyumbani baada ya kutenda kosa. Wewe ndio mzazi wake unataka aende kwa nani sasa, tena wengine hufukuza hata iwe usiku mwishowe mtoto abakwe utamlaumu nani,!!
Kumpiga mtoto hadi unamdhuru. Kuna watoto wanapigwa hadi wanavunjwa, kupigwa ngeo. Mtoto anakuwa na vidonda mwili mzima hadi huruma.
Kunyimwa chakula. Hivi mzazi utamnyimaje mtoto chakula eti adhabu hiyo dah! Mtoto anahitaji chakula ili akuwe na kujengeka mwili ( growth & development).
Kuchomwa moto. Baadhi ya wazazi huwachoma watoto viganjani hasa wale wadokozi iliwakome. Kwanza hii tabia ni indication kuwa mtoto hashibi sasa badala ya kumpa chakula cha kutosha mtu anaishia kumchoma moto mtoto.
Ewe mzazi/mlezi mpe mtoto adhabu inayolenga kumfunza sio kukomoa.
Adhabu za kikatili humfanya mtu kuwa na tabia za ajabu ukubwani.
Mostly tulivyo leo ni reflection ya malezi tuliopewa na wazazi/walezi wetu.