Wazawa wa mkoa wa Lindi mko wapi kutumia fursa zilizomo mkoani kwenu?

Kwa hio wabantu wote wanafana mkuu? Wachaga wnafanana na waha? Wahaya wanafana na wasukuma? Wasikuma ni mijitu yenye mili na nguvu lakini wapogoro hawajai hata mkono,wabantu wanafana vipi?
Hata ndani ya kabila moja kooo moja na nyingine hawafanani sembuse kabila na kabila.Kuna tofauti kubwa sana kati ya wabantu.
Hata hivyo raia wa Tanzania sio wabantu tu.Kuna nilotics(Masai), hotento mfano wahadzabe, wasandawe sio wabantu, ndugu zao ni Khoisan (bushmen) wa Afrika kusini.Tanga l,Tabora,Shyintanga, Mbeya huko kuna shombedhombe wa kiarabu.
Jaribu kujielimisha kuhusu historia ya watu Hapa Tz, watu hatufanani kivile, wazaramo wembamba warefu wastani huwezi kukuta bonge, utawafananisha na wanyakyusa mwili nyumba? Japo wote wabantu?
Hivi kuna mahali niliposema wanafanana?! Nimekuambia hivi wabantu wale wale wawepo wa eneo moja wawe ndo wabaya kuliko wote na wengine ndo wazuri?! Hilo la kwamba sio wote wabantu nimeshalisema; angalia post uliyoni-quote sentensi ya mwisho nimemaliziaje!!!

Suala sio kufanana bali suala ni "wale wana sura mbaya" kuliko wengine. Watu wanaweza wasifafane hata punje lakini wote wakawa ama wazuri sana au wana sura mbaya sana.
 
Habari wakuu,

Tukiwa tuna uaga mwaka, kuna mambo ya kujadiri haswa taswira na maendelea ya mikoa yetu tulioko au tuliko zaliwa au tunapoishi.

Mwaka huu nimejikuta nimekwenda mkoa wa Lindi kuliko mikoa mingine apa Tanzania mengi nimejionea zikiweno fursa, mazingira, mapungufu na mengine mengi.

Mkoa wa Lindi ni mkoa mzuri kuishi kwa sababu. Kwanza hari ya kijiografia yake mzuri, miinuko kidogo, tambarare, hari ya hewa, misitu, ardhi yenye rutuba. Kwa ufupi ni mkoa ambao una kila sababu ya kuwa mkoa ambao unavutia na wenye maendeleo kama mikoa mingine lakini cha kushangaza mkoa wa Lindi umepoa sana.

Upo kimya kana kwamba wapo katika maombolezo. Ukienda apo stendi na viunga vyake utashangaa kuona mitaa ipo kimya mno, hukuti muvumenti amabazo zinakufanya uone **** watu wanatafuta maisha au wanakiu ya kimaisha. Vijana hawaja changamka kabisa sijui kwa sababu ya rafidhi yao inawafanya wasichangamke, mi sijui.

Ukitembela wilayani, katani hata vijijini ndo kimya kabisa. UKIJA KWENYE FURSA ni nyingi mno. Kuna BAHARI, MISITU, MAZAO lakini sioni kama wanatolea macho ima viongozi au wananchi wenye. Ukiingia porini miti ya kutosha, matunda kama vile EMBE, boga zakutosha lakini zinaharibika tu aisee.

TATIZO LIKO WAPI?

VIONGOZI WETU WAMESHINDWA KUTUWEKEA NJIA ZA KUENDEA FURSA TULIZO NAZO?

AU NI SISI WENYEWE TUMESHINDWA KUZITUMIA NEEMA TULIZO PEWA NA MUNGU WETU?

UBINAFSI NA CHOYO NDIO INAYO DUMAZA MAENDELEO YETU.

EMU TUAMBIE UMEONA NINI LINDI?NA KIPI KIFANYIKE LINDI ILI KULETA MAENDELEO?
Elimu hi kitu muhimu sana. Kusoma na kuelimika. Sio kupata makaratasi tu
 
Hupendi ukweli? Nchi za Kiislam zilianza kupata maendeleo baada ya kugundua mafuta miaka ya 60 kati kati. Kabla ya hapo walikuwa kama watu wa Kigoma na Tanga tu, kushinda na kuvaa shuka siku nzima huku wakinywa kahawa na kulalamika.
Mkuu sasa naona unataka kulinganisha Waarabu na Wazungu!! Ingawaje mimi na wewe bila shaka imani yetu ni sawa na ile ya akina Trump, lakini sote sisi mbele ya akina Trump ni manyani tu, na kwahiyo tusikashifu Waafrika wenzetu kwa kuona hawa hoehae wakati sisi na wao hatuna tofauti yoyote kwa sababu utajiri wa Mkristo Mzungu katu hauwezi kuwa utajiri wa Mkristo Mwafrika!!

Hivyo basi, tuachanane na hao watu na badala yake turudi huku Afrika! Je, unataka kusema mataifa ya Afrika yenye Wakristo wengi ndo matajiri sana na yale yenye Waislamu wengi ndo maskini sana?! Ili kuweka kumbukumbu sawa, Tanzania tumezungukwa na mataifa ambayo majority ni Wakristo na yote hayo ni mataifa maskini!!! Sasa tuna tofauti gani na hao ndugu zetu Waislamu?!
 
Zao la nazi lindi vijijini usilisahau kuanzia Ng'apa mpaka Mtama ila linazidi kupotea. Mkakati uliopo ni kuinua zao kwa kuweka kiwanda cha Cocopeat na natumai muda wowote kitaanza kupiga kazi pale Ng'apa. Hii inaweza kuamsha hali na kuongeza nguvu kwa wakulima wa Nazi.
Mtoa mada umenena vyema. Changamoto kubwa iliyopo Lindi ni mzunguko mdogo sana wa kibiashara usioweza kuleta hamsha hamsha kwa vijana kuchangamkia fursa. Ni mkoa kwenye wageni wachache wanaoingia na kutoka.
Biashara kwa kiasi kikubwa inaendeshwa na wenyeji mwenyewe kwa wenyewe. Watu wanafungua biashara huku kodi za mapango zikiwa juu wakati biashara inafanyika kwa shida finally MTU anafunga.

Lindi hapana mulundikano wa vyuo ,hakuna kiwanda wala mradi wowote mkubwa wa kimkakati unaotekelezwa hapa. Kuwepo kwa hayo uchagiza population kubwa na kuchochea biashara na mzunguko wa fedha kuwa juu na hivyo watu kuchangamkia fursa mbalimbali kama ilivyo mikoa mingine.

Nenda kahama , Mz ,Moro. , Mbeya Arusha nk. Business ni 24h/7 wakati Lindi saa 12 hupati huduma yyte. na saa 3 asbh ndo biashara ufunguliwa. Nenda stand kuu uulizie vocha tu au supu au juice fresh uone kama utapata.

Pengine mkoa huu unahitaji kuwa engaged na mikakati mingi ya kiserikali mfano ujenzi wa viwanda , miradi mikubwa ofisi kuu za mashirika mbalimbali ngazi ya kanda badala ya kurundikana mtwara nyingine ziamie hapa. Tujenge matawi mbalimbali ya vyuo kadhaa hapa na lengo ni kuuchocheza mji kimaendeleo.

Nizungumzie suala la fursa za kilimo uvuvi na ufugaji bado pia fursa hizi watu hawajazitumia na ndio maana kutokea Kibiti/ Mohoro mpaka Mpapula mpakani na mtwara tunaona uwanda wa kijani wa misitu na mapori na hatuoni mashamba.

Ardhi yenye rutuba ipo maji ya kutosha kwa kilimo na mifugo kwa mazao yote tunayo huku tukishuhudia nyumba za tembe njia mzima. Utagundua pia kuna tatizo la jamii kutoengage vizuri nguvu kazi ili kujenga maisha bora ya mtu mmoja mmoja.

Kwa sasa wageni wengi waliopo na wengine wanakuja kuzikamata hizo fursa za kilimo uenda labda watachangia kuibadilisha jamii siku zinavyozidi kusogea.

Nawapongeza baadhi ya wazawa wanachapa kazi huko vijijini ukienda kanda za ndani utakubaliana na Mimi kuwa wanafanya kazi sana nyumba bora na mashamba makubwa ya korosho wanayo.
Yupo mzee mmoja anavuna tani 100 na wengine tano 40 za korosho kwa wastani kila mwaka. Hii ni fursa kubwa kwa uchumi wa wanalindi.

Kwa sasa mkombozi wa maisha ni Korosho na wapo waliofika mbali sana. Tatizo lipo bado kwa nguvu kazi inayokaa kando ya barabara wapo kwa kazi ya kuesabu gari za abiria zinazotoka na kuingia Dar.

Nawasilisha kwenu kwa ninayoyajua kuhusu Lindi.
 
Kuhusu utalii upo kwanza kwa majengo yaani Ancient buildings kwa maeneo ya kilwa pale,uwepo wa Mbuga ya Wanyama ya Selous katika wilaya za liwale na Nachingwea japo sina hakika kama hotel zimewekwa kwa maeneo husika licha ya kuwa nimeyatembelea sana na mwisho utalii wa ufukoni kuna beach nzuri sana kuanzia kilwa mpaka lindi mjini Ila beach bora inasemekana iko Mchinga pale
 
Mkuu sasa naona unataka kulinganisha Waarabu na Wazungu!! Tuachanane na hao watu na badala yake turudi huku Afrika! Je, unataka kusema mataifa ya Afrika yenye Wakristo wengi ndo matajiri sana na yale yenye Waislamu wengi ndo maskini sana?!
Tagsiri yako ya " mbantu yule yule was eneo moja" una maana gani.So unamaanisha mbantu ni mtu mmoja hivyo anafanana kwa nini wa hapa awe mzuri na pale awe mbaya.
Kwa ni ulikuwa una maana gani zaidi ya hiyo tafsiri?
 
Commercial farming bado Ila yapo na yanalimwa nenda Namupa Seminary,Ndanda mission na baadhi ya maeneo ya plateau za makonde na Rondo.
Sijamaliza study zangu ninazifanyia kazi na references ninazo mkuu ni masuala ya muda kuruhusu uwekezaji wa kibiashara.

Parachichi aina ya Hass tu ndio imeonyesha kufeli kwa 80%
Umeongea ukweli mtupu, ndo maana kuna mtu nimemwambia kama ulitarajia ukute Lindi au Mtwara wanalima maparachichi basi utakuwa na matatizo!! Tatizo la JF kila mtu anajifanya nyumbani kwao ni matajiri na anatoka mkoa wa kitajiri lakini cha ajabu mkoa wa Lindi na Mtwara una population ndogo sana lakini Tanzania ni miongoni mwa nchi maskini kabnisa duniani!! Sasa kama kwenye mikoa yao ni matajiri sasa sijui unakuwaje tena Tanzania ni maskini kwa sababu population ndogo ya kusini hawezi kuathiri average ya utajiri uliopo Tanzania.
 
Nafikiri Mh.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ndiye mzaliwa kindakindaki wa huko na walimkosakosa Rais wetu kupitia ule moshi wa kijadi anaupitia huu uzi na atakuja na mwarobaini wa hili bandiko lako mapema sana
 
Hapa umenenaa aisee Niko maeneo haya sijawah ona mwanamke wa maana wa kutetemesha .....ilaaa kuhusu kukata viuno sijui sababu sijahangaika kujihusisha nao

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
🤣🤣🤣
JF raha sana, haswa unapokutana na 'watasha' kama huyu..............anaonekana mambo safi, mzuri, anatoka sehemu bora na ni mtu wa viwango! safi sana!!!
 
kuna siku nimekwenda sokoni nikataka kununua samaki wote kwenye beseni...yule mama aligoma kwa sababu aliniuliza nikichukua wote yeye atauza nini wakati muda wa kurudi nyumbani bado haujafika...Dah Mtwara yetu bhana
ni aina ya vichekesho ambavyo nilianza kuvisikia tangu miaka ya 90 mwanzoni.......ni vijistori vya kujifurahisha ilikuwa, muda umeshaenda mkuu, achana na vijistori hivi!
 
🤣🤣🤣
JF raha sana, haswa unapokutana na 'watasha' kama huyu..............anaonekana mambo safi, mzuri, anatoka sehemu bora na ni mtu wa viwan
🤣🤣🤣
JF raha sana, haswa unapokutana na 'watasha' kama huyu..............anaonekana mambo safi, mzuri, anatoka sehemu bora na ni mtu wa viwango! safi sana!!!

go! safi sana!!!k
Hivi mkuu unafikiri mtu alie kulia masaki na kankoko kigoma watafanana kweli.
Nilipotoka Dar kwenda mbeya kwa Mara ya kwanza sikuyaamini macho yangu watu niliokuwa nawaona.kila mwanamke nilikuwa namuona mweusi ti,tipwatipwa, nikaa na assume wanawake wa mbya "wabaya".Baadae nikawazoea nikawa nawaona kawaida tu. Usibishe tunatofautiana kuona watu.
Wanaume wa Tanga utawafananisha na wa Njombe kimuonekano? Wamaume wa Tanga laini laini lakini wa Njombe kama wamekula chumvi sura ngumu!!
 
Kuna mambo ambayo ukiwa nje ya hii mikoa tukikuambia unaweza sema tunadanganya ila njoo mzee uone utofauti wa kusini na kwingine tena bora umakondeni, mtwara na sio umwerani lindi.
mh, kiongozi unavyoongea utafikiri ni wewe pekee uliyeishi lindi au mwenye uwezo wa kufanya research..........mi ni mmoja ya watu ambao tunaifahamu lindi vizuri tu na mikoa mingine kadhaa. punguza hisia na chuki kaka, vitakuweka huru. au kama vipi changamkia au lete watu wachangmkie hizo fursa bwerere ulizoziona kaka!!! tuwe tu wakweli wakati mwingine
 
Hivi mkuu unafikiri MTU alie kulua masaki na kankoko kigoma watafanana kweli.
Nilipotoka Dar kwenda mbeta kwa Mara ya kwanza sikyamini macho yangu watu niliokuwa nawaona.kila mwanamke nilikuwa namuona mweusi,tipwatipwa, nikaa na assume wanawake was mbdya "wabaya".Baadae nikawazoea nikawa nawaona kawaida tu. Usibishe tunatofautiana kuona watu.
Wanaume wa Tanga utawafananisha na wa Njombe kimuonekano? Wamaume wa Tanga laini laini lakini wa Njombe kama wamekula chumvi sura ngumu!!
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣🤣
haya bwana!
 
Mtoa mada umenena vyema. Changamoto kubwa iliyopo Lindi ni mzunguko mdogo sana wa kibiashara usioweza kuleta hamsha hamsha kwa vijana kuchangamkia fursa. Ni mkoa kwenye wageni wachache wanaoingia na kutoka.
Biashara kwa kiasi kikubwa inaendeshwa na wenyeji mwenyewe kwa wenyewe. Watu wanafungua biashara huku kodi za mapango zikiwa juu wakati biashara inafanyika kwa shida finally MTU anafunga.

Lindi hapana mulundikano wa vyuo ,hakuna kiwanda wala mradi wowote mkubwa wa kimkakati unaotekelezwa hapa. Kuwepo kwa hayo uchagiza population kubwa na kuchochea biashara na mzunguko wa fedha kuwa juu na hivyo watu kuchangamkia fursa mbalimbali kama ilivyo mikoa mingine.

Nenda kahama , Mz ,Moro. , Mbeya Arusha nk. Business ni 24h/7 wakati Lindi saa 12 hupati huduma yyte. na saa 3 asbh ndo biashara ufunguliwa. Nenda stand kuu uulizie vocha tu au supu au juice fresh uone kama utapata.

Pengine mkoa huu unahitaji kuwa engaged na mikakati mingi ya kiserikali mfano ujenzi wa viwanda , miradi mikubwa ofisi kuu za mashirika mbalimbali ngazi ya kanda badala ya kurundikana mtwara nyingine ziamie hapa. Tujenge matawi mbalimbali ya vyuo kadhaa hapa na lengo ni kuuchocheza mji kimaendeleo.

Nizungumzie suala la fursa za kilimo uvuvi na ufugaji bado pia fursa hizi watu hawajazitumia na ndio maana kutokea Kibiti/ Mohoro mpaka Mpapula mpakani na mtwara tunaona uwanda wa kijani wa misitu na mapori na hatuoni mashamba.

Ardhi yenye rutuba ipo maji ya kutosha kwa kilimo na mifugo kwa mazao yote tunayo huku tukishuhudia nyumba za tembe njia mzima. Utagundua pia kuna tatizo la jamii kutoengage vizuri nguvu kazi ili kujenga maisha bora ya mtu mmoja mmoja.

Kwa sasa wageni wengi waliopo na wengine wanakuja kuzikamata hizo fursa za kilimo uenda labda watachangia kuibadilisha jamii siku zinavyozidi kusogea.

Nawapongeza baadhi ya wazawa wanachapa kazi huko vijijini ukienda kanda za ndani utakubaliana na Mimi kuwa wanafanya kazi sana nyumba bora na mashamba makubwa ya korosho wanayo.
Yupo mzee mmoja anavuna tani 100 na wengine tano 40 za korosho kwa wastani kila mwaka. Hii ni fursa kubwa kwa uchumi wa wanalindi.

Kwa sasa mkombozi wa maisha ni Korosho na wapo waliofika mbali sana. Tatizo lipo bado kwa nguvu kazi inayokaa kando ya barabara wapo kwa kazi ya kuesabu gari za abiria zinazotoka na kuingia Dar.

Nawasilisha kwenu kwa ninayoyajua kuhusu Lindi.

Umenena vyema.
Uwekezaji wa kimkakati unatakiwa Lindi Ili kuchochea fursa
 
Upatikanaji wa ardhi kubwa kwa pamoja labda hekari elf 50 au laki kwa ajili ya kufungua estates za kilimo na ufugaji wa kisasa vipi inawezekana kupata.
 
Back
Top Bottom