Wazanzibari walioko Tanganyika waorodheshwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibari walioko Tanganyika waorodheshwe!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by masopakyindi, Jun 24, 2012.

 1. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Mambo yanavyoendelea huko visiwani na hatma ya muungano ni swala linaloendelea kuleta wasi wasi kwa Watanzania walio wengi.

  Suala la hivi karibuni la kuchoma moto makanisa zidi ya manne limetia doa kubwa katika "udugu" uliokuwepo kati ya Bara na Visiwani.
  Licha ya matamko ya kulaani vitendo vya kupinga muungano, harakati hizo zimekuwa zikirndelea, tena wazi wazi.

  Tanganyika tusije bweteka na hali hii na tukajikuta tumelea mahasimu ambao siku ya siku inakuwa vigumu kuwa tambua.

  Leo Kenya wanatatizo hilo na Wasomali.
  Mwaka 1939-45 wajerumani wote waliorodheshwa humu Tanganyika ili iwe rahisi kidhibiti vitendo vyao, ulipoingia utawala wa Kiingereza.

  Ni vyema na sisi leo tukafanya hivyo ili kudhibiti lile kundi linaloitwa" the 5th column".

  Wakuu tuchangie katika hili, tusije lia kilio cha mjukuu.
   
 2. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  hivi Wanzanzibar kuchoma Makanisa wana maana kwamba Wabara wengi ni Wakristo au wana maana ipi?
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wataorodheshwa kama muungano ukivunjika tena kue kabisa na VISA. mzenji akitaka kuja bara anaomba visa
   
 4. T

  Taso JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Wazanzibar wanaoishi Tanganyika wapewe grace period ya siku 180 ya kujiandikisha kuwa naturalized citizens wa Tanganyika au wawe wameomba na kukamilisha kibali cha ukazi wa muda kwa mujibu wa kile kitakachokuwa kimemuweka Tanganyika, kazi, utalii, biashara, au transit visa ya kuunganisha ndege, maana hata kiwanja cha ndege kumbe hawana, wakitaka kusafiri yabidi waje Dar. Wakikaidi tunaanza kuwakamata mipakani kama wasomali. Mpaka siku wataombea warudi kujiunga kama mkoa. Zanzibar ilibidi iwe mkoa, mbona mimi niko proudful na Utanzania kuliko kwetu Lindi?

  Watuache tupumue, tumechoka kubeba zigo la Zanzibar.
   
 5. a

  adolay JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Kwa upande wangu siamini sana kwamba kuchoma makanisa kunauhusiano wowote na Kuvunja muungano

  Kama ndivyo misikiti pia ingechomwa (kwasababu waumini wa muungano ni wa imani zote)

  Ofisi za serikali pia zingechomwa (kwa sababu ndio walioziba pamba masikioni kutatua kero za muungano)

  Muungano si kati ya zanzibar na makanisa, ukristu ni imani kama imani zingine zozote. Kwanini makanisa?????

  Ninachokiona hapa ni ubaguzi wa kidini kwa wale wanaoamini na kuaminishwa kwamba mfumo katoliki, mfumo kristu, makafiri nk ndio wanoididimiza zanzibar na huu ni uzushi na uongo mkubwa. Somalia, syria, Tunisia nk nako kunamfumo katoliki????? Mbona amani imetoweka huko?

  katika hili waislam wenye hekima zao na busara hawamo kabisa, bari vijana na malimbukeni wachache wanaoamini kabisa siku moja tanzania itatawaliwa kwa sharia law kwa mujibu wa mahakama ya kadhi, sio hivyo tu wanaamaini pia dunia nzima wataweza kufanya hivyo. Hii ni zana ya watu waliokosa maarifa, hekima wala busara, hawaoni mbali wala karibu kwa mustakabali wa taifa, familia za wakati huu wala vizazi vijavyo.

  Narudia tena uislam ni amani na waislamu wastaarabu wamejaa inchini kote na tunaishi nao kila siku kwa amani, ushirikiano na undugu. kibaya nipale kinazuka kikundi kikichochea na kuwawahadaa watu wema kwamba waislamu wanaonewa, mfumo katoliki, balaza la mitihani, mara masuala ya sensa, mgawanyo wa madaraka nk.

  Hapa kinachokosekana ni hekima ya Rais wetu kutafuta suluhisho mapema iwezekanavyo kuhakikisha amani ya tanzania haiwekwi rehani na watu wenye malengo ya kutugawa kwa itikadi za dini zetu na kwa malengo na dhana potofu.

  Kuswali na kusali ni haki ya msingi kwa kila mtanzania na serikali inawajibika kujenga mazigira yatakayopelekea kila mtanzania kuwa na uhuru kamili katika kuabudu iwe kuswali au kusali. Serikali ihakikishe hakuna matabaka ya kiimani miongoni mwetu, asiwepo wa kujiona yeye imani yake ni bora kuliko ya mwingine.

  Naamini kama serikali ingepiga marufuku kwa vitendo kashifa za kidini na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaoacha mahubili kwa maana ya vitabu vyao na kukejeri imani zingine mbegu ya ubaguzi wa imani haitatapakaa, lakini sasahivi serikali imejitoa nakuacha watumishi wa mungu kufudisha kwa kuchojoana, kuchoea vijana na upotoshaji.

  Mwisho kwa haraka haraka naiona hatari mbele yetu, Ni rahisi kuchoma makanisa na kuwatimua wakristu kule zanzibar, ifahamike kwamba huku tanganyika wazanzibar wanaoishi kwa amani, wakifanya biashara zao kwa uhuru kabisa watalazimika kurudi nyumbani na hapa ndipo ninapoiona hatari yenyewe, kule tanga, pwani kigamboni na kwingineko tanganyika yote.

  Watanganyika kwa umoja wetu tutaungana kudai haki yetu baada ya kubaguliwa na anayedhani tumelala anakosea. kama tunavunja muungano tufanye kwa amani uchomaji wa makanisa unaingiaje?

  Wapo wanaojenga hoja dhaifu na za kipuuzi kabisa kwamba waliochoma makanisa ni wakristu na wachungaji wao, wanachoma ili iweje? kama ni kichaa ni wakristu wa huko zanzibar tu wameehuka kuchoma makanisa yao mbona huku tanganyika hakuna hicho kichaa? wengine wanasema kwa sababu misikiti inachomwa ndio sababu, ukiuliza mingapi wapi na ulinganifu ukoje hakuna majibu ya msingi zaidi ya kupayuka, kuweka reference zilizopitwa na wakati wakati hata maudhui ya video na refrence hizo iko inje kabisa.

  Ni upuuzi kushabikia ubaguzi wa aina yoyote, lakini kama tatizo ni muungano kwanini makanisa????

  Alshababu walianza kwa utaratibu na njia kama hizo

  Historia ya boko haramu ilianza hivyo utaona mpaka sasa ugonvi wao si serikali as per say wanachoma na kuwauwa wakristu kila siku huko nigeria.

  Hatulazimishi muungano ikibidi tuuvunje lakini swali linabaki palepale makanisa kwa nini???
   
 6. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Kadri siku zinsvyosonga mbele, na katika miaka hii ya karibuni tofauti za mitizamo katika mambo mengi kati ya Tanganyika na Zanzibar imekuwa kubwa.
  Hadidu rejea ya muafaka kati ya Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe kuunda Serikali yao ni kitendawili kwa hata wana CCM wa ngazi za juu Dodoma.
  Kwa wengi wetu hilo bado si tatizo.
  Tatizo lililojitokeza ni pale muafaka huo ni wa kuua muungano, na hata hivi karibuni fujo zilizojitokeza Zanzibar na makanisa kuchomwa moto na wan Uamsho, SMZ ilijikongoja sana kuthibiti na hata kutoa tamko.
  Kwa mtu mwenye akili hapo anajua unatekelezwa muafaka.
  Kwa waTanganyika tuliomo gizani, ni heri kuchukua tahadhari before it is too late.
  Kuorodhesha wazanzibari walioko Tanganyika ni muhimu.
   
 7. Dogo1

  Dogo1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,102
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Aliyetoa hoja kwamba wazanzibari walioko tanganyika waorodheshwe ni maskini wa habari kwa sababu hajui kwamba sasa haivi idadi ya watanganyika walioko zanzibar ni karibu nusu ya wakazi wote zanzibar. So yeyote anaezungumzia suala la kuvunja muungano asidhani madhara yatawapata wazanzibari walioko bara, but hata watanganyika walioko zenji wataumia pia.

  Ni vema mada nyengine mnazozianzisha na kuchangia mtumie busara zaidi na uhalisia badala ya ushabiki. Ni kweli wazenje wameenea bara but also wabara wako kila kona ya zenji, so chunga sana!

  Kwa ni mnashabikia kuchomwa makanisa bara na mnakaa kimya kinapochomwa kiwanda cha kuchapisha kitabu kitukufu cha Qur'an hapa dar? Au kwa vile tukio hilo lilitokea bara? Ndio tuseme waliofanya hivyo wanataka waislamu walioko tanganyika watafute nchi yao au tuigawe tanganyika ya wakristo na tanganyika ya waislam kama ilivyotokea India na Pakistan then katika mtafaruku wao ikazaliwa Jammu and Kashmir ambayo hadi leo kuna mzozo baina India na Pakistan.

  Tushabikie maelewano badala ya mifarakano. Wewe uliyeko Lindi huyajuwi yanayotokea dar wala zanzibar. Zaidi ya hayo usitambe sana na utanganyika wako coz hata kule Newala imebainika wapo wakenya wa kabila la wagunya ambao walikuja miaka mingi wakifanya biashara ya dagaa wakaoa na wakazaa watoto, usishangae ukijikuta wewe si raia wa tanzania!
   
 8. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Tuwaache tu kwa tukishavunja muungano watatuingizia kipato kwa kulipia vibali vya kufanyia kazi. Pia sheria za Tanganyika hazikuwa zinaruhusu wageni kumuliki ardhi so kuna uwezekano wa kupata viwanja na mashamba ya SANDAKALAWE AMINA
   
 9. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mpaka sasa hakuna ushahidi kamili kuwa wananchi walioandamana ndio waliochoma makanisa serikali nyingi na si ya tanzania tu,kuchafua malengo ya wapinzani au waandamanaji ni jambo la kawaida.
   
 10. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe na al-shabab una tofauti gani??!!
  yani wenzako wachume kwa jasho lao wewe utegemee sadakalawe kwenye mali zao,akili hizi au pumba??!!
  watu walivyopinda sasa hivi hawatoneemeka na mali wao wala wewe watakumwaga machango nje!na litakalo kuwa na liwe!
   
 11. a

  adolay JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  mkuu naungana nawewe tushabikie maelewano badala ya mifarakano big up.

  Lakini umenisikitisha inamaana makanisa yanachomwa kwa sababu kitabu kitukufu kilichomwa?

  Sijakuelewa vema maelewano unayoamanisha ni kama yale ya wahindi? au unamaana gani? ubaguzi wa dini au?

  kwamtazamo wako kwasababu watanganyika wengi zenji ndo mnawafukuza? japokuwa si kweli kwamba watanganyika wanakaribia nusu ya wazanzibar huko zenji.
   
 12. Dogo1

  Dogo1 JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,102
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  maana yangu ni kwamba machafuko ya kidini na kiitikadi hayachagui bara wala znz, muungano au kutokuwepo muungano, kikundi cha watu wachache wakiamua kuitia dosari amani hufanya hivyo.

  Nadhani viongozi wa makundi yote ya kijamii wawahubirie waumini na wafuasi wao juu ya kuvumiliana، kuheshimiana, na kuheshimu haki za kila mmoja.
   
 13. a

  adolay JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280

  Nimekuelawa mkuu
   
 14. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Tena hii ni murua kabisa maana hao Watanganyika walioko Zanzibar wote watapewa ardhi kule Madale, na wataenea katika jiji la watu milioni 4 la Dar es salaam.
  Wazanzibari walioko Tanganyika hata kama wako watano au milioni, ni lazima waanze kufungasha kurudi kwao.
  Wengine wamejenga maghorofa wakijuafika nchi hii si yao.
  Muungano ukuvunjika hata kwa kuogelea mtarudi kwenu tu.
   
Loading...