Wazanzibari wajipanga kuishitaki Tanganyika

Wazanzibari wajipanga kuishitaki Tanganyika

TIGOPESA

Senior Member
Joined
Apr 2, 2014
Posts
190
Reaction score
64
Hati halali ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haiko UN, kuna ya Tanganyika tu,ambayo Nyerere aligushi mambo mengi .
Hati ya Zanzibar ni ile ya Muungano wa Muda wa miaka 10 tu , lakini kwa undumi la kuwili wa Juliasi hio hati hakuipelekwa UN na kilichopelekwa ni hati ya upande moja tu wa Muungano Tanganyika .

Lakini yote hayo na vielelezo vitatolewa hapo Wananchi wa Zanzibar watakapo fungua case na kuangaliwa uhalali wa Muungano huu
na Vitisho vya Nyerere na Uhaini wa Kujadili Muungano kwa kipindi chote hicho cha Muungano.
Wazanzibar njia ya Muongo ni fupi na mara zote uongo hauwezi kushinda ukweli hata ukaie miaka 100 lakini ukweli utakujaa juu tu, Nyerere alihisi Wazanzibar ni wajinga na niwatu wa kuburuzwa tu.

Tukija katika Wahusika wa Muungano ?,

Wahusika wa Muungano sio Piusi Msekwa pekeyake tu,wapo wahusika vile vile kwa upande wa Zanzibar na walikua wana nafasi nyeti katika Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Mfano Mzee wetu Abdallah Rashid alikua katibu mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Mzee Hassan Nassor Moyo mbona hamuwaiti hawa mukawahoji ?.

Lakini kinacho Shangaza wengi nikua watu muhimu wa liiobakia ni Piuse Msekwa tu? Vipi Upande wa Zanzibar Abdallah Rashid na Mzee Moyo?. Au hamuwataki hao kwakua na itikadi tafauti na zachama , hili si swala la kichama linahusu mustakubali wa mataifa mawili yalio unganicha nchi zao.
Maana kuulizwa Msekwa Peke yake ni kuchukua maoni ya upande mmoja tu wa Muungano haliyakua nchi ni mbili zilizo ungana na watu wapande hizo mbili ?.

Hili ni jambo kubwa linalo wahusu watu wote wa pande mbili za Muungano kujua na sio itikadi za chama hapa ,sasa kuridhika na maneno ya Msekwa tu sio solution ya Ukweli .

Nyerere na Mwenye kujadili Muungano ni Wahaini .
Wale wenye kusema kwa mujibu wa Sheria ,Muungano unaweza kuwa halali kwa vile umedumu kwa kipindi kirefu ? Hapa hawakwenda mbali kufafanua uhalali wenyewe , Jee unaweza kufanya negotiation na Mfungwa asie uhuru hata wa kutoa maoni na mawazo yake binafsi ?

Muungano umeishi kipindi chote hicho sio kwa ridhaa ya wananchi ,ni kwa viticho vya watawala na kuvitumia vyombo vya dola kukandamiza wale wenye kupinga Muungano hata kwa kutoa maoni yao huru.
Wako walio tiwa magerezani, wako fanywa vilema na wako walopoteza maisha yao kwa kwenda kinyume na Nyerere kwa kisingizio hichi hichi cha Muungano .

Kwa hio hakuna Sheria ya kukandami na kuchurutisha ,halafu ukasema ni halali kwa Mujibu wa Sheria, Huu Muungano tokea awali Nyerere alitumia vitisho na ndio ukaweza kukubalika kuwepo mpaka leo.
Na vitisha hivyo vilisibitisha zahiri kua huu ulukua ni Muungano wa kimabavu na ulahai tu, wakutumiaa ujanja ujanja na nguvu zakuwazibiti wale wenye kwenda kinyume .

Na mpaka hivi sasa mundo huu wa Muungano unadumu zaidi ki siasa kwa kunganishwa ccm Bara na ccm Zanzibar, lakini kwa ridhaa bado hauna ridhaa na ndio ukaona hata tume ya Jaji Warioba ilipewa sindikizoo lakua usiguswee au kujadiliwaa .
Mpaka watu walipokuja juu ndio ukajadiliwa lakini hata hivyo ujadili wenyewe ni kuboresha na kufanywa eti ni tunu za Taifa?.
Sasa ikiwa Muungano huu ni wa ridhaa ya watu wa pande mbili , kuna hofu gani kwa wananchi wasi ulizwe ? Si ujadiliwe kwa kuulizwa wananchi wanautaka au hawautaki ,wanaogopa nini? Lakini hofu kubwa ni kua Nyerere ali kushi na viongozi wanajua hilo .
Nandio hata huo waraka wa Muungano uloko UN tukiashana na kua ni waupande mmoja wa Muungano lakini vile vile Viongozi wa

Tanganyika wanaona aibu
kuonyesha au kutoa katakana na mambo yalioingizwa kinyemelaa na upande mmoja.
Lakini hayo yote tutayaona mbeleni ya case zidi ya Muungano huu kutarishwa na kujua ukweli wa HATI ya Tanganyika iloko UN na hati walonazo wasisi na vigogo Zanzibar .

Samuel Sitta na mfano wa hati ya Muungano na cheti cha Ndoa .
Huyu mzee anachukulia mambo haya ni simple tu ,au kuleta zarau na kuona wamesha zowea kuwaburuza Wazanzibar kwa misingi ya kichama ,kwa hili yaguujuuu , ikiwa mumezowea kuiba majimbo ya kura hili halihusiani na hayo .
Kwa tarifa yako hili halitoishia tu kwenye Bunge la Katiba , Wazanzibar wataendelea kufungua kesi ndani ya nchi na nje ya nchi na jambo hilo linafanyiwa kazi . Iko kesi katika mahkama ya Zanzibar Iliofunguliwa na Wazanzibar akina Rashid Adye na vielelezo V-engine vitatumika vile vile na kuongeza V-engine.
Ile kesi ipoo kwenye mahakama ya Zanzibar na hivi sasa Wazanzibar wanajipanga kufungua ya kimataifaa ,kwa hio ukweli wa jambo hili utawekwa wazi na ikiwa mutababaisha kwa kesi za ndani lakini za Kimataifa hili jambo litakua ni series issue .

M/mungu ibariki Zanzibar na watu wake.
 
Haya!!!!!!!!! yetu macho. hiyo kesi itakuwa ya siri au ya wazi? au mashtaka na mashauri ya kesi yatakuwa siri halafu hukumu I we wazi? Napita turn jamani.
 
ni kesi ya wazi mkuu.msimamo wao ni mmoja.wanataka ipigwe kura,wanaotaka MUUNGANO na wasioutaka.maana wanavosema Muungano ulikuwa ni wa miaka kumi,na KARUME alikufa kabla ya hio miaka 10 kuisha,ni Tanganyika ndio waliomuuwa KARUME,maana kabla ya kufa KARUME alikuwa hasemi na Nyerere,na ndio maana hata hio HATI ya Muungano iliandikwa kwa muda wa miaka kumi tu,na sio Maisha.
Haya!!!!!!!!! yetu macho. hiyo kesi itakuwa ya siri au ya wazi? au mashtaka na mashauri ya kesi yatakuwa siri halafu hukumu I we wazi? Napita turn jamani.
 
me natamani wapewe nchi yao fasta.
tukomae kujenga hapa kwetu
 
Tanganyika ipi ya kushtakiwa? Hata Zanzibar yenyewe yenye Rais wake huwezi kuishtaki kuwa ilishapoteza International Legal Personality yake!
Anyway, kama wanataka kujifurahisha tu na kutafuta cheap popularity wafungue hako kakesi!
 
ni kesi ya wazi mkuu.msimamo wao ni mmoja.wanataka ipigwe kura,wanaotaka MUUNGANO na wasioutaka.maana wanavosema Muungano ulikuwa ni wa miaka kumi,na KARUME alikufa kabla ya hio miaka 10 kuisha,ni Tanganyika ndio waliomuuwa KARUME,maana kabla ya kufa KARUME alikuwa hasemi na Nyerere,na ndio maana hata hio HATI ya Muungano iliandikwa kwa muda wa miaka kumi tu,na sio Maisha.

Mkuu fuatilia mambo, Karume aliuawa na Mwarabu ambaye alilipiza kisasi cha kuuawa baba yake na Karume! Hata kama mnawachukia hao mnaowaita "Watanganyika" msiwasingizie mabaya!
 
Haya!!!!!!!!! yetu macho. hiyo kesi itakuwa ya siri au ya wazi? au mashtaka na mashauri ya kesi yatakuwa siri halafu hukumu I we wazi? Napita turn jamani.

Mkuu hakuna kesi hapo, endelea na shughuli zako za kujitafutia kipato!
 
Waache unafiki kwa nini wanaipigia kura ccm wakati hiyo ndiyo symbol ya muungano(tanu/asp) anzeni kumshitaki nahodha na ali karume
 
Mkuu hakuna kesi hapo, endelea na shughuli zako za kujitafutia kipato!

Buchanan inamaana huamini katika lisemwalo lipo na kama halipo laja? Mbona walisema CCM itashinda Kalenga na Chalinze na ikawa? ila mm napita tu yangu macho
 
Wapewe nchi yao tuu ImageUploadedByJamiiForums1396886702.006247.jpg
 
Buchanan inamaana huamini katika lisemwalo lipo na kama halipo laja? Mbona walisema CCM itashinda Kalenga na Chalinze na ikawa? ila mm napita tu yangu macho

Usilinganishe suala la Tanganyika kushtakiwa na uchaguzi wa Chalinze/Kalenga, havifanani kabisa!
 
Buchanan unadharua wewe, waswahili usema mdharau mwiba mguu uota tende!!
Zanzibari kuna chuki ya wazi kwa Watanganyika, ikiwa tutaendelea kungangania huo muungano boya,
Siku moja tutapokea majeneza ya vijana wetu wa JWTZ naPolisi!!
Kama MaCCM wanadhani muungano ni unapendwa ZNB, waitishe refrendum, kura ya maoni, waondoe udhia!!
 
Last edited by a moderator:

Mimi sina dharau hata kidogo! Wazanzibari kama unafikiri chuki waliyo nayo itaondolewa na uwepo wa Serikali 3 umekosea vibaya sana! BTW: Ni afadhali kuwa na Muungano "Boya" (Serikali 2) kuliko Muungano "hewa" yaani Serikali 3!
 
mtanichukia bure, huu muungano hakuna miaka 10 ijayo
 
Ajabu unashitaki nchi ambayo haipo!! sasa nani atasimama mahakamani?
 
Mkuu fuatilia mambo, Karume aliuawa na Mwarabu ambaye alilipiza kisasi cha kuuawa baba yake na Karume! Hata kama mnawachukia hao mnaowaita "Watanganyika" msiwasingizie mabaya!

Kumekua na hii hadithi ya kuwa muuaji wa karume Humoud alilipa kisasi cha kuuliwa baba yake na Karume...huu ni uongo mwengine kuficha kisa kizima cha kuuliwa Karume.
Baba yake Humoud huyo mwarabu unayemsema alikamatwa kwa kesi ya mauaji ya kiongozi mmoja aitwaye Mugheir..inasemekana alimchoma kisu mbele ya hadara na hii ilikuwa ni kabla ya Mapinduzi..
Kesi yake ikaendeshwa na serikali iliyokuwapo chini ya muingereza na baba yake akahhukumiwa kifo
Wakati hukumu inatolewa katika kipindi kifupi znz ikapata uhuru wake na baada ya mwezi mmoja mapinduzi.
Humoud akiwa mwanajeshi alikua upande wa kina karume kwenye mapinduzi .kama yalivyo mapinduzi ya kumwaga damu basi wafungwa huwa wanatilowa kwa lengo la kujiunga na movement ya mapinduzi na walipotolewa jela baba yake humoud hakuwa mmoja ya alie tolewa kwani hukumu yake ya kuuwawa ilishatekelezwa kabla ya mapinduzi.
Hivyo karume hahusiki na ndio maana karume hakuwa na wasi wasi na humoud na humoud naye hakua ma chuki na karume kwa sababu ya baba ake..
Hivyo muuaji wa karume alikua na motives nyengine nje ya hizo
 
Back
Top Bottom