Wazanzibari: Rasimu imetupuuza!

wazanzibari wengi wamesikika wakiiponda rasimu ya katiba mpya iliyozinduliwa jana na makamu wa rais,dr.mohamed gharib bilal. Sehemu kuuw aliyoilenga ni ya uwepo wa serikali tatu: Serikali ya jamhuri ya muungano watanzania,serikali ya tanzania bara na serikali ya zanzibar.

'tulichotaka ni zanzibar kuwa na mamlaka kamili na yenye vyombo vyake vyote huru vya dola kama jeshi,polisi na mahakama.pia tulitaka,kama kutatakiwa muungano, basi uwe muungano wa mkataba. Serikali tatu hazina maana yoyote kwetu.hatukusikilizwa.tumepuuzwa. Hatutakubali' wamesikika wazanzibari mbalimbali walihojiwa na vyombo mbalimbali vya kimataifa kama bbc,dwna voa jioni hii.

ni kweli wazanzibari hawakusikilizwa? Can we dare to let zanzibar go now?

mzee tupatupa wa lumumba,dar es salaam.
yeyote anayegusa muungano huenda na maji by sheikh ilunga
 
Wazanzibari wengi wamesikika wakiiponda Rasimu ya Katiba Mpya iliyozinduliwa jana na Makamu wa Rais,Dr.Mohamed Gharib Bilal. Sehemu kuuw aliyoilenga ni ya uwepo wa Serikali tatu: Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania,Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Zanzibar.

'Tulichotaka ni Zanzibar kuwa na mamlaka kamili na yenye vyombo vyake vyote huru vya dola kama jeshi,polisi na Mahakama.Pia tulitaka,kama kutatakiwa Muungano, basi uwe Muungano wa Mkataba. Serikali tatu hazina maana yoyote kwetu.Hatukusikilizwa.Tumepuuzwa. Hatutakubali' wamesikika wazanzibari mbalimbali walihojiwa na vyombo mbalimbali vya kimataifa kama BBC,DWna VOA jioni hii.

Ni kweli Wazanzibari hawakusikilizwa? Can we dare to let Zanzibar go now?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.

Kwani si Katiba itapigiwa kura ya maoni - basi wasubiri wakati huo ili wapige kura ya kuikataa. kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala. mamlaka kamili mana yake nini??
 
Mbona
Jusa aliunga mkono fasta fasta!
Mi nadhani tuvunje alafu tupeane saa 12 kila mtu kwao! Full stop watu wamejazana bara kuanzia wababu, wabii, wamama, wa baba,wajukuu, vitukuu mpaka vilembwe! Waende zao waanze kuja na pasport
 
Sasa nyie serikali tatu, si moja ndo yenu? Au mlitaka nini. Mlitaka muendelee kutunyonya? Eti dola kamili ndani ya serikali ya Tanzania au? Tumechoka kuwabeba, basi tu hamkujua. Mlidhani tutang'ang'ania muungano wa serikali mbili? Tumechokaje? Bahati nzuri ni ninyi mliotaka kushuka kutoka mabegani mwetu.. Japo tulikuwa tumechoka kuwabeba.. kama ndugu hatukuwa tayari kuwatua chini.. ili msiteseke.. ili msibaguane ninyi kwa ninyi, ili tubaki wamoja kama Tanzania. Mungu mkubwa sasa tunatumaini kupata ahueni. Ni serikali tatu. Moja yenu, moja ya kwetu na moja ya wote. Maana ile keki tuliyokuwa tunagawana, nasi tunaambulia robo, sasa walau nusu. Maana tulikuwa tunagawana keki nusu, afu ile nusu yetu tunagawana tena na ninyi, sisi tunabakiwa na robo, ninyi robo tatu. Sasa je? Mtoto akililia wembe mpeeee... Yaani tunavyosubiri kwa hamu siku hiyo...
 
Hawa watu ni wakuwazibiti mapema sana hizi damu za kisultani hazina maana..
Tatizo tnatengeneza katiba tukiwa na Rais dhaifu sana!
 
nawaungamkono wazanzibari hawa please msikubali kupuuzwa

Serikari tatu sio suluhisho la kutokomeza kero za Muungano Tiba ni wananchi waungane kuwa wamoja na kuunda serikari moja imara au utawala Wa Magavana mmoja atawale Zenji na mwingine Bara na Rais awe mmoja aishi Dodoma vinginevyo Watawale mawaziri wakuu Tu Bara na visiwani kisha Rais awe mmoja tu huko USA MA UK TAWALA ZA AINA HIZO NI ZA AMANI NA MAENDELEO .SERIKARI TATU NI MZIGO KWA WALIPA JODI
 
Ohh!
Nina hakika hii rasimu ina mambo mengi tu ya kuwakwaza Watanganyika! badala ya Watanganyika nao kuangalia wapi pa kupigania yale yanayowakwaza wanawashupalia Wazanzibar wanaolalamikia ya kwao katika rasimu.

au Watanganyika wanakubaliana na yote yaliyopo kwenye rasimu?! kwa staili hii ni rahisi sana kwa kiongozi yoyOte yule kuwakokota Watanganyika namna anavyotaka, kwa sababu huu ni UDHAIFU mkubwa unaoonyeshwa na Watanganyika.
 
Tena suala la ARDI LISIWE LA MUUNGANO.. Ili muanze rasmi kuachia ardhi huku bara
 
Serikari tatu ni utawala Wa kianologia sana hauna nafasi katika Dunia hii ya Digtal
 
Walitakiwa kuungana na CHADEMA kudai mabadiliko stahiki ya sheria ile ya mabadiliko ya Katiba.

Wao walikuwa busy kuwatukana/kuwadhihaki CHADEMA.

Sijui kama wanafahamu wanachotaka.

Niliandika hapa JF mwaka jana ndoa ya CUF na CCM itavunjikia kwenye suala la kura ya maoni ya katiba mpya, tusubiri tuone, uchafu ulifichwa chini ya kapeti
 
let them go if they seemed they are humiliated kwani kwa tz bara hatuwezi tukagawana mapato na mkoa na bado wanalalamika tu kutokana na elimu duni na umaskini wao LET THEM GO AND SOON THEY WILL DISINTERGRATED INTO TWO POOREST COUNTRIES OF PEMBA AND UNGUJA and this will paved way to alqaeda and other terrorist group in zanzibar, let them go ukibebwa jibebe.
 
Ni kweli kabisa Rasimu hii ya katiba imewaongezea Mzigo Wazanzibari.Kwanza,itabidi Wazanzibari waondoke kwenye Idara zote zisizo za Muungano.Pili,Itabidi waanze kulipia gharama zote walizokuwa wakizipata kwa Mgongo wa Muungano.Tatu,Zanzibar itatakiwa iingie gharama ya kuihudumia serikali Kuu ya Muungano na sio kupokea Ruzuku kama ilivyo sasa.Wazanzibari walibipu,tumewapigia. USHAURI:Napendekeza waikubali hii Rasimu ili iwe njia rahisi ya kujitoa katika Muungano kwa kugoma kuchangia Gharama za Serikali Mpya ya Muungano.
kumbe kelele zote zile walikuwa wanatishia nyau?
 
Mkataba maana yake ni nini? Kwangu mimi ni aidha serikali moja au hakuna muungano kitu ambacho Zanzibar wanaomba usiku na mchana wajitenge. Choko choko yoote ktoka Zanzibar ni kujitenga na kwa nia hiyo wanabeza wazi wazi mchango mkubwa kutoka bara. Mpe mtu roho yake inapenda.
 
Back
Top Bottom