Wazanzibari kuajiriwa Tanganyika (Bara) ni sawa?

Wazanzibari kuajiriwa Tanganyika (Bara) ni sawa?

FreedomTZ

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2012
Posts
1,104
Reaction score
251
Nimefuatilia tangazo la TAMISEMI kuhusu ajira za walimu mwaka 2015 nikabaini kuwa Wazanzibari ambao hawastahili kuajiriwa Tanzania bara katika idara au taasisi isiyohusu mambo ya muungano wamepangwa katika Halmashauri mbalimbali Tanzania Bara kwa ajira katika shule za sekondari. Je serikali imetumia kigezo gani kutoa ajira hizo?

source: http://www.pmoralg.go.tz/noticeboar...u_Sayansi_2015_OWM-TAMISEMI_30April2015_3.pdf
 
Wanzibar ni wanjanja mbele ya watanganyika,

Nchi ndogo kuliko hata Wilaya ya ilala , Lakini ina watumishi, mawaziri,wabunge Utitiri kuliko hata nzige na woote wanalipwa mishahara na posho na Tanganyika, Serikali ya Tanganyika ni buzi la Zanzibar inachunwa mpaka huruma na hawajitambui hadi leo.

Chao ni chao lakini cha Tanganyika ni cha woote! Huu ni muungano Analogia na wa Ajabu uliosalia Duniani, muungano wenye Rais na baraza la mawaziri kibao huku wabunge wa Zanzibar wao wanakula posho Dodoma na wanakuwa mawaziri Tanganyika lakini wabunge wa tanganyika ni marufuku huko zenji. Huu ni muungano Hasara kwani inatumika pesa nyingi sana kuubembeleza na kuwalea Utitiri wa watumishi waliojilundika huko zenji.

Tiba pekee ya hii Kero ni kuwa na Serikali moja tu Rais mmoja.
 
Unaweza kufafanua ubaguzi kivipi? kwani elimu ya msingi na sekondari ni mambo ya muungano?

Ubaguzi upo Zenji nitajie mbunge wa bara ambaye ni waziri kule zenji? Na kwa nini wabunge wa Tanganyika hawanusi baraza la wakilishi? Na kwa nini hawajilipi mishahara kwa pesa zao? Tambua kuwa walipa kodi wa Tanganyika ndiyo huwalipa mishahara Utitiri wa watumishi wa Zanzibar kwenye Nchi ndogo Kama kijiji cha kasanvulasole.
 
mkitaka hivyo itabidi watanganyika kule kwenye shule wasiajiriwe, maana tunao ndugu zetu wanasomesha kule
 
Ubaguzi upo Zenji nitajie mbunge wa bara ambaye ni waziri kule zenji? Na kwa nini wabunge wa Tanganyika hawanusi baraza la wakilishi? Na kwa nini hawajilipi mishahara kwa pesa zao? Tambua kuwa walipa kodi wa Tanganyika ndiyo huwalipa mishahara Utitiri wa watumishi wa Zanzibar kwenye Nchi ndogo Kama kijiji cha kasanvulasole.

unajua kwanini sisi tanzania hatuendelei na kwanini wanasiasa wanatucheza akili, kila siku wanaelimishwa ila hawaelewi. kwa ujinga huu CCM watatutawala maisha yote
 
Nimeshapiga kelele sana jamani,tunanyonywa na huu muungano wa chuna buzi,hili zimwi tutaliondoa lini?
 
muungano unawapendelea wazanzibar licha ya kuwa hawachangii chochote katika uendeshaji muungano wao wana tra yao(ZRB)inakusanya mapato cha ajabu hela yote inabaki kwao mishahara inatoka Dar!huku kwenye ajira za muungano watu milini 1.2 wametengewa 21% afu watu milioni 40 na ushee ndio hiyo 79% tunagombea,chao chao,chetu cha wote
 
Ng'ombe akiungana na kupe. Kupe atanenepa ng'ombe atakonda
 
Angeajiliwa mkenya vipi ingekua Sawa?
Mnalalamika walimu hakuna wakiajiliwa Kutoka zanzibar mnalalamika.
Sijafika zanzibar ila nasikia Kuna wa tanganyika wengi wanafanya kazi kwenye mahoteli ya kitalii yaliyopo zanzibar.
 
Hivi Kuna mwalimu mtanganyika mwenye sifa ameachwa kuajiliwa kwa sababu ya walimu Kutoka zanzibar?
 
Mbaguzi on duty!
Kama kuna kitu kinatufanya Watanzani wengi (Kama sio Waafrica) ni ugonjwa wa kukariri, tukisha jua NENO ubaguzi basi tunafanya application ya hilo NENO popote tu, ungejiuliza, suala la elimu from chekechea to secondary school ni la muungano? Nina hakika usingeandika ulicho kiandika! Wazanzibari wanaye waziri wao wa elimu, hivi wakiwa BARA na kufundisha shule zetu (hawakuanadaliwa mazingira ya elimu ya bara) watakua wana report kwa waziri wa elimu wa Zanzibar au wa bara? Umeisha wahi kujiuliza kwanini magari za yenye namba za Zanzibar yakija bara TRA wanayataka kulipa ushuru? Sababu ni 1 tu, TRA na ZRA ni vyombo vinavyo onana kama vya nchi 2 tofauti, so TRA ya Tanzania na URA ya Uganda pamoja na ZRA ya Zanzibar zinajiona ziko sawasawa! KWa hili la walimu wa Kizenji bara litakiwa serikali ilitolee ufafanuzi, ni kama madereva tu wenye leseni za bara wakienda Zanzibar wanatakiwa kuhakikiwa upya na hoja ya ubaguzi haijawahi kutloewa!
 

Mkuu ujinga ni kutojua, hivyo mtu kuambiwa ni mjinga kwa kutokujua, akiishajulishwa akajua, ujinga unamtoka na kumuingizia werevu, hivyo kwenyi hili wewe ni mjinga.

Naomba kuchukua fursa hii, kukuelewesha ili kukutoa huo ujinga wako, hivyo hutakuwa mjinga tena!.

Kila Mzanzibari, kwanza ni Mzanzibari, mwenye haki zote Zanzibar, kisha ni Mtanzania mwenye haki zote Tanzania. Hakuna mahali popote ambapo Mzanzibari anaweza kunyimwa ajira mahali popote Tanzania kama haki yake ya Utanzania, ila kwenye zile Taasisi za Muungano, Zanzibar ina quota yake ambapo lazima idadi ya watumishi fulani wawe Wanzanzibar.

Mfano wizara ya Elimu sio ya muungano, Watanzania wote wenye sifa za kuajiriwa wizara ya Elimu, wakiwemo Wanzanzibari wako huru kuomba kazi na wakikizi vigezo, wanaajiriwa kama Mtanzania mwingine yoyote!.

Hii inamaanisha nafasi za kazi zikitangazwa kwenye taasisi yoyote ya Tanzania iwe ya muungano au isiwe, Wazanzibari wenye sifa, wako huru kuomba nafasi hizo, ikitokea hakuna Mzanzibari yoyote mwenye sifa, then sii lazima kwa Mzanzibari kuajiriwa kwenye taaisi ambazo sio za Muungano.

Lakini kwenye taasisi za muungano, zikitangazwa kazi, pia Watanzania wote wenye sifa, wako huru kuomba, wakiwemo Wanzanzibari, ikitokea hakuna Mzanzibari mwenye sifa, then atatafutwa hata Mzanzibari asiye na sifa, hivyo kujengewa uwezo hadi kupata sifa na kukidhi vigezo, kwa sababu kwenye taasisi hizo, lazima asilimia fulani ya watumishi wake wawe Wazanzibari. Mfano ni Benki Kuu ya Tanzania, ni taasisi ya Muungano, kwenye set up yake, inaongozwa na gavana, na chini yake, wako ma deputy gavana watatu na mmoja wao, lazima awe ni Mzanzibari. Gavana ni Mtanzania, lakini kwa kipindi kirefu, alikosekana Mzanzibari, mwenye sifa za Deputy Governor, hivyo nafasi hiyo ilibaki wazi hadi alipopatikana Mzanzibari mwenye sifa hizo, Bw. Juma Reli, kwa sababu hiyo ni nafasi ya quota ya Zanzibar.

Gavana huyu aliyepo akimaliza muda wake na nafasi kubaki wazi, kama kuna Mzanzibari mwenye sifa za kuwa gavana, anaweza kuteuliwa kuwa gavana kwa mujibu wa Utanzania wake na sio Uzanzibari wake kwa sababu Kila Mzanzibari pia ni Mtanzania, ila sio kila Mtanzania ni Mzanzibari.

Natumaini umeelimika!.

Pasco
 
Mazindu Msambule

Tukiisha jiuliza haya watakuja wanawake wa bara na kuhoji uhalali wa wanaume wa Bara kuoa wapemba na waunguja....nadhani ni wa kulaumiwa hapa ni serikali yako kwa kuwa na kigugumizi kwenye mambo ya aina hii...let them be employed...hata kama hawataripoti kwa mtu!
 
Last edited by a moderator:
muungano unawapendelea wazanzibar licha ya kuwa hawachangii chochote katika uendeshaji muungano wao wana tra yao(ZRB)inakusanya mapato cha ajabu hela yote inabaki kwao mishahara inatoka Dar!huku kwenye ajira za muungano watu milini 1.2 wametengewa 21% afu watu milioni 40 na ushee ndio hiyo 79% tunagombea,chao chao,chetu cha wote
Binafsi huu muungano si jui wa nini
 
muungano unawapendelea wazanzibar licha ya kuwa hawachangii chochote katika uendeshaji muungano wao wana tra yao(ZRB)inakusanya mapato cha ajabu hela yote inabaki kwao mishahara inatoka Dar!huku kwenye ajira za muungano watu milini 1.2 wametengewa 21% afu watu milioni 40 na ushee ndio hiyo 79% tunagombea,chao chao,chetu cha wote
Kwenye miungano yote kuna kitu kinitwa 'the minority' ambao wanapata upendeleo fulani!.

Mfano mzuri ni ile taasisi ya ndoa, mume na mke ni watu sawa ndani ya ndoa na wote wana haki sawa za ndoa, kama ni kufurahi, mnafurahi wote, lakini siku zote ni mume ndiye anayelipia mahari, ni mume anayetoa fedha za matumizi, ni mume ndio mwenye wajibu wa kumlisha mke, kumtunza, na kumvisha, hata kama mke ana biashara yake kuweza kulisha nyumba au kujitegemea kwa mawazi, bado ni wajibu wa mume kumtunza mkewe.

Hivyo ndivyo ulivyo Muungano wetu huu adhimu ni kama ndoa, Zanzibar inahudumiwa na bara kwa haki zote kama alivyo mke, ikiwemo umeme bure na asilimia 4.5 ya pato la misaada. Hizo fedha inazokusanya Zanzibar ni biashara ndogo ndogo ya mke!. Asilimia 21% ya ajira ni miongoni mwa halali za mke huyu!.

Ni kutokana na kupenda, mume huwa radhi kufanya kila kitu kwa mkewe kwa ridhaa yake!.

Pasco
 
Wewe upo Nchi gani? Kwani haujui kuwa Cha Zanzibar ni cha Zanzibar lakini cha Tanganyika ni cha woote?

Muungano wa nchi moja kuinyonya nchi nyingine haufai kwa ustawi wa nchi yetu.
 
Back
Top Bottom