Mkuu ujinga ni kutojua, hivyo mtu kuambiwa ni mjinga kwa kutokujua, akiishajulishwa akajua, ujinga unamtoka na kumuingizia werevu, hivyo kwenyi hili wewe ni mjinga.
Naomba kuchukua fursa hii, kukuelewesha ili kukutoa huo ujinga wako, hivyo hutakuwa mjinga tena!.
Kila Mzanzibari, kwanza ni Mzanzibari, mwenye haki zote Zanzibar, kisha ni Mtanzania mwenye haki zote Tanzania. Hakuna mahali popote ambapo Mzanzibari anaweza kunyimwa ajira mahali popote Tanzania kama haki yake ya Utanzania, ila kwenye zile Taasisi za Muungano, Zanzibar ina quota yake ambapo lazima idadi ya watumishi fulani wawe Wanzanzibar.
Mfano wizara ya Elimu sio ya muungano, Watanzania wote wenye sifa za kuajiriwa wizara ya Elimu, wakiwemo Wanzanzibari wako huru kuomba kazi na wakikizi vigezo, wanaajiriwa kama Mtanzania mwingine yoyote!.
Hii inamaanisha nafasi za kazi zikitangazwa kwenye taasisi yoyote ya Tanzania iwe ya muungano au isiwe, Wazanzibari wenye sifa, wako huru kuomba nafasi hizo, ikitokea hakuna Mzanzibari yoyote mwenye sifa, then sii lazima kwa Mzanzibari kuajiriwa kwenye taaisi ambazo sio za Muungano.
Lakini kwenye taasisi za muungano, zikitangazwa kazi, pia Watanzania wote wenye sifa, wako huru kuomba, wakiwemo Wanzanzibari, ikitokea hakuna Mzanzibari mwenye sifa, then atatafutwa hata Mzanzibari asiye na sifa, hivyo kujengewa uwezo hadi kupata sifa na kukidhi vigezo, kwa sababu kwenye taasisi hizo, lazima asilimia fulani ya watumishi wake wawe Wazanzibari. Mfano ni Benki Kuu ya Tanzania, ni taasisi ya Muungano, kwenye set up yake, inaongozwa na gavana, na chini yake, wako ma deputy gavana watatu na mmoja wao, lazima awe ni Mzanzibari. Gavana ni Mtanzania, lakini kwa kipindi kirefu, alikosekana Mzanzibari, mwenye sifa za Deputy Governor, hivyo nafasi hiyo ilibaki wazi hadi alipopatikana Mzanzibari mwenye sifa hizo, Bw. Juma Reli, kwa sababu hiyo ni nafasi ya quota ya Zanzibar.
Gavana huyu aliyepo akimaliza muda wake na nafasi kubaki wazi, kama kuna Mzanzibari mwenye sifa za kuwa gavana, anaweza kuteuliwa kuwa gavana kwa mujibu wa Utanzania wake na sio Uzanzibari wake kwa sababu Kila Mzanzibari pia ni Mtanzania, ila sio kila Mtanzania ni Mzanzibari.
Natumaini umeelimika!.
Pasco