Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,958
- 7,697
Mayahudi ni moja ya jamii ya watu waliofadhiliwa sana na Mungu huko zamani kwasababu walipelekewa mitume mingi sana ila wengi wao waliwakanusha na hata kufikia kuwaua.
Wakati Mtume Muhammad (sala na amani ziwe juu yake) alipohamia katika mji wa Madinah kutoka makkah alikuta jamii kubwa sana ya kiyahudi ikiishi katika mji wa Madinah.Moja ya sababu ya kuishi katika mji wa Madinah ni kuwa walisoma kuhusu bishara za ujio wa Mtume wa Mwisho ambaye si mwingine bali ni Muhammad.
Mayahudi walitegemea kuwa Mtume huyo angelitoka miongoni mwao kama vile ambavyo Mungu aliwapa mitume mingi hapo kabla ila kutokana na ukaidi na ukafiri wao waliishia kuwakanusha na kuwaua.
Baada ya Mtume Muhammad kuwasili katika mji wa madinah na mayahudi kufahamu wazi kuwa ni Mtume wa kweli kutoka kwa Mungu, waliamua kumkataa waziwazi kwasababu hakuwa Myahudi.
Moja ya hoja zao walizomtaka Mtume Muhammad azifanye zilikuwa ni hii hapa
Quran 4:153
"Watu wa Kitabu wanakutaka uwateremshia kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika walikwisha mtaka Musa makubwa kuliko hayo. Walisema: Tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi. Wakapigwa na radi kwa hiyo dhulma yao. Kisha wakamchukua ndama kumuabudu, baada ya kwisha wajia hoja zilizo wazi. Nasi tukasamehe hayo, na tukampa Musa nguvu zilizo dhaahiri."
Mayahudi baada ya kujua kuwa Quran haikuwa imeteremshwa mithili ilivyoteremshwa Taurat kwamaana ya kitabu kamili kwa Mtume Mussa (a.s). basi walimtaka Mtume awateremshie kitabu chao mahususi kutoka mbinguni...Mungu akawajibu kuwa Mtume Muhammad asishange hilo ombi lao bali ajue kuwa walimtaka makubwa sana Mussa zaiidi ya hayo ikiwamo na kumtaka awaoneshe Mungu waziwazi wamuone kwa macho yao. Matokeo yake walipigwa na radi kali sana.Licha ya adhabu hiyo bado wayahudi walikwenda kuchukua ndama mmoja aliyenona na kuanza kumwabudu badala ya Mungu wa kweli.