Seasonal migration kwenye ulingo wa siasa imeanza... Moja inafanyika kwa hiari na uamuzi binafsi nyingine ni nguvu ya shekeli na ahadi ya kazi na madaraka
Hongera Nyalandu Kwa kumchapa kofi yule mjamaa.. It was a very calculated timing....! Umefanya kusudi ili upime ubavu kati ya tukio lake na lako lipi litafunika... Lipi litapata kiki...

siasa bhana.....!!!
CCM imepata pigo lingine jana.. Pigo kubwa... Ile hotuba imewasononesha wengi, kwamba wale wakazi 3000 waliovamia maeneo sensitive ya jeshi la polisi na jeshi la ulinzi pamoja uwanja wa ndege wasibomolewe nyumba zao kwakuwa MWANZA ndio walimpa kura..

Kuna watu wamepata kinga ya kutochukuliwa hatua za kisheria kwakuwa tu walimpa mkulu kura... Poleni ccm... Kiza kimetanda ndani ya chama... Na hakuna mwenye nyongo ya kuongea tena! Mwigulu na Kinana wanajua vema
Mchoko na kukata tamaa sasa ni dhahiri shahiri ndani ya chama dume na wenye kujitambua wameanza kuchukua hatua mapema.... Kujitenga na giza
Ukiachana na kizungumkuti cha uchaguzi 2020 kama utakuwepo ama la., lakini ccm itapukutika wanachama wake mahiri kuelekea 2020 na hawatakuwa na kimbilio lingine zaidi ya CHADEMA japo na mapandikizi yatakuwepo
Kuna tofauti kubwa ya mapenzi ya kweli hata kama mtu alikuwa changu na mapenzi ya pesa hata kama mtu alikuwa mlokole... CHADEMA itashutumiwa sana kupokea mafisadi, kupokea watuhumiwa wa kashfa mbalimbali, kupokea wachafu wa ccm... Lakini najua hawatayumba kwakuwa ufalme umefitinika....