Kkiukweli mimi ni shabiki wa simba lakini nilitegemea kuwa usajili wa kwanza simba kwenye dirisha dogo ni golikipa lakini si kiungo kwani wapo wa kutosha. Dhaira hatabiriki kama mvua za vuli kuna siku yupo vizuri kuna wakati anakuwa kama shati. Huyo andrew ntalla kibadeni anajua kwa nini alaimsajili simba lakini sio kipa mwenye hadhi ya kuchezea simba. Yule dogo hashim abuu ni mzuri sana ila anahitaji kama miaka miwili ya uzoefu apate mechi za mara kwa mara atatisha. Kwa sasa simba inahitaji kipa mzoefu kwa hararka na kama sio chuki binafsi kaseja alitakiwa aendelee kuwepo simba then huyo dogo angemrithi vizuri.