Wawekezaji kutolipa kodi miaka kumi- EPZA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wawekezaji kutolipa kodi miaka kumi- EPZA

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ntemi Kazwile, Jul 19, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Na Joseph Mwendapole
  18th July 2010

  Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje (EPZA), imesema wawekezaji wanaowekeza katika maeneo maalum watasahemewa kodi ya mapato kwa miaka kumi.

  Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Meneja Uwezeshaji wa mamlaka hiyo, Lamau Mpolo, wakati akizungumza na Nipashe mara baada ya mazungumzo na ujumbe wa wawekezaji 15 kutoka nchini Thailand, ambao wamekuja kuangalia fursa za kuwekeza.

  Alisema kivutio hicho cha msamaha wa kodi kimewekwa kwa makusudi ili kuvutia wawekezaji kuja kwa wingi nchini.

  Alisema wawekezaji hutumia muda mrefu kujiandaa kwa ajili ya kujenga viwanda na kuanza kuzalisha hivyo kuwatoza kodi mapema kutawafanya wakimbilie nchi nyiingine.

  Lamau alisema makampuni mengi yamekuwa yakianza kupata faida baada ya miaka mitano hivyo wameona kuna haja ya kuwapa unafuu wa kodi.

  “Mtu anaweza kuona miaka kumi ni mingi lakini mwekezaji anapokuja sio kwamba anaanza moja kwa moja kuzalisha na kuuza, anatumia muda mwingi kufanya maandalizi ya uzalishaji hivyo kumpa unafuu huo kwa miaka kumi ni mwafaka kabisa,” alisema.

  “Sisi tunaangalia na wenzetu duniani wanafanya nini kuhusu suala la kodi kwa wawekezaji maana hawa watu wanagombaniwa kote duniani, kila nchi inajitahidi kuwavutia kwa njia mbalimbali sasa mkiweka mazingira ambayo hayawavutii wanakwenda nchi zenye mazingira mazuri kuwekeza,” alisema Lamau.

  Aidha, alisema baada ya miaka hiyo kumi mwekezaji analazimika kuanza kulipa kodi serikalini ila akishindwa anatakiwa kutoa sababu za msingi.

  Lamau alisema mwekezaji akijieleza kwanini bado hana uwezo wa kulipa kodi serikali itaangalia sababu alizotoa na kama ikiona haikuridhika na sababu zilizotolewa basi atalazimika kulipa.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

  -------------------------------------------------------------------------

  Wajinga ndio waliwao
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Haya maeneo maalum ni yapi?
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu, moja lipo pale External karibu na TFDA, lilifunguliwa kwa mbwembwe na mkulu akiambatana na BWM.

  Sasa kama siyo wendawazimu ni nini kuwapa miaka 10. Au kuna watu maalumu wamelengwa? Tumetoka kuibiwa kwenye migodi, sasa tunarudi kwenye viwanda.
   
 4. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Binafsi sina ufahamu sana kwenye mambo ya uwekezaji, ila ningeuliza hizo nchi nyingine zinafanyeje kuwavutia wawekezaji?

  Kama nchi zote zinasamehe codi kama kivutio, basi litakuwa ni suala la kawaida. Ila kama ni sisi peke yetu, basi hapo kuna mchezo.

  Ila kwa ufahamu wangu, kusamehe kodi sio kivutio pekee. Ukiachilia mbali kusamehe kodi, ni nini kingine kimefanyika? Urasimu wa serikali umepungua, au bado red tape ipo pale pale?
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Nilidhani haimaanishi area-location ya EPZA bali fursa ya biashara.
   
 6. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
 7. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tatizo watz tukiona unyasi tu tunafikiri nyoka.....tutakosa mengi kwasababu hiyo siku nyingine...
   
 8. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
Loading...