GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,216
Kumezuka haka katabia ambako sijui hata hawa wanawake na akina mama walikutana wapi kukaa kikao na kufikia makubaliano au maazimio kuwa wote wafanye hivyo.
Nataka kusema kwamba sasa kumezuka kamtindo wanawake na akina mama kuwanunulia watoto zao wa kike (mabinti) taulo za usafi pedi ( sanitary pads) na kuwalazimisha kuwa lazima wawe wanazitumia hizo kila mwezi na pia kila wanapokuwa wanatumika wawe wanazihifadhi na wakimaliza periods zao waende kuwaonyesha mama zao.
Inasemekana kwamba sababu kubwa ya hawa wanawake au akina mama kuamua kufanya hivi kwa watoto zao wa kike ni katika hatua ya kuwakagua na kuhakikisha kuwa hawapati ujauzito.
Najua humu JF tumebarikiwa kuwa na mama na dada zetu (namaanisha wanawake) naomba leo mtusaidie je hii tabia ni sahihi kweli? Je huu siyo unyanyasaji? Na nani aliyewaambieni kuwa watoto wa kike wanachungwa kiasi hiki au kwa namna hii? Je na nyie mlipokuwa mabinti mama zenu walikuwa wanawafanyieni hivi?
Naomba kuwasilisha.
Cc:
nifah
miss chagga
faizafoxy
vitaimana
tatty
victoire
Na wanawake /akina mama wengine wote ambao sijawataja.