Wauza kila kitu ili waishi wakisafiri kwenye meli maisha yao yote

puker

JF-Expert Member
Nov 22, 2018
940
1,847
Wanandoa waliojulikana kwa majina ya John Hennessee, mwenye umri wa miaka 76 na mkewe Melody Hennessee, mwenye umri wa miaka 64, wameamua kutumia muda wa maisha yao yote wakisafiri katika sehemu mbalimbali ulimwenguni kwa kutumia usafiri wa meli, ambapo walibainisha kuwa miaka mitatu iliyopita waliamua kuuza kila kitu walichokuwa nacho, ikiwemo biashara na makazi yao, kisha kununua gari maalumu lenye makazi ndani yake, ili waweze kusafiri wakizunguka sehemu mbalimbali za nchi ya Marekani.

Wanandoa hao wenye asili ya Florida nchini Marekani, wamesema baada ya kuzunguka kwa muda mrefu na gari walichoka kuendesha gari hilo ndipo walipoona tangazo kupitia mtandao wa facebook la safari ya siku 274, la kampuni ya meli ya Royal Caribbean, ndipo safari yao ya kudumu baharini ilipoanza.

Wawili hao ambao hadi sasa wametembelea sehemu mbalimbali ikiwemo Australia, New Zealand, Canada, Misri na Pasifiki ya Kusini, wamesema maisha ya ndani ya meli ni rahisi wakilinganisha na ya ardhini na kwamba hivi karibuni watachukua makazi ya kudumu kwenye meli ya kitalii ya Villa Vie ambayo 30% ya wasafiri wake watakuwa ni wakazi wa kudumu.

Wanandoa hao wamesema maisha hayo ni rahisi kwa sababu hayana gharama nyingi kama Bima ya gari, ankara za nyumba na bima za mali, na kwamba gharama za melini hajazijafikia hata nusu ya maisha ya ardhini.

wonder-up-close.jpg
 
Hilo suala tu la kusafiri 'kuizunguka dunia', kiukweli I envy them, nahisi kuna watu at least wamebahatika to live their dream..!
Sisi tumekariri kwamba maisha mazuri ni lazima ujenge nyumba, uwe na gari na uiahi mtaa fulani. Kumbe unaweza huwa huna anuani we popote duniani unapatikana.

Raha zaidi ukute hiyo meli hua inatia nanga nchi mbalimbali inakaa hata siku kadhaa mnapata mda wa kuzurura huku na kule.. Maisha sindio hayo?
 
Hao ndio ma global citizen sasa!sisi tuendelee na uzalendo wetu
 
Sisi tumekariri kwamba maisha mazuri ni lazima ujenge nyumba, uwe na gari na uiahi mtaa fulani. Kumbe unaweza huwa huna anuani we popote duniani unapatikana.

Raha zaidi ukute hiyo meli hua inatia nanga nchi mbalimbali inakaa hata siku kadhaa mnapata mda wa kuzurura huku na kule.. Maisha sindio hayo?
'I wish'...!!
Yes, inatia nanga sehemu tofauti tofauti lazima, ifanyiwe marekebisho pengine baada ya siku chache mnaamsha tena..!!
Siye kusafiri ni mpaka mwisho wa mwaka kwenda kaskazini, aiseeeh'..!
 
Back
Top Bottom