Waungwana naombeni msaada na ushauri wenu

vanquisher

Member
Sep 24, 2019
53
64
Wakuu habari, poleni na majukumu.

Mimi ni mtanzania umri wangu ni miaka 30 nilishafanya kazi kampuni kiasia kwa miaka 3 na miezi 5 nikiwa kama mtu wa data ila walifungasha virago wakahamia nairobi toka mwezi December 2018 binafsi akiba niliyokuwa nayo nikaamua kujiajiri katika ujasiriamali maana tayari nilishakuwa na familia inayonitegemea.

Lakini katika business kuna ups and downs. Bahati mbaya au kwa kutokufanya effective observation katika soko, biashara yangu haikwenda vizuri na haikufanikiwa.

Kutokana na hilo, na ili familia pamoja na maisha binafsi yaendelee nalazimika kutafuta ajira kwa mara nyingine ili nijipange upya tena. Nahitaji nafasi ya kufanya kazi kwenye shirika lolote, taasisi yoyote, kiwanda au kampuni yoyote,

Elimu yangu ni degree. Nina uzoefu wa kufanya kazi kwa miaka 4 sasa, katika maeneo tofauti tofauti kama data entry, researcher, instructor specific kwenye administration, customer care na zinazoenda na hizo. Nina ufaulu mzuri (degree).

Ninatafuta nafasi kwenye shirika lolote, taasisi yoyote,kiwanda au kampuni yoyote ya muda mfupi au mrefu nipo tayari.

Pia kwa ambaye anaweza kuniunganisha kwenye kazi zozote za miradi yoyote nipo tayari.

Namba yangu ni 0686 546724
 
Una umri gani na umefanya kazi kwa muda gani katika kampuni ya Kiasia?
 
Mungu akusimamie upate.....
Pia jaribu kipitia pitia kwenye websites za ajira ukikuta kazi ambayo sifa zake unazo tuma tuu
 
Umenigusa sana mkuu ila Mungu wa Yakobo akujibu siku ya dhiki yako na kukutimizia matakwa yako yote.
 
Back
Top Bottom