Waungwana mnijibu.... hili linanitatiza

Waungwana mnijibu.... hili linanitatiza

MwanaHaki

R I P
Joined
Oct 17, 2006
Posts
2,401
Reaction score
710
Wadau

Napata shida kuelewa, jambo hili linanitiza.

Unakuta mtu anaingia humu ndani na kuuliza swali ambalo hajalifanyia utafiti wa kina. Mtandao mzima wa Intaneti ni darasa tosha. Ukiwa na shaka unaingia na kufanya utafiti. Kuna "browser" kama vile Firefox, ambayo inakupa nafasi ya kuuliza swali au kufanya utafiti kwenye wavuti mbalimbali kama vile Google.

Mtu anakurupuka huko anakuja na swali badala ya yeye mwenyewe kulifanyia kazi; au Watanzania tumezoea kutafuniwa na kumezewa kila kitu bila ya sisi kuanza kutafuta chakula?

Au huu kweli ni uvivu wa kufikiria? Hebu nielimisheni. Limenishinda.
 
Mkuu, umeona sasa?Google haina majibu ya maswali yote.Na hili ;ililokushinda ungeweza ku-google ukapata majibu?

Kwa kifupi usishangae sana ndugu yangu. JF ni kama jarife.Likakokoa kila aina ya kiumbe kwenye wavu wake,kuna watu wa aina zote hapa. Chambua mwenyewe linalokufaa.Lisilokufaa achana nalo.
 
mkuu watu wapo tofauti sana kwenye hiyo maada uliyoitupia hapa kuna baadhi ilimradi tu aweke post sasa kwa hali hiyo ndio maana unakuta mauzauza ila hata wewe umeshindwa kupata jibu kwenye google ukaja hapa teh tehe teh hh
 
Sasa wewe kabla ya kuuliza hili, si ungeenda huko gogo na fayafox kuuliza? Kwa hiyo wee mvivu wa kufikiri?
 
M to the P anajua track hii natambaa na chaki narusha fataki fi fikiri kabla ya kutenda mwanangu naanza na ile ile gia yangu we ukitaka denda nyukwa lakini baku@+u panua mizuka inapanda yanantoka maganda! Kamua baba kamuaa kamua hakuna kutumia hirizi wakijisifu na kujitamba washkaji watawaona machizi.
 
Nilianza na Google kabla ya kuja huku. Niko makini MNO. Kwangu Internet ni shule, ni darasa, ni chuo kikuu!
 
Labda niulalamikie mfumo wetu wa elimu na utamaduni; Elimu imechakachuliwa. Badala ya kuwafundisha watu kujitegemea, inawafundisha kuwa tegemezi. Badala ya kuwafundisha watu kufikiria na kuwa wabunifu, inawafundisha kuwa "copy and paste". Hebu nenda Sinza, Shekilango Road. Kila baada ya nyumba mbili au tatu kuna ama Guest House, Salon au Bar!

Utamaduni wetu umegubikwa na mila na desturi kandamizi, haswa kwa wanawake. Hivi nyie mwajua kuna sheria ambazo mpaka sasa Mke hawezi kuchukua mkopo - kama ameolewa - mpaka Mume wake naye aridhie na aweke sahihi yake? Kule Arusha kuna kabila moja - sitalitaja - ambapo mwanamke, kama yu mjamzito, ananyonyesha au vinginevyo, hawezi kwenda kutibiwa akiwa mgonjwa mpaka apate RIDHAA ya mume wake, hata kama yuko Nairobi?

Mpo hapo? Tunaelimishana tu. Huu ni mjadala. Tusikashifiane. Mie nimeuliza swali, nyie njooni na majibu. Mngeuliza: Je, wewe ulianzia kwenye Google? Lakini wengine mnasema hata mimi ni mvivu wa kufikiri. Ningekuwa mvivu wa kufikiri ningetaka kujua undani wa tatizo hili?
 
hapa ndio chuo kikuu tulia utayapata majibu
 
Mkuu, wakati mwingine humu kunakuwa na watu ambao wana ujuzi ama wamepitia hiko kitu mtu anachouliza,, sasa kwa kuuliza hapa humsaidia muuliza swali kupata mwongozo mzuri zaidi na ikiwezekana akapewa material ambayo Google usingeyapata..

Halafu, kwa kuuliza swali humu huwa inawasaidia na wengine kupata kujifunza kutokana na swali la mhusika na majibu ya wachangiaji. Kila mtu akiwa na swali akaamua kutafuta majibu yake Google kisha akakaa kimya basi itapoteza hata umuhimu wa kuwepo kwa Jamiifuroms...

Nikitaka kununua simu inakuwa rahisi nikiuliza as mtu atanielekeza duka wanapouza simu nzuri na itanisaidia kuokoa muda wa kwenda kuzunguka Kariakoo ama Posta, si ndiyo? Halikadhalika kuhusu Online Materials, kuna watu wana-access na sites ambazo zina info nzuri halafu mimi nikakosa hiyo access e.g, sites za baadhi ya Taasisi ni mpaka uwe member kuweza kuiaccess, kuwa member inabidi aidha uwe Part ya hiyo Taasisi ama ulipie....

Japo kwa namna moja ama nyingine nakubaliana na wewe, kuwa tuache uvivu na tujishughulishe...
 
M to the P anajua track hii natambaa na chaki narusha fataki fi fikiri kabla ya kutenda mwanangu naanza na ile ile gia yangu we ukitaka denda nyukwa lakini baku@+u panua mizuka inapanda yanantoka maganda! Kamua baba kamuaa kamua hakuna kutumia hirizi wakijisifu na kujitamba washkaji watawaona machizi.

hahahahahahahahahahahahahahahahahaha,kaka leo umeshindaje,naona hili track hadi msalani utakuwa unaliimba tu uongo,kweli?
 
Back
Top Bottom