Habari za mchana nyote.
Naomba niende kwenye topic yangu ipo hivi, nina kijibiashara changu kidogo nakifanya kujikimu kimaisha sasa nina mashine ya Efd na ni kawaida yangu kutoa risiti kulingana na mauzo yangu,
Sasa leo bahati mbaya mashine yangu hii ya risiti ikawa imekata moto na ikabidi niiweke chaji na mda huo wateja wanakuja ila risiti sitoi sababu ilikua imeisha chaji kabisa, baada ya kupata moto nikaiwasha na kutoa risiti moja kwa makadilio ya wateja wangu wote waliokuja wakati mashine ikipata moto.
Baada kama ya dakika si Chini ya tatu watu wa TRA wakapita kukagua matumizi ya machine na kukuta nimetoa hiyo risiti moja lakini nikawaelezea hali halisi ilivyokua kama hapo juu, wakagoma kunielewa na kudai kuwa sitoi risiti na ninatakiwa kutoa faini
Wakanipa fomu waliyojaza wao ili nisaini tayar kwa faini lakini nimegoma kwa kuamini sina kosa lolote kabisaaa.
Sasa wadau kwa wenye ufahamu na maswala haya naomba anipe mwongozo kama nilivyoeleza hapo juu je ni sahihi?.
Sent using Jamii Forums mobile app