Waungwana hii imekaaje, Nimekataa kusaini fomu za faini za TRA?

bisti

Senior Member
Aug 29, 2017
167
151
Habari za mchana nyote.
Naomba niende kwenye topic yangu ipo hivi, nina kijibiashara changu kidogo nakifanya kujikimu kimaisha sasa nina mashine ya Efd na ni kawaida yangu kutoa risiti kulingana na mauzo yangu,

Sasa leo bahati mbaya mashine yangu hii ya risiti ikawa imekata moto na ikabidi niiweke chaji na mda huo wateja wanakuja ila risiti sitoi sababu ilikua imeisha chaji kabisa, baada ya kupata moto nikaiwasha na kutoa risiti moja kwa makadilio ya wateja wangu wote waliokuja wakati mashine ikipata moto.

Baada kama ya dakika si Chini ya tatu watu wa TRA wakapita kukagua matumizi ya machine na kukuta nimetoa hiyo risiti moja lakini nikawaelezea hali halisi ilivyokua kama hapo juu, wakagoma kunielewa na kudai kuwa sitoi risiti na ninatakiwa kutoa faini

Wakanipa fomu waliyojaza wao ili nisaini tayar kwa faini lakini nimegoma kwa kuamini sina kosa lolote kabisaaa.
Sasa wadau kwa wenye ufahamu na maswala haya naomba anipe mwongozo kama nilivyoeleza hapo juu je ni sahihi?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za mchana nyote. Naomba niende kwenye topic yangu ipo hivi, nina kijibiashara changu kidogo nakifanya kujikimu kimaisha sasa nina mashine ya Efd na ni kawaida yangu kutoa risiti kulingana na mauzo yangu, sasa leo bahati mbaya mashine yangu hii ya risiti ikawa imekata moto na ikabidi niiweke chaji na mda huo wateja wanakuja ila risiti sitoi sababu ilikua imeisha chaji kabisa, baada ya kupata moto nikaiwasha na kutoa risiti moja kwa makadilio ya wateja wangu wote waliokuja wakati mashine ikipata moto. Baada kama ya dakika si Chini ya tatu watu wa TRA wakapita kukagua matumizi ya machine na kukuta nimetoa hiyo risiti moja lakini nikawaelezea hali halisi ilivyokua kama hapo juu, wakagoma kunielewa na kudai kua sitoi risiti na ninatakiwa kutoa faini wakanipa fomu waliyojaza wao ili nisaini tayar kwa faini lakini nimegoma kwa kuamini sina kosa lolote kabsaaa. Sasa wadau kwa wenye ufahamu na maswala haya naomba anipe mwongozo kama nilivyoeleza hapo juu je ni kweli sahihi?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni vizuri zai na ndivyo inavyotakiwa kwamba kama mashine ya EFD imereta mushkiri au huwezi itumia basi yakupasa uandika mauzo yote kwenye kitabu cha risiti cha kawaida na kumpatia mteja ili siku ikipona basi utoe kila risiti kwa mteja husika.

Sasa kama wewe umetoa risiti moja kwa mauzo yote technically upo sahihi ila unapaswa uwe na copy ya risiti za kitabu zote ambazo umewatolea wateja na wakitafuta jumla ifanane na ya kwenye risiti hiyo yenye mauzo yote.

Lakini pia afisa anatakiwa aje na mteja ambe hujamtolea risiti kama kidhibiti chake kwa sababu yeye kosa kalijuaje kama hana mtu aliyeuziwa bila risiti?
 
Okay Asante sana. Nimekupata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu..jaribu kwenda TRA uwaelezee haiwezekani upigwe faini kwa kosa la hiyo mashine kuisha chaji
 
Waipige faini mashine iliokataa moto kwa kushindwa kutimiza wajibu wake,wewe wanakuonea.
 
Back
Top Bottom