Waumini wenu sio waadilifu! - Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waumini wenu sio waadilifu! - Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maxence Melo, Feb 20, 2011.

 1. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #1
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema viongozi wa dini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhimiza uadilifu miongoni mwa waumini wao kwa sababu wengi wao ndiyo waajiriwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo Serikali.

  Amesema katika kundi kubwa la waumini wamo watumishi wasiotimiza wajibu wao na hata wengine kudiriki kuiba au kupokea rushwa, lakini wote ni waumini wao na wanahitaji kuchungwa kiroho.

  Ametoa rai hiyo leo mchana (Jumapili, Februari 20, 2011) katika kanisa la Mt. Paulo wilayani Bunda, mkoani Mara wakati wa sherehe za kumsimika Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Bunda, Mhashamu Renatus Nkwenda.

  Waziri Mkuu ambaye alikwenda Bunda kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko safarini Mauritania, alisema: “Baba Askofu umeteuiwa kushika jimbo hili jipya katika kipindi ambacho kuna changamoto nyingi za umaskini, za waumini waadilifu na wasio waadilifu, kondoo unaotuongoza sisi haohao ndiyo wezi na wengine wala rushwa ambao tuko Serikalini…lakini ni kondoo wako”

  Alisema viongozi wote wawe wa dni au wa Serikali hawana budi kulivalia njuga suala la uadilifu ndani ya nchi kwani hali imefikia pabaya. “Ninyi mnayo nafasi kubwa ya kiroho na kimwili lakini ni lazima sote tilivalie njuga… lazima tupige kelele, tukiputisha maadili ya nchi, sote twafa!”

  Akiwahutubia melfu ya waumini walioshiriki ibada hiyo, waziri Mkuu alisema kila mmoja ana jukumu la kulinda amani na utulivu wa nchi ambavyo vimedumu kwa miaka 50. “Sisi tumepokea wakimbizi kutoka kila kona, leo hii tukivurugana tutakwenda wapi? Rwanda au Burundi ambako hawana ardhi ya kutosha?

  Alitumia fusa hiyo kuwakumbusha Wartanzania kwa wasibaguane kwa misingi ya dini, kabila au jinsi kwani kwa kufanya hivyo, Taifa litasambaratika.

  Mapema, akitoa nasaha katika ibada hiyo kabla ya kuweka wakfu Askofu Mteule Renatus Nkwande, Askofu Mkuu wa Jimbo la DSM, Muadhama Poycarp Kardinali Pengo alisema Askofu Nkwande amepata uongozi katika kipindi ambacho kuna changamoto ya mgawanyiko baina ya viongozi wa dini mbalimbali, viongozi wa serikali ambayo matokeo yake yanawaumiza wananchi walio wengi.

  Alisema changamoto zilizopo hana budi kukabiliana nazo lakini akamtaka awe tayari kuubaini uovu na kuusimamia ukweli hata kama itagharimu maisha yake. “Si vizuri kuunyamazia uovu na kushindwa kuutambua kuwa ni uovu. Ni vema kuwa na ujasiri wa kulitamka na kulisema hili ovu… Huu ndiyo msimamo uanotakiwa katika Tranzania ya sasa,” alisema.

  “Uwe na ujasiri wa kusimama nyuma ya ukweli na kuwa kufa kwa ajili ya hilo… ukiogopa kufa leo utakufa kesho. Ukiogopa kusema ukweli leo, kesho au kesho kutwa utakufa, kikubwa ni kuhakiksha unakufa katika mikono ya Kristu na si vinginevyo.”

  Naye Rais wa Barza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mhashamu Askofu Juda Thadeus Ruwa’ichi wa Jimbo Katiliki la Mwanza akizumgumza kwa niaba ya m,aaskfu wote wa TEC, alisema wao kama viongozi wataendelea kuhimiza mshikamano wa Kitaifa licha ya kudaiwa kuwa wao ni wadini.

  Alisema wanaodai hivyo wana lao na kuongeza: “Sisi siyo wadini bali ni wakweli, wenye uwezo wa kukemea na kusahimsha mambo yanapokwenda ndivyo sivyo. Kama hatukuwahi kuwagawa raia huko nyuma, kamwe hatutafanya hivyo kesho wala kesho kutwa.”

  Mhashamu Askofu Nkwande ambaye amesimikwa leo alizaliwa Novemba 12, 1965 katika kijiji cha Mantare, Sumve, wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Ni mtoto wa kwanza kati ya watoto 10 wa Mzee Alphonce Masalu na Mama Mamertha Masabula. Mtoto mmoja alifariki na sasa wamebaki watoto tisa.

  Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na Mama Maria Nyerere, Waziri wa Nchi (OR-Mahusiano), Bw. Stephen Wassira, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Aggrey Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Col. Enos Mfuru, Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Mara, Maaskofu 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na mapadei na masista kadhaa.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMAPILI, 20.02.2011
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Serikali haina dini aache domo huyu waziri mkuu! Kuna hatua za kuwachukulia wasio waadilifu serikalini, sambamba na kwenye hizo institutions za dini!

  Mimi nashangazwa sana tunaongozwa na watu wa aina gani! Nchi haiongozwi kiimani imani, nchi inaongozwa kwa vitendo!

  Waache kutuona siye wajinga! Hii nchi kweli inahitaji revolution na si vinginevyo!
   
 3. r

  rmb JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hakuna lolote hapo, PM mzima badala ya kuchukua hatua, yeye anaenda "kusemelea" kwa viongozi wa dini ili iwe nini sasa na wakati yeye anauwezo wa kuwashughulikia? Huku ni kutuchezea sisi wavuja jasho wa nchi hii!
   
 4. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Pinda kumbe unajijua kama na wewe mwizi na wezi wengine unawajua, umewachukulia hatua gani, jamani Pinda anachosha na ngonjera zake.
   
 5. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Pinda huyu anasema Anna Makinda ni muumini mzuri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mviringo na siku zote hakosi Misa. Upande mwingine madudu ya Makinda yanaoashiria dhuluma kwa wanyonge tumeyaona bungeni. Huko ni kukwepa wajibu wa serikali pale watumishi wanapokiuka maadili na kama majibu kwa Maaskofu wanao kemea uovu
   
 6. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  kwani yeye ni mwaminifu? Si kaajiriwa na sisi na hatimizi wajibu kabisa? Aache uzushi
   
 7. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni aibu kwa PM kuongea pumba kama hizi..yaani yeye aliyekabidhiwa dola anashindwa kuwashughulikia mafisadi wala rushwa anatarajia askofu afenyeje sasa, maana huyu hana nguvu za dola kuwawajibisha mafisadi..sana sana atawakosoa then, atawaombea kwa Mungu ili wajirudi!! Nothing more they can do..hawana nguvu za dola.
   
 8. M

  Miken Member

  #8
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli ndugu,hakuna wa kumnyooshea kidole mwenzake katika serikali.

  Yeye angekuwa mwadilifu asingetetea Kulipa Dowans, asingedanganya umma mbele ya bunge tukufu,asingekubaliana na hoja ya kutafsiri upya kanuni za bunge na kusaliti watanzania, asingekuwa kimya wakati wasaidizi wake wamekula mabilioni kwenye ruzuku za wakulima,asingedanganya wanafunzi na wahadhiri UDOM.

  Angewasikiliza watoto wa wakulima walipoandamana kutaka kupewa 10,000, asingeahirisha uchaguzi wa meya kule kigoma ili CCM watafakari watashindaje.

  Hakuna kiongozi mnafiki ndani ya hii serikali kama Pinda ambaye alisoma seminari. Anataka kutueleza nini huyu?
   
 9. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Na hili kanisa vp? kwa nini wasingemualika 'Rais' wao ambaye ni msafi asiye na kasoro Nabii Wilbroad Peter Slaa.(padre rtd)
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,545
  Likes Received: 81,981
  Trophy Points: 280
  Hii njemba inelekea kuna wakati inaongea kabla ya kufikiri.
   
 11. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kikwete asingehudhuria, hata kama angekuwepo Dar. Ana chuki na kanisa. Kama ni uwakilishi wa rais angekwenda Dr. Bilal. Mizengo amehudhuria kama muumini binafsi.
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  ukipanda bangi usitegemee kuvuna mchicha
   
 13. O

  Ogah JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  so far kwa maneno yaliyoandikwa hapo juu Mh Pinda is quite right..................
   
 14. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  wote hovyo tu kuanzia jk mwenyewe,kwani hakuna wakuchukua hatua kudhibiti maovu,kurekebisha mambo,kusimamia uwajibikaji hata kutoa ufumbuzi wa matatizo yanayotukabili kama taifa.Wao nao wanalalama na kusikitika kama sisi.WAMEISHIWA HAWA WATU TUWAFUKUZE KAZI!
   
 15. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nashangaa kwanini watu wana badili maana,uadilifu si kwa viongozi tu hata sisi tunaongozwa yatupasa kuwa waadilifu na kumuogopa Mungu katika yote tunayofanya!
  tunawaangalia sana viongozi which is ok,lakini pia matendo yetu sisi yakoje????:hand::hand::rain:
   
 16. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu hpa PM alikua SOKOINE basi!
   
 17. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kabisa mkuu,kabla hajanyooshea wengine vidole amejitazama yeye? Uvivu kazini ni dhambi kubwa,awashughulikie hao mafisadi atuoneshe mfano..hatujampa kazi ya kuimba ngonjera
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Achape kazi huyu mtu ameshindwa kuwawajibisha wezi anasingizia dini?
   
 19. BULLDOZZER

  BULLDOZZER Senior Member

  #19
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh. PINDA yupo sahihi kabisa: WATUHUMIWA KARIBU WOTE WA UFISADI NA UBADHIRIFU WA UMMA NI WAUMINI WA KANISA. NA WAMETOA MCHANGO MKUBWA KULIFIKISHA KANISA HAPO LILIPO. NDIO MAANA TUKAONA JINSI WALIVYOWAPOKEA BAADHI YA MAFISADI (EL) KISHUJAA(mou).
  Mkakati uliopo sasa ni kujisafisha - au kwa lugha nyepesi KUHAMISHA UFISADI KUTOKA CCM - CDM. NI AIBU YA KARNE. Pinda kawatolea uvivu. Anayemponda Pinda naye FISADI muathirika.
   
 20. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Aloo we Pinda naomba ufahamu kuwa viongozi wa dini hawajalifumbia wala hawajafumbia huo uovu mnaotutendea, wamekemea sana na wataendelea kukemea, lakini ongopeni pale watakapochoka na kuanza kutamka laana juu yenu na kuiachia hasira ya BWANA ifanye kazi, itakuwa ni ole kwenu! Nakumbuka siku ya mazishi ya mashujaa wetu waliopigwa risasi hapa Arusha na CCM Askofu mkuu wa kanisa la KKKT jimbo la Arusha alihutubia umati wa maelfu ya watu waliohudhuria mkutano hou kwa kulaani kitendo cha mauaji yalotendeka Arusha, na akasema kuwa hata yeye pamoja na kanisa lake hamtambui Meya aliyechaguliwa, kwani uteuzi wake una walakini na umejaa njama zisizo na mema kwa mtanzania na bado hatuwezi kupata kiongozi ambaye ujilio wake umeanza na kuja kilio na simanzi mioyoni mwa watu wetu! Lakini juzi namshangaa Pinda anasimama bungeni na kusema kuwa Meya amepatikana kwa njia halali kabisa! na bado akaitupia lawama CHADEMA kuwa ndo imesababisha vurugu na vifo vya ndugu zetu hao. Pinda usitake kutufanya sie kuwa ni vichwa vya wenda wazimu, tuna akili zetu na bado tunawaamini Wakuu wetu wa dini kuliko nyie coz hata nyie mko chini yao. Heshimuni mashauri yao na maonyo wanayowapa, La sivyo mtakuja muwe kama Mfalme Nebkadreza! Ni ole kwenu kama hamtatubu maana viongozi wetu wa Kiroho wamechoka hata sisi tumechoka pia, na karibu wataanza kuomba laana juu yenu badala ya rehema!
   
Loading...