Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari za wakati huu wapendwa

Katika dini zote au madhehebu yote au makanisa yote hakuna kanisa au waumini ambao wanaongoza kupigwa vita na kusemwa vibaya kama wakatoliki.

Ukienda kwenye mikusanyiko ya waislamu wanaopondwa ni wakatoliki ukienda kwenye mikutano ya injili ya walokole wanaopondwa na kusimangwa ni wakatoliki lakini huwezi kusikia wakijibizana na mtu.

Tangu nizaliwe hadi sasa sijawahi kusikia wala kuona wakatoliki wameandaa mkutano wa injili kuponda au kusimanga dini kinzani au dhehebu kinzani.

Isipokuwa wao mafundisho yao kwa watoto wa kimunio ya kwanza na kipaimara yamejikita katika kuufahamu ukatoliki na kuuelewa vizuri ndio maana ukikuta mkatoliki ameiva kabisa kwenye mafundisho huwezi ukamkuta anatetereshwa kwa mambo ya kijinga.

Wakatoliki wengi wao wamepewa mioyo ya uvumilivu ndio maana wanasimangwa sana kuhusu ubaya madhaifu yao lakini bado wapo imara na wameendelea kushikilia imani yao.

Huwezi ukakuta wakatoliki wanashawishi watu wahamie dini yao kwa kuwaambia madhaifu ya dini kinzani huwezi kukuta wakatoliki wapo mtaani wanahubiri au kwenye mabasi kisha kuwaambia watu watoe sadaka huwezi kukuta hiyo.

Ushauri wangu kwa dini na madhehebu mengine ni bora katika mafundisho yenu mjikite katika kuwaambia watu mazuri ya dini na madhehebu yenu ili kama mtu akivutiwa na mafundisho yenu awafate bila kuchafua dini za wenzenu.

Maana unaweza ukachafua dini/dhehebu la mwenzio siku na lako likija kuchafuliwa usianze kupaniki na kuanza kuleta maandamano ya kufunga barabara kwa kusema dini /dhehebu lako limechafuliwa.

Najua yapo mengi sana yanaongelewa huko mtaani kila dhehebu likisema ubaya wa dhehebu kinzani na wote ni mashahidi.
Kama wote lengo letu kufinga mbinguni muache afike kwa njia anayotaka yeye usimpangie njia ya kupita afike mbinguni.

Nilichogundua asilimia kubwa wanaohubiri kwa kuwachafua wenzao anataka wapate waumini tu ili SADAKA ziongezeke hakuna kingine.
 
Halafu Roman Catholic ni kwaajili ya Italy tu.Mmakonde,Mmachinga,Mmsai,Mchagga au Mnyakyusa na Catholic wapi na wapi !.Umewahi kuona au kusikia Pope Mwafrika au Mungu wa wa Catholic ni Mungu kwaajili ya wazungu pekee yake.
Roma ni Italia. Waingereza, wajerumani, wagiriki, wahispaniola, na hata wahindi na wachina nao hawahusiki na Catholic.

Na wao wakatafute Mungu wao.
 
Kanisa la Roma lina miaka 2000 toka limeanzishwa.

Hivi mtu mwenye umrinwa miaka 2000 atabishana nini na mtu aliyeanzisha karne ya 20?

Kanisa la Roma limewekeza kwenye elimu ndo maana wana shule na vyuo vikuu vya kutosha nchi nzima.

Afya
Kanisa la Roma lina hospital na dispensary nchi nzima.

Fedha
Kanisa la Roma lina Mkombozi bank. Kanisa la Roma ni taasisi imara na kongwe kabisa.

Waumini wake ni sehemu ya taasisi kwa hiyo hawana muda wa kuanza kujibizana na walokole ni kupoteza energy.
 
Imani sahihi ni ipi? Au ni hizi za makanisa ya mabati?
Imani sahihi ni kumuabudu Mungu katika roho na kweli huku ukijiepusha na ibada za sanamu.

Kuwa na masanamu yaliyojaa makanisani mwenu ni ibada ya kishetani.

Kumuamini Mariam ni ibada ya kishetani. Mariam anaitwa Malkia wa Mvinguni katika Ukatoliki. Hii title ya Malkia wa Ulimwengu imekatazwa kutumika katika Biblia.

Yeremia 7:18
[18]Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.

Vile vile ukisoma Yeremia 44 :17-19

17 Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya. 18Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa. 19 Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimwandalia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mimiminiko, waume zetu wasipokuwapo?

Hizo ndizo ibada za sanamu zinazokatazwa.
 
Kanisa la Roma lina miaka 2000 toka limeanzishwa.
Hivi mtu mwenye umrinwa miaka 2000 atabishana nini na mtu aliyeanzisha karne ya 20?

Kanisa la Roma limewekeza kwenye
elimu ndo maana wana shule na vyuo vikuu vya kutosha nchi nzima.
Afya
Kanisa la Roma lina hospital na dispensary nchi nzima.

Fedha
Kanisa la Roma lina Mkombozi bank.
Kanisa la Roma ni taasisi imara na kongwe kabisa.

Waumini wake ni sehemu ya taasisi kwa hiyo hawana muda wa kuanza kujibizana na walokole ni kupoteza energy.
Una upeo dhaifu wa kuelewa mambo. Kwako Taasisi kuwepo muda mrefu ndio ithibati ya imani yake?
 
Una upeo dhaifu wa kuelewa mambo. Kwako Taasisi kuwepo muda mrefu ndio ithibati ya imani yake?
Na ndo ilivyo mzee.
Hii nchi tu rais yoyote akitoka upande wa imani ya kikristu lazima awe mkatoliki
Anzia Nyerere,mkapa hadi JPM.
Kwenye deep state RC wamejichomeka vilivyo.

KALENDA UNAYOTUMIA INAITWA GREGORIAN CALENDAR ILIANZISHWA NA POPE GREGORY WA VATICAN.

Taasisi imara inachangiwa h na kudumu muda mrefu pia.

Huwezi fananisha kanisa katoliki na dini za walokole..
 
Back
Top Bottom