Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Wauguzi wawili wa hosipitali ya wilaya ya Mpwapwa wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za uzembe uliosababisha kifo cha kichanga tumboni kwa mama aliyefahamika kwa jina la Rehema Amos kutokana na kucheleweshewa huduma alipofika hospitalini hapo kujifungua.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mohammed Utaly ametoa agizo kwa watumishi hao kusimamishwa alipotembelea hospitali hiyo kufuatia tukio hilo ambapo inadaiwa wakiwa zamu kwenye wodi ya wajawazito kwa makusudi walifanya uzembe kwa kuchelewesha huduma hali iliyochangia kichanga cha mama huyo kufia tumboni huku akiunda tume ya watu watano kwa ajili ya kuchunguza tuhuma hizo.
Kwa upande wao wauguzi walipokutwa na tuhuma hizo Adam Mwampashi na Pendo chibutu wakizungumza na jopo lililoongozana na mkuu wa wilaya wakekiri kumuhudumia mama huyo wakati wa kijifungua huku wakikanusha madai ya kuhusika na kifo cha kichanga hicho.
Mganga Mkuu wa hosipitali hiyo Dk. Said Mauji amesema uongozi utashirikiana na tume hiyo bega kwa bega ili hatua zaidi kwa watumishi hao zichukuliwe endapo watabainika kuwa na hatia