Wauaji wilayani Kibiti wadaiwa kutuma ujumbe kuwa wataendelea kuwauawa Polisi kwa sababu huwadhulum

Huna akili nzuri ya kung'amua jambo. Hao tiss umeambiwa ndio kazi yao? Wao wamefikisha msg full stop. Polisi ndio wajiangalie kama kweli hudhulumu watu huko na waache na warudishe waliyodhulumu kwa raia yaishe. Wewe unaleta ujinga machafuko duniani dhuluma ni chanzo kikuu cha machafuko. Waswahili walisema Kubali yaishe...
Huna akili nzuri ya kung'amua jambo. Hao tiss umeambiwa ndio kazi yao? Wao wamefikisha msg full stop. Polisi ndio wajiangalie kama kweli hudhulumu watu huko na waache na warudishe waliyodhulumu kwa raia yaishe. Wewe unaleta ujinga machafuko duniani dhuluma ni chanzo kikuu cha machafuko. Waswahili walisema Kubali yaishe...
Kwa hiyo hao wote waliouawa?? Usitukane weka hoja ndg. KAZI YA TISS NI NINI? JE, KWENYE situation YA KIBITI HAWAHITAJIKI KUWABAINI HAO WAHALIFU, then POLISI WACHUKUE HATUA?? Au uelewa wako kihusu kitengo cha usalama wa taifa ni nini? Nahisi utakuwa mmoja wa hao genge huko kibiti, hili povu si la kawaida... Semeni mmedhulumiwa nini??
 
Yaani mpaka imefikia hiyo hali wahalifu wanatuma ujumbe kuwatisha serikali? Hivi hao watu wana roho ya kibidamu kweli? Sasa kwa nini wanawaua raia wa kawaida? Wamewadhulumu nini hao raia wa kawaida? TISS waende huko mara moja hill genge litajulikana mbona, tumeshachoka na hao mashetani
Hao uliowataja wao wapo kumlinda Bashite tu na kumsaidia kazi zake vingine hawana habare
 
Usijifanye unauchungu sana zaidi ya wengine.DHURMA ni neno pana mno. Habari yako haina ushahidi wakutosha, kutuaminisha walioandika hicho kiujumbe ni watu wasiojulikana kwa sababu unamuamini kiasi gani aliekwambia hicho kiujumbe wamekitoa watu wasiojulikana? Tena kwakisababu ambacho ni dhaifu kwa matukio ya watu wenye sifa tofauti tofauti.
hao ni bodaboda wahuni wanaotumia fursa kuwa tisha askari wetu wa barabarani kutimiza majukumu yao ipasavyo,baada ya mauaji ya hao askari wa barabarani

 
Ushauri ambayo unaweza kumaliza tatizo hili Jeshi la Polisi ndiyo wajiangalie kama kweli hudhulumu watu huko na waache na warudishe waliyodhulumu kwa raia yaishe.Hakuna njia nyingine siku dhuluma ni mbaya sana

Wao hawajasema haya kwamba polisi wanadhurumu watu. WAmesema wanawaua wanaodhurumu!. Wanadhurumu nini? Dhurma hiyo ni nini? Je kama wanaona hawataki kuwa na muundo wa serikali ulipo kwa kuwa uandhurumu wakitakchaow wao, tutaondoa serikali tuwpe wao utawala?

Na kama wanasema kulazimisha watu kwenda shule ni dhurma, hawataki shule kule au mitaala infundishwayo hawaitaki wanataka wafundishwe watoto kile wakitakacho wao, tutafung shule au kubadili mfumo wa elimu ili kufuata vile watakvyo wao?

Kama wakisema mahakama na sheria zilizopo zinadhurumu kwa kuwa hawataki sheria hizi zitumike, tutafunga mahakama tuache kila mtu afanye sheria azitakazo yeye, kwama mtu akikukosea, basi umhukumu utakavyo bila hata ya kuwa na chombo ch akusililiza?

Vipi kama wanataka kibiti na visiwa vyake viwe nchi nyingine, na kwamba kuunganisha ha tZ ni dhurma, tutajitadhmini na kuwamegea sehemu ya Kibiti na visiwa vyake iwe nchi nyingine?

Ni kweli mtu mwenye akiili sahihi anadaiga madai yake kwa utaratibu wanaoutmia hawa magaidi?

Ni sahihi kwamba polisi kwa kuwa wanadhurumu hukumu yako iwe kifo? Ni kweli kwamba polisi wote ni wadhurumaji? Ni kweli kwamba wanaouawa ndio waliowahi kudhurumu?

Dhuruma ipi hiyo wanaoyisema hawa magaidi? Mbona hawaiweki wazi?

HIZI ZOTE NI SABABU ZA KUVURUGA MAISHA YA WATU KWA KUWA HAWA WATU HAWANA MAISHA NI WACHOVU NA WANAFANYA FUJO ILI TUKOSE WOTE!.

HIZI KAULI NI ZA KIGAIDI NA HUWEZI KUKAA MEZA MOJA NA GAIDI ETI MNAWEKA MAKUBALIANO!. HAWA NI WA KUWASHUGHULIKIA TU KWA MWENDO KASI!
 
Hili suala linaitaji akiri nyingi kupambana na awa wauwaji wa kibiti lakini bahati mbaya tuliyonyo tuna viongozi wanaotumia Nguvu nyingi akiri baadae
 
Kama wauwaji madai yao ndio hayo dhulma basi tuwe na aman madai yatashughulikiwa siro anasema atariboresha idara ya police Tz ili kila aliyetokwa na iman na police arejeshe iman yake nadhani ni vyema tukazichukua kila dondoo na kuzipima
 
Raisi atalisolve bila kujua nani anataka nini?

Hizo dhuruma ni zipi?

Wananch gani wanaoweza kutoa taarifa za dhurma kwa magaidi ili wakalipize visasi?

Inaonekana hawa watu hawana elimu yoyte zaidi ya matumizi ya silaha.

Hawana Imani ya Mungu na hawana utu. Wangelikuwa na maarifa ama ya elimu ya duniani ama Ufahamu wa Ki Mungu bila shaka wasingefanya dhuruma juu ya dhurma isiyothibitishwa. Wanaua watu kwa majungu? Wanaua watu kwa vyeo? Kwa hiyo wanataka nchi isiwe na polisi? Nchi isiwe na viongozi? Watu waishi kama wanyamapori?

No, ni waongo. WAnadanganya ili kupotosha attention za mapambano.
Kwanza wameua viongozi wanaowakilisha serikali katika maeneo ya kule. Maana yake hawataki muundo wa uongozi uliopo.
Pili wameua raia wote wanaotoa taarifa zako kwa serikali. Kwa maana hawataki wafahamike. Kama ni majasiri si wajitokeze hadharani? Kama wanataka kufa, kufa kwa ajili ya nani? Watoke hadharani ili watafute suluhu.
Sasa wanaua polisi na wanasema watawasaka kokote waliko. Hapo maana yake wanateketeza ulinzi ili nchi isiwe na ulinzi!.
Wakimaliza polisi, nani atafuata? Maana yake wakimaliza polisi wataanza kuua raia wote kwa ulaini bila pingamizi lolte na kuwalazimisha wafanya vile watakalo!!!!!!!!!!!!!. Lengo lao si kuua watu kwa ajili ya kukomesha dhurma, wanatengeneza mazingira ya utawala wautakao wao bila pingamizi la serikali wala polisi!.

Asomanye na afahamu!

Serikali iongee vizuri na huyo diwani aliyesema kwamba wanaolengwa ni askari waliouawa juzi barabarani. Ufafanuzi huu haumo kwenye maandishi ya haya magaidi. Kwa hiyo inawezekana ni nyongeza iliyopatikana kwa maneno ya mdomoni. Anahitaji ulinzi sana huyu diwani.

KAULI ZILIVYOKWENYE HUO WARAKA ZINA PATTERN SAWA KABISA NA KAULI ZILIZOWAHI KUTOLEWA NA KUNDI LA KIGAIDI LA AL SHABAB, WAKATI WAKITISHIA KUVAMIA TANZANIA. CLIP HIYO ILIKUWEPO HAPA JF.

SERIKALI IWE SERIOUS NA HILI GENGE. HAWA NI ALSHABAB WALA SI MTU MWINGINE.
Genuine of the truth
 
Ayo madai hayana msingi wowote.na sio kweli sababu sio iyo.waeleze ukweli.na wenyeviti nao ni askari wa usalama barabarani???


anyway HAPA CHUMA TUU.
 
N
nenda kibiti ukafahamu kinachoendelea sio blah blah tu... au soma nyuzi zote zinazohusu kibiti... Sirro kasema mengine hawawezi yasema kwa raia... huko now ni vita ushaambiwa wao wamejitolea kufa sababu ya dhuluma ya viongozi hao raia hufa sababu ya umbea wao.. nadhani na wao wanamtandao mzuri maana wanafahamu kila kitu na idadi ya wambea na kuwasaka hadi nyumbani kwao
Hujui nipo wapi,acha kuhisi hisi tu.

Weka akiba ya maneno yako,wanauwawa sababu ya umbea upi ndugu ambao ni siri???
 
Ushauri ambayo unaweza kumaliza tatizo hili Jeshi la Polisi ndiyo wajiangalie kama kweli hudhulumu watu huko na waache na warudishe waliyodhulumu kwa raia yaishe.Hakuna njia nyingine siku dhuluma ni mbaya sana
Hakuna kitu wewe,polisi sio wajinga wasijue suruhisho kirahisi namna hii mpaka uje uwakumbushe.

Hao ni wahuni tu waamizi wanatafuta sababu ya kuungwa mkono na wananchi.
 
Back
Top Bottom