Wauaji wilayani Kibiti wadaiwa kutuma ujumbe kuwa wataendelea kuwauawa Polisi kwa sababu huwadhulum

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,509
2,000
tmp_20228-IMG_20170624_074323894294138.jpg

Siku mbili tangu kuuawa kwa polisi wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambao walikuwa kazini katika kijiji cha Bungu B, hali ya wasiwasi imezidi baada ya wauaji hao kusambaza ujumbe unaoeleza kuwa wanaendelea kusaka askari kwa kuwa ni wadhulumaji.

Watu hao wametuma ujumbe mfupi ulioandika kwenye karatasi na kisha kuutuma katika mitandao ya kijamii, ukidai kuwa waliouawa (japo hawajatajwa majina yao) wanadhulumu watu kwa kutumia kazi yao.

"Tunawatangazia wananchi tumewaua hawa kwa sababu wanadhulumu watu kwa kutumia kazi zao na yeyote atakayefanya kazi hapa au nje ya hapa tutamtafuta hadi nyumbani kwake.

Sisi tumejitolea kufa kuliko kuishi, kwa hiyo dereva au raia popote uwaonapo toa taarifa iwe nyumbani au kazini", unasema ujumbe huo.

"Hakuna njia ya kumaliza dhuluma isipokuwa chuma tu, hapa chuma tuuu!"

Ujumbe huo ambao umeandikwa kwa mkono kwa kutumia kalamu ya rangi ya bluu unadaiwa kuwa unazungumzia vifo vya askari polisi wawili wa kituo cha polisi Kibiti, Sajent Salum na PC Masola waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa kazini.

Mmoja wa madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Kibiti) jina tunalo) alisema ujumbe huo unawalenga askari wa kawaida na wa kikosi cha usalama barabarani.

Diwani huyo alisema kundi hilo linalofanya mauaji katika wilaya za Kibiti na Rufiji bado lina nguvu.

"Linaonyesha bado lina uwezo mkubwa wa kufanya mauaji na kutokomea kusikojulikana", alisema

Alisema kwa sasa Serikali inapaswa kuongeza nguvu zaidi ya wapelelezi ili kukomesha kikundi hicho ambacho hakijulikani kinafanya hivyo kwa sababu zipi na wala kinakojificha.

Akizungumza ujumbe huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga alisema jeshi la polisi litaendelea kuwasaka. "Tutapambana nao tu", alisema Kamanda Lyanga na kukata simu

Chanzo: Mwananchi
 
Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,584
2,000
Dhuluma gani, ziainishe hapa JF mubashara kabisa ili tulinganishe na hali harisi ya madai hayo.
Pia, wametuma ujumbe wakauacha wapi!? .

Je, na viongozi wa vijiji na mgambo nao tatizo ni lipi !?

Weka picha ya ujumbe huo hapa JF.
 
Mkomavu

JF-Expert Member
Jan 25, 2016
10,539
2,000
Dhuluma gani, ziainishe hapa JF mubashara kabisa ili tulinganishe na hali harisi ya madai hayo.
Pia, wamemtuma ujumbe wakauacha wapi!? .

Je, na viongozi wa vijiji na mgambo nao tatizo ni lipi !?

Weka picha ya ujumbe huo hapa JF.
Ukikaa kitengo cha kuhoji wahalifu unafaa sana afande
 
Duduwasha

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,714
2,000
Yaani mpaka imefikia hiyo hali wahalifu wanatuma ujumbe kuwatisha serikali? Hivi hao watu wana roho ya kibidamu kweli? Sasa kwa nini wanawaua raia wa kawaida? Wamewadhulumu nini hao raia wa kawaida? TISS waende huko mara moja hill genge litajulikana mbona, tumeshachoka na hao mashetani
Huna akili nzuri ya kung'amua jambo. Hao tiss umeambiwa ndio kazi yao? Wao wamefikisha msg full stop. Polisi ndio wajiangalie kama kweli hudhulumu watu huko na waache na warudishe waliyodhulumu kwa raia yaishe. Wewe unaleta ujinga machafuko duniani dhuluma ni chanzo kikuu cha machafuko. Waswahili walisema Kubali yaishe...
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
5,000

Kwani una uhakika kuwa hawapo?!! Wakati idara hiyo inaanzia ngazi ya wilaya? Kuwepo na kuwa na uwezo ni vitu viwili tofauti.
 
Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,509
2,000
Tunawatangazia wananchi tumewaua hawa kwa sababu wanadhulumu watu kwa kutumia kazi zao na yeyote atakayefanya kazi hapa au nje ya hapa tutamtafuta hadi nyumbani kwake.

Sisi tumejitolea kufa kuliko kuishi, kwa hiyo dereva au raia popote uwaonapo toa taarifa iwe nyumbani au kazini",

"Hakuna njia ya kumaliza dhuluma isipokuwa chuma tu, hapa chuma tuuu!".unasema ujumbe huo
 
Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,509
2,000
Wamemtumia nani kwa namna gani?
Ujumbe huo ambao umeandikwa kwa mkono kwa kutumia kalamu ya rangi ya bluu na umetumwa kwenye mitandao ya kijamii unadaiwa kuwa unazungumzia vifo vya askari polisi wawili wa kituo cha polisi Kibiti, Sajent Salum na PC Masola waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa kazini.
Huo ujumbe wametuma kwa njia IPI. Email. SMS au kupiga sm
Naona police waanza Na gazeti
Wamemtumia nani na kwa njia ngani? Tupe taarifa pia
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
21,065
2,000
Huna akili nzuri ya kung'amua jambo. Hao tiss umeambiwa ndio kazi yao? Wao wamefikisha msg full stop. Polisi ndio wajiangalie kama kweli hudhulumu watu huko na waache na warudishe waliyodhulumu kwa raia yaishe. Wewe unaleta ujinga machafuko duniani dhuluma ni chanzo kikuu cha machafuko. Waswahili walisema Kubali yaishe...
Nao wanapenda wakidanganya watu,watokeze wajinga kuuingia mkenge kama wewe.

Hivi kulipiza kisasi kwa dhuruma huwa unajumuisha watu wote tu!!!???au unachagua wahusika zaidi.mgambo na wenyekiti nao ni polisi???
 
Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,599
2,000
Yaani mpaka imefikia hiyo hali wahalifu wanatuma ujumbe kuwatisha serikali? Hivi hao watu wana roho ya kibidamu kweli? Sasa kwa nini wanawaua raia wa kawaida? Wamewadhulumu nini hao raia wa kawaida? TISS waende huko mara moja hill genge litajulikana mbona, tumeshachoka na hao mashetani
TISS wa nchi gani hao? Wa hapa Tanzania wapo huko kitambo tu. Hili suala mimi nadhani rais aangalie namna ya kulisolve kwa upya.
 
mputamaseko

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
1,401
2,000
Yaani mpaka imefikia hiyo hali wahalifu wanatuma ujumbe kuwatisha serikali? Hivi hao watu wana roho ya kibidamu kweli? Sasa kwa nini wanawaua raia wa kawaida? Wamewadhulumu nini hao raia wa kawaida? TISS waende huko mara moja hill genge litajulikana mbona, tumeshachoka na hao mashetani
TISS?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom