Watumishi wa vyuo vikuu:"serikali inatunyanyasa" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watumishi wa vyuo vikuu:"serikali inatunyanyasa"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tonge, Aug 26, 2010.

 1. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  KWA UCHUNGU MKUBWA TUNAUTOA MALALAMIKO YETU KWA SERIKALI, WAFANYAKAZI WA VYUO VIKUU TULIPATA WARAKA UNAOONYESHA KUWA MSHAHARA UMEPANDA KUANZIA JULY 2010, LAKINI CHA AJABU HATA SALARY SLIP ZILIZOTOKA LEO ZINAONYESHA MSHAHARA WA ZAMANI WAKATI WENZETU WA SERIKALI KUU NA HALMASHAURI WAMESHALIPWA MSHAHARA MIPYA TANGU JULY, KWELI HAYA SI MANYANYASO KWA WATUMISHI WA VYUO VIKUU? MI NAJIULIZA SHIDA NI KUWA SISI SI MUHIMU NCHINI AU NDIO ILE KAULI YA KIRANJA MKUU INAFANYA KAZI? MAMBO HAYA YAMESHATOKEA HATA MWAKA JANA TUKALIPWA MASHAHARA MPYA JEB 2010 BADALA YA JULY 2009.

  TUMECHOKA NA SASA TUNASEMA MWAKA HUU TUNAMCHAGUA RAIS ATAKAE WAJALI WATUMISHI WOTE PASIPO UBAGUZI, NCHI INAONGOZWA KISIASA ZAIDI NA WATAALAMU HATUDHAMINIWI KWELI TUTAENDELEA KWA JINSI HII?

  DR SLAA NJOO HUKU VYUONI TUKUPE KURA ZETU, TUNAHITAJI MABADILIKO YA KWELI.

  kny WAKEREKETWA WOTE.:sleepy:
   
 2. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pumba!
   
 3. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tena njaa imekuzidi,kama unataka kula si uombe!
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hayo ni matokeo ya uvuvuzela wa watumishi wa vyuo vikuu nchini. Juzi kati hapa wanataaluma wa vyuo vikuu waliandaa mgomo kupinga mafao madogo ya uzeeni, cha ajabu mkageukana na kuanza kutafunana, mkasalitiana na mgomo wenu ukaishia tu mahali.

  Kikwete keshajua kwamba nyie ni mavuvuzela, usomi wenu na uprofessor wenu haujawasaidia kuwa na msimamo katika kudai haki zenu, ndiyo maana na yeye kaamua kuwapuuza kwa kuwa hamna lolote mnaloweza kulifanya na unafiki wenu wa kujipendekeza kwa CCM. Bora tu msilipwe milele manake nyie tuliyewategemea kwamba ni wasomi mgeweza kuwa na msimamo katika kudai haki zenu ndiyo kwanza mnaongoza kwa kujipendekeza kwa CCM. Nenda zako kalilie huko, msituletee upuuzi wenu hapa.
   
 5. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Siasa imewafunika wataalamu ila nakubali kuwa wasome wengi hwana misimamo kwa lolote, si kudai haki zao au hata kutoa ushauri kwa serikali kitaalamu, sijui tunaenda wapi ila kuna kazi kubwa wasomi wa Tanzania.
   
 6. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,501
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Jamani taratibu msishambulie sana na wala kuponda sana, haya matatizo yapo kila sehemu si Chuo Kikuu tu. Hii pesa ni ya kwao wafanyakazi wa UDSM watalipwa. Unless kama kuna mtu ana vivid evidence kwamba mshahara huwa unaongezeka halafu nyongeza yao haitoki kabisa, atueleze, ila nadhani hamna. Mbali na hivyo kwa upande wangu mimi ninadhani nyongeza ya mwaka huu imetolewa kwa wafanyakazi wote wa serikali Tanzania nzima na kwa makusudi maalumu. Hao wakubwa waing'ang'anie, wao wana mifuko mikubwa kiasi gani, kiasi cha kuweza kuiweka serikali ya JK mfukoni? Hawajipendi? Ukizingatia mwaka huu nadhani ni wa uchaguzi kwao pia kama viongozi wa chuo. Kunaweza tu kukawa na technical delay at some point somewhere, possibly hata nje ya chuo chenyewe, but believe me, hiyo pesa wataitoa tu tena hata kabla ya October 31
   
 7. P

  Pokola JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  poleni sana wadau, juteni sana, kuwa katika nchi ya kichaa..!
   
 8. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,501
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Mzee Lukolo;
  Tuacheni kupondana sisi walalahoi kwa walalahoi hatutaenda mbali!
  Kuhusu mgomo, kuna jamaa yangu yeye alinisimulia kuwa pande zote mbili, (serikali na wafanyakazi) wote walikatiana tamaa kabla ya mda, yaani wagomaji walikata tamaa kuendelea na mgomo, na serikali nayo ikakata tamaa kuendelea kusikiliza mgomo,...., sasa si tayari hiyo ikawa ni suluhu? sababu kila upande uliridhika.
   
 9. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Labda vyuo vikuu ni mashirika ya umma na hawako chini ya serikali kuu moja kwa moja?
   
 10. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,501
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Hata mimi huwa ninadhani hivyo!
   
 11. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,225
  Trophy Points: 280
  anzisheni umoja kama DARUSO ili muwe mnagomea ukandamizaji
   
 12. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Mh! Yaani hiyo ndiyo "solution" uliyoiona wewe????:confused2:
   
 13. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  unakumbuka mapesa mliyolipwa miaka 2 iliyopita na serikali hii hii ya JK mbona hamkuja jf kutuambia mamilioni mlioyapata....maana mlilipwa duh! leo kidogo tuu nga'aa ng'aa mnanyanyaswa eeeeeheeeeeeh! hayo ndio maisha yetu sisi tusio watumishi siku zoote heri wewe una salary slip.....wenzio hata ya sh 200 hatuna
  mix with yours
   
 14. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Scenario hii imeniijia akilini: Mgonjwa anaenda kwa daktari kuomba tiba halafu anambiwe; "Ulipokuwa mzima jana mbona hukuja hapa? Leo unapata homa unalia ng'aaa ng'aaa!"
   
 15. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Wewe umeanza kazi chuo kikuu lini? Hakuna hata mwaka mmoja mashirika ya umma yamepata nyongeza ya mishahara ya Julai na kulipwa mwezi huo huo. Kwa kawaida mishahara hiyo hupatikana kati ya Oktoba na Novemba ila nasikia mwaka huu utatoka Septemba kwa ajili ya uchaguzi. Kimsingi haicheleweshwi kwa makusudi ila inapopandishwe inabidi ioanishwe na scheme of service inayo-prevail kwa wakati huo. Sana sana maofisa utawala wanaweza kuchangia kucheleweshwa kwa nyongeza hiyo kama watachelewa kuchakachua scheme husika. Hivyo usiilamu serikali kwa hilo. Naamini utakuwa umenipata mdogo wangu kwanii naamini hujafanya kazi muda mrefu chuoni ndo maana hulijui hilo au hufuatilii maslahi yako kwa karibu kama wewe ni wa siku nyingi kazini. Cheers.
   
 16. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wana umoja wao unaitwa UDASA kwa UDSM na SUASA kwa SUA sijui vyuo vingine, lakini kila leo utasikia makelele mengi, hakuna utekelezaji hata kidogo. Waache wakome kwanza hawa. Maana tunafikiri tuna wasomi wa kuwatetea watanzania maskini badala yake kila leo wanawakandamiza watanzania kwa kupitia REDET na mashirika mengine uchuro yanayoisifia CCM kwa maslahi yao binafsi.
   
 17. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mix with yours
   
 18. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,501
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu Kapuni:
  Kutokukuambia wewe kipindi kile, hakumkoseshi haki ya kudai haki yake mbele ya safari. Still, hapakuwa na ulazima wa kukuambia, japo pia alikuwa na option ya kuweza kufanya. Tuangalieni issues hizi kwa makini na pasipo jazba ya nani atapata nini na nani atakosa nini. Sawa baba yangu?
   
 19. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Ninaamini kabisa Tonge sio mfanyakazi wa Chuo Kikuu; na sidhani kabisa wafanyakazi wa Vyuo Vikuu wamekosa mahali pa kujitetea kiasi cha kuja hapa! Mbona juzi tu walikuwa na kikao kikubwa tu cha kuzungumzia masuala yao ya pension na hausi allawanzi! Tonge usisababishe JF ikawajambie maprofesa wetu!!!!!! ha hah hahaa
   
 20. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hilo neno. Inaonyesha kaajiriwa mwaka huu huyu.
   
Loading...