Watumishi wa Serikali naomba ushauri wenu

Strawberry

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
274
108
Habari za leo wapendwa wa JF,

Naomba kuuliza ili niweze kupewa japo mwongozo kwa hilo swala linalonisumbua. Kuna rafiki ngu aliomba msaada yeye alifiwa na mme wake, mme wake alikuwa mtumishi wa maliasili, akapelekwa mkoa wa dodoma.Yule jamaa bahati mbaya akafariki.

Sasa mke wake akaanza kufatilia pesa ya usafirishaji wa vifaa vya mme wake kwa mkuu wa kitengo cha huko alipofia mme mkoani.Yule mkuu wa hicho kitengo akamwambia pesa hakuna na itakuchukua miaka miwili kuzipata.

Swali, anauliza anaweza kufatilia malipo ya mafao ya mme wake huku wizarani DSM anapoishi yeye, au itamlazimu aende kule mkoani kwa ajiri ya kufatlia hayo mafao?

Maana mahakamani kesha fungua mirathi na kapewa form za kujaza kwa ajiri ya mirathi ya mmewe.
 
Si akaulize ofisi za maliasili pale? Katibu mkuu wao ana ushirikiano sana kwa wafanyakazi wake.
 
Si akaulize ofisi za maliasili pale? Katibu mkuu wao ana ushirikiano sana kwa wafanyakazi wake.

Kumwona KM ni kazi kweli kweli, wapambe watakuzungusha mpaka uchoke. hivyo kama wajua jaribu kumsaidia
 
Kuna wakuu wa idara, sidhani kama watamzungusha makusudi. Hata hivyo hatua moja yashinda sifuri, bora aanzie pale, aulize utaratibu, basi kutokea hapo atajua la kufanya.

Kumwona KM ni kazi kweli kweli, wapambe watakuzungusha mpaka uchoke. hivyo kama wajua jaribu kumsaidia
 
ende tu wizarani hapa Dar akaulizie ofisa rasilimali watu, au afisa utumishi kwa lugha za zamani sijui kama bado zinatumika. Atapata msaada na zaidi maelekezo ya hatua za kufuata ili apatiwe haki anayostahili kwa utumishi wa mumewe (ambaye ni marehemu). Ilimradi awe anatambulika kama mke rasmi
 
Back
Top Bottom