Watumishi wa Serikali hawampendi Magufuli

Watumishi wa Serikali hawampendi Magufuli

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
8,593
Reaction score
17,553
Nimejaribu kufuatilia mwenendo wa watumishi wengi wa serikali katika kipindi hiki nimegundua watumishi walio wengi hawampendi mh.
Wengi wao wamekua wakitumia msemo wa HAPA KAZI TU kuwanyanyasa watu wanaohitaji huduma kutoka ofisi za serikali.

Kwa mfano, walimu wakiwa wanatoa adhabu kwa wanafunzi wanasema hapa kazi tu. Kuonyesha kwamba hapa kazi tu ni adhabu.

Madaktari na Manesi ndo usiseme.
Askari nao hali ni the same.

Nini tatizo la watumishi?
Hawapendi uwajibikaji?
Karibu tujadili
 
Acha uongo mbona ofisini kwetu shangwe tu hao watumishi labda siyo hawa wa tanzania.

Jaribu kufanya uchunguzi ndugu, inaonekana kuchaguliwa kwa Magu imekua mwiba kwao
 
Kila kitu ukawa heeeee tunajipanga ndio kwanza asubuhi subirini kwanza
 
Hayo ni Mabaki ya Ukawa yatashughulikiwa tu usiwe na wasiwasi

Acha ushamba wewe serikali ilikuwa ikishikiliwa na Ukawa ? Si hao hao ccm mnachekesha yaani leo mmeamua kukikimbia kivuli chenu maajabu ya Musa haya.
 
Acha uongo mbona ofisini kwetu shangwe tu hao watumishi labda siyo hawa wa tanzania.

kweli mkuu watu tunafanya kazi kwa moral ile mbaya sa cjui huyu jamaa kafanya uchunguzi wapi
 
Nikusaidie bwana mdogo. Watumishi wanawapenda wananchi wote ndio maana wanajitoa kuwatumikia hata bila kulipwa mshahara unaostahili. Wasichokipenda ni mfumo ulioasisiwa na serikali ya CCM ambapo asiyefanya kazi au anayefanya kazi kidogo analipwa mshahara mkubwa mno usiopimika wala kudhaniwa wakati wanaofanya kazi kubwa yenye kuumizwa wakipata kiduchu. Kwa kifupi wanaichukia CCM si Magufuli. Sasa kama anataka kuleta mabadiliko aanze na hilo ataeleweka nje ya hapo itaishia kaulimbiu tu "Hapa kazi tu" kwani Maisha bora kwa kila mtanzania yamepatikana?
 
Acha uongo mbona ofisini kwetu shangwe tu hao watumishi labda siyo hawa wa tanzania.

Mimi nadhani labda wale watumishi wenye madai ya muda mrefu ambao walikuwa wanahitaji mafao yako yalipwe. Hebu fikiria nesi au mwalimu ambaye hana nyumba waliyopewa kazini, hana rent allowance, hana posho ya nauli halafu anapanda gari mbili afike kazini, na anatakiwa afike saa1:30as. mpaka 10 alasiri. hivi huyu atafurahia usimamizi mkali wakati mshahara ni finyu na inamlazimu afanye shughuli nyingine ile amudu mahitaji ya familia?
Naamini falsafa ya Rais wetu mpendwa itazingatia pia maslahi na hali za wafanyakazi.
 
watanzania utawaweza kwa unafiki, pale wizara ya fedha mkuu wa idara anaulizwa hii meza ya nani amjibu "hajui" huyu hapa ameenda wapi anajibu "kaenda kunywa chai", haya wapiga soga wakataka kutoka mbio akawaita warudi. ofisi nzima wameachwa viwete tu wengine wameshapuyanga.

Muhimbili nako yule jamaa mwenye koti jeupe ndo alimtia hasira rais yaani alikuwa anachombeza utafikiri sio mfanyakazi anajibu hata asiyoulizwa eti "tangu mwezi wa pili mashine mbovu" "hatuwezi kabisa kumtibu bila hicho kipimo" kwahiyo waliolala chini walisubiri CT-Scan ndo wapewe vitanda?
 
Nikusaidie bwana mdogo. Watumishi wanawapenda wananchi wote ndio maana wanajitoa kuwatumikia hata bila kulipwa mshahara unaostahili. Wasichokipenda ni mfumo ulioasisiwa na serikali ya CCM ambapo asiyefanya kazi au anayefanya kazi kidogo analipwa mshahara mkubwa mno usiopimika wala kudhaniwa wakati wanaofanya kazi kubwa yenye kuumizwa wakipata kiduchu. Kwa kifupi wanaichukia CCM si Magufuli. Sasa kama anataka kuleta mabadiliko aanze na hilo ataeleweka nje ya hapo itaishia kaulimbiu tu "Hapa kazi tu" kwani Maisha bora kwa kila mtanzania yamepatikana?

kawaulize kwanza Tan Road na NHC ndo uje kutoa hoja hapa.
 
wafanyakazi hawapendi kazi zao sio hawapendi magufuri, hawapendi kazi zao kwa sababu hazina tija kwao hila ni bora liende.
 
mwendo mrefu hatimaye utaishia sakafuni uliona yako wapi sasa wanapaa tu itabaikia mafuvu kona ya nazi haipo
 
Back
Top Bottom