Watumishi wa Serikali hawampendi Magufuli

Nimejaribu kufuatilia mwenendo wa watumishi wengi wa serikali katika kipindi hiki nimegundua watumishi walio wengi hawampendi mh.
Wengi wao wamekua wakitumia msemo wa HAPA KAZI TU kuwanyanyasa watu wanaohitaji huduma kutoka ofisi za serikali.

Kwa mfano, walimu wakiwa wanatoa adhabu kwa wanafunzi wanasema hapa kazi tu. Kuonyesha kwamba hapa kazi tu ni adhabu.

Madaktari na Manesi ndo usiseme.
Askari nao hali ni the same.

Nini tatizo la watumishi?
Hawapendi uwajibikaji?
Karibu tujadili

Wewe unatembeza pichu huko mtaani halafu unakurupuka kusema Watumishi wa Serikali hawampendi Mhe. Magufuli!!!! Huo utafiti wako wa mahesabu ya pichu umeufanyia wapi? mbona sisi tuko huku na hatujakuona??? Acha ubwege na uchonganishi wewe!!!! Loh!!! Aibu yako hata wewe?????
 
Watanzania hawapendi kufanya kazi maofisini ni story na dharula zisizoisha,harusi,ugonjwa nk
 
Mimi nadhani labda wale watumishi wenye madai ya muda mrefu ambao walikuwa wanahitaji mafao yako yalipwe. Hebu fikiria nesi au mwalimu ambaye hana nyumba waliyopewa kazini, hana rent allowance, hana posho ya nauli halafu anapanda gari mbili afike kazini, na anatakiwa afike saa1:30as. mpaka 10 alasiri. hivi huyu atafurahia usimamizi mkali wakati mshahara ni finyu na inamlazimu afanye shughuli nyingine ile amudu mahitaji ya familia?
Naamini falsafa ya Rais wetu mpendwa itazingatia pia maslahi na hali za wafanyakazi.

Ndugu yangu kama unasubiri hadi upandishiwe mshara ndio utoe huduma nzuri hapo kwa kweli hatutafika mbali. Nadhani alikua ni Raisi keneddy wa USA aliwaambia wananchi wake "usielize serikali ikufanyie nini, jiulize wewe itaifanyia nini serikali na nchi yako"
Niko sweden na ni nchi ya kitajiri lakini miaka 90 iliopita ilikua nchi ya kimaskini hadi baadhi ya wananchi wakakimbilia USA.
Mzee mmoja alinielezea maisha yake alipokua kijana na alikua anafanya kazi yukuendesha treni. Anasema hali ilikua ngumu mshahara mdogo kiasi kwamba alikua hana uwezo wa kununua socksi ndefu kwa ajili ya baridi akawa anatumia magazeti akichomeka ndani ya suruali lakini walifanya kazi kwa bidii na upendo wakijua ipo siku maisha yatabadilika na ndio maisha tunayo yaona leo ya Sweden.
Hapo hospitalini jinsi manesi wanavyo fanya kazi inasikitisha, ni wajeuri kupita kiasi. Kwa hiyo inamaana hadi mshahara upandishwe ndio atoe huduma nzuri??
Raisi wetu ameanza vizuri, tumpongeze na tumpe moyo ili naye azidikupata nguvu
 
Naheshimu sana mawazo yako, japo umetoa mfano tofauti kabisa, Mimi sijaishia tu kusema mshahara ni mdogo Bali nimeenda kwenye specific, toka karne ya 19,mshahara haujawahi kuwa mkubwa kwa mfanyakazi. Hivi Sweden mfanyakazi anaweza kuwa anaidia serikali yake kwa miaka mitatu? Tunataka wafanyakazi wawajibike ipasavyo lakini pia hali zako na maslahi yao yaboreshwe.
 
Hii ni kweli wafanya kazi wengi tu watamchukia hasa hao wenye vyeo kwani uzembe na uwizi utapungua. Tusishangae ikatokea mgomo baridi ambapo baadhi ya hao vigogo au wakurugenzi kuzidi kufanya uzembe au kuchelewesha kazi ili mradi kasi ya mh raisi kupungua na wao wapate kujichotea. Ndio maana tunahitaji wasomi wengi ili huyu akileta uzembe anatimuliwa na kumweka mwingine mwenyo uwezo. Lakini wasomi wakiwa wachache basi inabidi awabembeleze hao waliokua wazembe na wezi.
Mfumo huu wa elimu bure hadi kidato cha 4 na mikopo kwa wanavyuo italeta wasomi wengi na maendeleo
 
Mafisadi, wazembe, na wabadhilifu wa mali za umma lazima wamchukie. but wachapakazi na waaminifu wataenjoy sana
 
Acha uongo mbona ofisini kwetu shangwe tu hao watumishi labda siyo hawa wa tanzania.
ni hapo kwenu lakini wengi hawampendi,tena hapa kwetu tokea kampeni,wanasema atawapelekesha sana,Watanzania hawapendi kufanya kazi aise,inaniuma sana ,watu wanataka wakae tu ,kisha wabebe mshahara na kula rushwa,kama hatutabadilika kila mmoja, kamwe Tanzania itabaki hapahapa hata aje Malaika kutuongoza..
 
Wapende wasipende ni lazima wafanye kazi.

Shoka tayari limewekwa kwenye mti, ule usiozaa matunda ni lazina ukatwe. Vivyo hivyo chekecheo limeanza kuchekecha watumishi wabovu.
 
Wewe unatembeza pichu huko mtaani halafu unakurupuka kusema Watumishi wa Serikali hawampendi Mhe. Magufuli!!!! Huo utafiti wako wa mahesabu ya pichu umeufanyia wapi? mbona sisi tuko huku na hatujakuona??? Acha ubwege na uchonganishi wewe!!!! Loh!!! Aibu yako hata wewe?????

Sidhani kama busara bado unazo. Hapa ni hoja tu
 
wengi wanampenda isipokuwa wale wenye makandokando.
 
Nimejaribu kufuatilia mwenendo wa watumishi wengi wa serikali katika kipindi hiki nimegundua watumishi walio wengi hawampendi mh.
Wengi wao wamekua wakitumia msemo wa HAPA KAZI TU kuwanyanyasa watu wanaohitaji huduma kutoka ofisi za serikali.

Kwa mfano, walimu wakiwa wanatoa adhabu kwa wanafunzi wanasema hapa kazi tu. Kuonyesha kwamba hapa kazi tu ni adhabu.

Madaktari na Manesi ndo usiseme.
Askari nao hali ni the same.

Nini tatizo la watumishi?
Hawapendi uwajibikaji?
Karibu tujadili
Wasiompenda ni WEZI, WABADHIRIFU, MAFISADI, WANAPITISHA DILI ZA WASIOLIPA KODI, wapo wengi na uzuri wanafahamiks.
 
Back
Top Bottom