habari ya hapa
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 12,791
- 8,748
Nakusalimuni nyote kwa jina la Mungu muumba mbingu na ardhi, poleni na majukumu,
Wapendwa nimeshakutana na hii kitu mara kadhaa kwa watu tofauti tofauti, kwamba wanna mahusiano na wachungaji au mapadri tena kwa kujifia kabisa bila kuwa na hofu ya Mungu, sijui wamekuwaje na wamepatwa na nini.
Hii kitu inashingaza sana kuona watumishi wa Mungu siku hizi wamecharuka kweli kweli kuzini yaani Msharika na mchungaji kuanzisha mahusiano imekuwa kitu cha kawaida kabisa, tena bila hata haya wanatumia neno la Mungu kufanya ujinga wao.
Kuna mpendwa mmoja jana alinitaka niende kwake bahati mbaya nikawa sipo mjini, kikubwa alichonambia ni kuwa alihitaji niende kwake nikamuone na kumthaminisha huyo mchungaji ili nimshauri kama anafaa au hafai, nikamwambia nimetoka kidogo akasema nikirudi mjini nimjuze ili nimwone huyo mtumishi wa Mungu nipate kumshauri awe nae ama la.
Nashangaa tu yaani sijui niwapi tunaenda, kuna Padri mmoja yeye yupo Kiwalani nae katembea na mke wa mtu jirani yangu hadi kumpachika mimba, na sasa mke ya mtu huyo anahangaika jinsi ya kutoa hiyo mimba, halafu Jumapili unasimama madhabahuni una hubiri dhambi kweli?