KERO Watumishi wa Fountain Gate tuna hali mbaya kiuchumi, Serikali itusaidie tupate stahiki zetu

KERO Watumishi wa Fountain Gate tuna hali mbaya kiuchumi, Serikali itusaidie tupate stahiki zetu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mdau wa elimu, naomba ujumbe huu ufike kwenye mamlaka za Juu Serikalini, lengo sio kuchafua taasisi yetu bali ni kutusaidia sisi Watanzania ambao tuna hali ngumu na hatuna mtu wa kutusaidia.

Siwezi kuharibu taasisi yangu wakati najua ndio sehemu ambayo Napata ugali wangu na familia yangu.

Taasisi ya Fountain Gate Academy imekuwa na changamoto yua kutolipa mishahara na stahiki mbalimbali za Wafanyakazi wake, hapa ninavyoandika ni zaidi ya miezi 6 sasa, hatujalipwa na kila siku tunajipa imani labda kesho.

Wafanyakazi tukiuliza juu ya haki yetu hiyo tunajibiwa “Geti lipo wazi, anayetaka aondoke”, sasa tutaondokaje wakati tunadai stahiki zetu!

Hali hiyo hasa Tawi la Dodoma imesababisha watumishi amba oni Walimu, Walinzi na madereva kuwa kuishi kwa kudowea chakula cha Wanafunzi Shuleni, hali ni mbaya.

Siku za nyuma ilipokuwa ikitokea hali hii, taarifa zilipofika kwa Wakubwa, Uongozi wa Taasisi ulichokuwa ukifanya ni kulipa miezi miwili au mitatu kisha hali ikipoa, wanarejea kulekule.

Baadhi ya Walimu wameshindwa kujihudumia kwenye matibabu kutokana na kutokuwa na hela.

Ujumbe huu ufike kwa Wizara ya Elimu, TAMISEMI na Ofisi ya Rais kwamba Watumishi wa Fountain Gate tunalazimika kudowea vyakula vya Wanafunzi ili njaa isituue.
 
Sasa ndugu yangu si ungekuja tu hapa kwangu kuliko ninavyokuona umenyong'onyea.
 
Ni hatari sana hao wenye shule ni wakatili sana?? Mnafanya kazi bila mkataba??? Hao inaonekana wanajuana na wakubwa! Ujumbe umefika!
 
Acha Kaz mkuu tutafute passport tukabebe box USA hapa bongo kama siyo mtu wa system kutoboa labda ufuge majini
 
Pole sana mwalimu. Hakika hakuna maumivu makali kama yale ya kutokujua kesho yako! Yaani unaishi huku ukiwa hujui kama mwisho wa mwezi utapata mshahara, au la! Na wakati una familia inayo kutegemea.

Ila bahati mbaya sasa hili ombi lako nalo linaweza lisiifikie hiyo serikali unayotaka ikusaidie! Kwa sababu wameifungia jamii forums kwa siku 90 kutokana tu na hila zao za siku zote. Na nitashangaa kama bado wapo humu!

NB; ushauri wangu kwenu; mjitahidi ndugu zangu kuanzisha vishughuli vidogo vidogo vya kuwaingizi kipato kama hiyo mishahara yenu ina unafuu kidogo. Na kama haiwezekani, basi muanze kufikiria kwenda kwenye taasisi zenye uhakika wa malipo. Mnaweza kuitumia hiyo Fountain Gate kama daraja la kuwapeleka mbele zaidi, badala ya kuendelea kuishi kwa matumaini.
 
Poleni jf imefungiwa ujumbe hauwezi kuwafikia wakubwa
labda wamkamate yeye kwanza aelezee amewezaje kupost shida yake.

Watanzania em tuwe na akili kdg aisee

Anyway, pole sana mtoa mada
 
Mwisho wa kufanya kazi bila kulipwa ni 2month labda kama una malupu lupu unapata huko kazini.
Mishahara ikishalimbikizwa zaidi ya miez mi3 kulipwa ni 10% sasa bora unak nyumbani ulime mchicha.
 
Kazi kweli kweli,,, unaweza kuonekana unaamka asbh umenyonga tai smart kabisa,,,kumbe hupewi mshahara unakopwa
 
Back
Top Bottom