Mara zote matarajio ya mtumishi hasa pale uongozi mpya unapoingia madarakani huwa ni positive. Kipindi cha Benno Malisa tulikuwa tunapata mishahara kwa wakati. Sadifa alikuwa anachelewa 10-15 days then tunapata mishahara. Sasa Kheri tokea aingie madarakani ni zaidi ya miezi 9 sasa, hali yetu inakuwa mbaya as days goes on. Ninapoandika uzi huu ni zaidi ya miezi mitatu sasa hatujalipwa. Sasa sijui anategemea tutaishi vipi wakati yeye anazunguka nchi nzima kufanya ziara ambazo hata impact zake hatuzioni.
Dr. Bashiru tafadhali tusaidie katika hili. tuna familia, watoto, ndugu na majamaa wanaotutegemea. Na wengine tunasomesha watoto. Tunaomba utusaidie katibu Mkuu. hali ya maisha ni ngumu sana, tunaomba utuokoe