Watumishi tumechoka kuhakikiwa

Watumishi tumechoka kuhakikiwa

nasikia zoezi ni endelevu haliishi leo wala kesho....kwa vile watumishi hewa huzaliwa kila leo..wapo wanaokufa,wagonwa,wanaostaafu,wanaoenda masomoni,na wanaoamua kuacha kazi bila kutoa taarifa kila wakati.
 
Kubadilishia gia angani kunawatafuna ndani kW ndani. Sio jambo dogo kutumia mwendokasi kutangaza elimu bure japo imefaidish na inaendelea kufaidish wengi.nikuonean huruma tu hamna namna mzigo aloubeba sio Wa kutua Leo. Aisee mtapigwa sn danadana.
 
bado hapajafikia pa kumkumbuka JK kabisa mkuu....wacha tuhakikiwe kuna watu walikuwa wanatunyonya mkuu
JPM anasema kila siku lakini watu hawamuelewi. Watu walikuwa wanajineemesha kwa kasi wakitumia watumishi hewa. Wengine hawana vyeti sasa waachwe tu?
 
Mambo bado jamani tuvumilie huu mchezo hauhitaji hasira!!

Uhakiki unaofuata ni kujua Kama mfanyakazi mke au mume aliyenaye ni wake kweli au fake.

Halafu Uhakiki watoto wa mfanyakazi ili tujue wake kweli au kabambikiwa tuu.Hapo sasa naona tutapelekwa kwa mkemia Mkuu wa serikali kupima D.N.A.

Mambo haya yanaenda kwa vipaumbele. Kipaumbele cha Taifa kwa sasa ndo hiki.
Wanahakiki na jinsia yako, ni me au ke kweli? hahahahaaa
 
Tunashukuru zoezi hili lirudiwe ;mara ya kwanza lilifanyika kimizengwe chini ya Wakurugenzi watiifu kwa Edo.

Tunaomba wakurugenzi wapya wahakiki upya , Chini ya Magufuri.

Tuhakikiwe vyeti na nafasi tulizonazo kama kweli zinaendana na level ya Elimu.

Ata iwe miezi 6 ; hAKI ITENDEKE

WAKURUGENZI WAHAKIKI VYEO VYA WATUMISHI NA MISHAHARA INAENDANA NA TAALUMA ZAO.
Ni kweli kunawatu walikua wakipandishwa madaraja kwa ujanjaujanja, na mtu mwngne unakuta n diploma holder cha kushangaza mshahara wake anaanza na ule wa degree holder.acha tuendelee kuisoma namba tukisubir HAKI
 
Wanapewa muda kukimbia wenyewe bila kusumbua wahakiki.
haya ndo madhara ya upole kuzidi kiasi maana watawala wanaweza kufanya lolote lile kwakujua kua hawezi kufanyiwa lolote na watawaliwa coz huwezi kumlaza mlipakodi njaa huku ukisema unamkagua how comes? but kwasababu tulimchagua sisi wenyewe acha tuione mbombo acha tuhakikiwe tu mpaka ajiridhishe
 
Morali na ufanisi wa kazi kwa watumishi wa umma umeshuka sana. Hili zoezi linaanza kuwa la kisiasa sana maana binafsi sioni mantiki ya zoezi hili kuambatana na kusitisha nyongeza za mishahara,promisheni,ajira mpya na mabadiliko ya mishahara kwa waliohama ofisi kwa kipindi kirefu hivi cha miezi zaidi ya mi4.

Alisema lengo lake sio ku-frustrate watumishi wa umma lakini kiuhalisia tupo frustrated na desperate sana.
 
Hu
mkuu.

uhakiki lazima ufanyike...

nashukuru unaelewa kwamba yapo madai mengi ya walimu na wafanyakazi wengine ya posho ya likizo au uhamisho....
ni afadhari uhakiki ufanyike kuepuka kuwalipa wafanyakazi hewa au wasio na vigezo
Huo uhakiki mbona taasisi zingine haujatufikia? Mrejesho nao utachukua muda
 
Wakuu habari za J'mosi..

Kuna jambo linanishangaza kidogo kuhusu utendaji kazi wa hii awamu ya "hapa kazi tu"
Jambo lenyewe ni hili la watumishi wa serikali kutopewa stahiki zao mfano malimbikizo ya mshahara,kupandishwa vyeo,kulipwa likizo,kuajiliwa kwenye utumishi wa umma n.k kwa sababu ambayo ni "very minor" eti uhakiki wa watumishi hewa!!

Miongoni mwa maswali nayojiuliza ni haya;

1.Mh. Alipoingia alianzisha hili zoezi mpaka kufikia watumishi waliopo masomoni walirudi kwenye vituo vyao vya kazi ili kuhakikiwa,ilifikia mpaka baadhi ya viongozi na watumishi wengine wa halmashauri walitumbuliwa sababu ya kukwamisha zoezi hili,hivi ukaguzi ule ulitekelezwa kwa kukurupuka?Hatuwezi kusimamia jambo kiukamilifu mpaka kurudia rudia?

Najiuliza hayo maana watumishi na wanaosubiri ajira utumishi wa umma wanateseka kwa kukosa stahili zao kama nilivyoeleza hapo awali kwa sababu zisizo na tija.

2.Kwa ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia,rasilimali watu/wataalam wa IT tuliona na kwa idadi ya watumishi wa umma ni kweli serikali imeshindwa kufanya haya kwa wakati mmoja?yani kuhakiki waliopo na kuajili wapya?

Tanzania ina idadi ya watumishi wa umma wasiozidi laki sita(kama sijakosea),kweli tumeshindwa kuhakiki idadi hiyo kwa muda mfupi mpaka program ichukue muda muda mrefu hv?Ni kheri wale wataalam wa Rwanda wake basi kutusaidia,ili haki za watumishi zipatikane haraka(Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini).

Isije kua serikali inafanya haya kiujanja ujanja pale bajeti ya kuwalipa watumishi inapokua finyu na kutumia sababu za watumishi hewa na uhakiki ili kupata muda wa kujipanga,maana kama kweli ni uhakiki zoezi lisingeenda slow hivi kama nilivyoeleza hapo juu #2.

Karibu tujadili kwa pamoja,tokwa povu ila usitukane...
Acha kazi kama umechoka kuhakikiwa
 
hii ni geresha tuuu. maana mkuu wa nchi anachezea akili zetu mbona hao watumishi hewa atuwaoni...? maana mimi nilitegemea kuwa magereza yangejaa watumishi hewa ila tokea zoezi lianze nasikia tuu kama tetesi kuwa kulikuwa na watumishi hewa ina maana siku hizi mkono wa serikali umekuwa mdogo sana
 
Mi natabiri miaka miwili badae hali itakuwa mbaya zaidi kwa watumishi anayeamini aamini asiye amini sawa
 
hii ni geresha tuuu. maana mkuu wa nchi anachezea akili zetu mbona hao watumishi hewa atuwaoni...? maana mimi nilitegemea kuwa magereza yangejaa watumishi hewa ila tokea zoezi lianze nasikia tuu kama tetesi kuwa kulikuwa na watumishi hewa ina maana siku hizi mkono wa serikali umekuwa mdogo sana
kama ni hewa utawaonaje? labda wanaoweza kupatikana ni hao waliofanikisha kuwepo kwa watumishi hewa
 
Back
Top Bottom