Watumishi tumechoka kuhakikiwa

Watumishi tumechoka kuhakikiwa

Sheikh23

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Posts
1,202
Reaction score
2,001
Wakuu habari za J'mosi..

Kuna jambo linanishangaza kidogo kuhusu utendaji kazi wa hii awamu ya "hapa kazi tu"
Jambo lenyewe ni hili la watumishi wa serikali kutopewa stahiki zao mfano malimbikizo ya mshahara,kupandishwa vyeo,kulipwa likizo,kuajiliwa kwenye utumishi wa umma n.k kwa sababu ambayo ni "very minor" eti uhakiki wa watumishi hewa!!

Miongoni mwa maswali nayojiuliza ni haya;

1.Mh. Alipoingia alianzisha hili zoezi mpaka kufikia watumishi waliopo masomoni walirudi kwenye vituo vyao vya kazi ili kuhakikiwa,ilifikia mpaka baadhi ya viongozi na watumishi wengine wa halmashauri walitumbuliwa sababu ya kukwamisha zoezi hili,hivi ukaguzi ule ulitekelezwa kwa kukurupuka?Hatuwezi kusimamia jambo kiukamilifu mpaka kurudia rudia?

Najiuliza hayo maana watumishi na wanaosubiri ajira utumishi wa umma wanateseka kwa kukosa stahili zao kama nilivyoeleza hapo awali kwa sababu zisizo na tija.

2.Kwa ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia,rasilimali watu/wataalam wa IT tuliona na kwa idadi ya watumishi wa umma ni kweli serikali imeshindwa kufanya haya kwa wakati mmoja?yani kuhakiki waliopo na kuajili wapya?

Tanzania ina idadi ya watumishi wa umma wasiozidi laki sita(kama sijakosea),kweli tumeshindwa kuhakiki idadi hiyo kwa muda mfupi mpaka program ichukue muda muda mrefu hv?Ni kheri wale wataalam wa Rwanda wake basi kutusaidia,ili haki za watumishi zipatikane haraka(Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini).

Isije kua serikali inafanya haya kiujanja ujanja pale bajeti ya kuwalipa watumishi inapokua finyu na kutumia sababu za watumishi hewa na uhakiki ili kupata muda wa kujipanga,maana kama kweli ni uhakiki zoezi lisingeenda slow hivi kama nilivyoeleza hapo juu #2.

Karibu tujadili kwa pamoja,tokwa povu ila usitukane...
 
inakera sana na inaashiria ni namna gani watumishi wa uma tanadharirika na viongoz wa kisiasa wana Uhuru wa kutunyanyasha na kuvunja sheria, hivi kwan polisi sio watumishi wa uma? Mbona vyeo wamepanda!? What about us? Hivi TUCTA inafanya kazi gani maana wananitia hasira tu, hata increment jamani?? Haya mambo yanatia kichefu chefu sana
 
Mambo bado jamani tuvumilie huu mchezo hauhitaji hasira!!

Uhakiki unaofuata ni kujua Kama mfanyakazi mke au mume aliyenaye ni wake kweli au fake.

Halafu Uhakiki watoto wa mfanyakazi ili tujue wake kweli au kabambikiwa tuu.Hapo sasa naona tutapelekwa kwa mkemia Mkuu wa serikali kupima D.N.A.

Mambo haya yanaenda kwa vipaumbele. Kipaumbele cha Taifa kwa sasa ndo hiki.
 
Kwa kweli watumishi wa umma tuna madai mengi lkn kila siku wanakwambia jaza form...bado yanahakikiwa uhakiki gani usiokwisha? Kigumu ni nini hapo? Sasa tunazisoma namba za siri....
 
Kwa kweli watumishi wa umma tuna madai mengi lkn kila siku wanakwambia jaza form...bado yanahakikiwa uhakiki gani usiokwisha? Kigumu ni nini hapo? Sasa tunazisoma namba za siri....

mkuu.

uhakiki lazima ufanyike...

nashukuru unaelewa kwamba yapo madai mengi ya walimu na wafanyakazi wengine ya posho ya likizo au uhamisho....
ni afadhari uhakiki ufanyike kuepuka kuwalipa wafanyakazi hewa au wasio na vigezo
 
Back
Top Bottom