Watumishi tumechoka kuhakikiwa

Watumishi tumechoka kuhakikiwa

Wakuu habari za J'mosi..

Kuna jambo linanishangaza kidogo kuhusu utendaji kazi wa hii awamu ya "hapa kazi tu"
Jambo lenyewe ni hili la watumishi wa serikali kutopewa stahiki zao mfano malimbikizo ya mshahara,kupandishwa vyeo,kulipwa likizo,kuajiliwa kwenye utumishi wa umma n.k kwa sababu ambayo ni "very minor" eti uhakiki wa watumishi hewa!!

Miongoni mwa maswali nayojiuliza ni haya;

1.Mh. Alipoingia alianzisha hili zoezi mpaka kufikia watumishi waliopo masomoni walirudi kwenye vituo vyao vya kazi ili kuhakikiwa,ilifikia mpaka baadhi ya viongozi na watumishi wengine wa halmashauri walitumbuliwa sababu ya kukwamisha zoezi hili,hivi ukaguzi ule ulitekelezwa kwa kukurupuka?Hatuwezi kusimamia jambo kiukamilifu mpaka kurudia rudia?

Najiuliza hayo maana watumishi na wanaosubiri ajira utumishi wa umma wanateseka kwa kukosa stahili zao kama nilivyoeleza hapo awali kwa sababu zisizo na tija.

2.Kwa ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia,rasilimali watu/wataalam wa IT tuliona na kwa idadi ya watumishi wa umma ni kweli serikali imeshindwa kufanya haya kwa wakati mmoja?yani kuhakiki waliopo na kuajili wapya?

Tanzania ina idadi ya watumishi wa umma wasiozidi laki sita(kama sijakosea),kweli tumeshindwa kuhakiki idadi hiyo kwa muda mfupi mpaka program ichukue muda muda mrefu hv?Ni kheri wale wataalam wa Rwanda wake basi kutusaidia,ili haki za watumishi zipatikane haraka(Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini).

Isije kua serikali inafanya haya kiujanja ujanja pale bajeti ya kuwalipa watumishi inapokua finyu na kutumia sababu za watumishi hewa na uhakiki ili kupata muda wa kujipanga,maana kama kweli ni uhakiki zoezi lisingeenda slow hivi kama nilivyoeleza hapo juu #2.

Karibu tujadili kwa pamoja,tokwa povu ila usitukane...
Mbona wanafunzi hawajachoka kuitwa majina darasani. Kuwa mpole hili zoezi ni la muda tu. Mbona watanzania mara nyingi kwenye maswala nyeti tunafanya mizaha?
 
Hii serikal haina vipaumbele...TRA wanajigamba kuvunja record ya mapato lkn wanafunz wanakosa mkopo...reason..tunahakiki f***ck
 
Du! Kama haya yote aliyofanya Mkubwa we hujayaona basi hutaona hata akikupandisha cheo. Pia ikumbukwe kuing'oa system iliyojengwa tangu enzi hizo sio kazi ndogo lazima wenye upeo mdogo watamlaumu tu.
Ndugu Muyanza, ni kweli bwana mkubwa anafanya mema lakini Kwanini huu wema ufanyike kwa kunyima haki stahiki za walio wema? Huoni kama hayo malimbikizo yanaendelea kulimbikizwa?
 
Tuvute subra, kama ndio mbinu yake atafika mwisho tu ila kwenye uhakiki kuna wakubwa ambao hawatendi vyema wajibu wao ndio maana naona hii mambo inakuwa ya kurudia rudia. Mi naona Rais angeandaa kifaa maalum cha finger print ambacho kila Mfanyakazi wa Serikali awe anaweka dole gumba mara mbili kwa mwezi popote alipo. Mfano wewe ni mwalimu wa Arusha ila upo Mbeya unasoma utaandikiwa barua na Mkuu wako wa shule ili uruhusiwe kuchomeka dole lako kwenye shule iliyopo karibu na chuo chako, na hizo mashine ziwekwe kwenye Ofisi za Wakuu wa shule tu au wakuu wenye dhamana ya watu ili pakiwa na Mfanyakazi hewa tumtumbue vizuri.

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo kitu inaitwa time genius ni nzuri na haina udanganyafu ni nzuri iwekwe ofisi zote za Serikali mkuu.
 
Wakuu habari za J'mosi..

Kuna jambo linanishangaza kidogo kuhusu utendaji kazi wa hii awamu ya "hapa kazi tu"
Jambo lenyewe ni hili la watumishi wa serikali kutopewa stahiki zao mfano malimbikizo ya mshahara,kupandishwa vyeo,kulipwa likizo,kuajiliwa kwenye utumishi wa umma n.k kwa sababu ambayo ni "very minor" eti uhakiki wa watumishi hewa!!

Miongoni mwa maswali nayojiuliza ni haya;

1.Mh. Alipoingia alianzisha hili zoezi mpaka kufikia watumishi waliopo masomoni walirudi kwenye vituo vyao vya kazi ili kuhakikiwa,ilifikia mpaka baadhi ya viongozi na watumishi wengine wa halmashauri walitumbuliwa sababu ya kukwamisha zoezi hili,hivi ukaguzi ule ulitekelezwa kwa kukurupuka?Hatuwezi kusimamia jambo kiukamilifu mpaka kurudia rudia?

Najiuliza hayo maana watumishi na wanaosubiri ajira utumishi wa umma wanateseka kwa kukosa stahili zao kama nilivyoeleza hapo awali kwa sababu zisizo na tija.

2.Kwa ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia,rasilimali watu/wataalam wa IT tuliona na kwa idadi ya watumishi wa umma ni kweli serikali imeshindwa kufanya haya kwa wakati mmoja?yani kuhakiki waliopo na kuajili wapya?

Tanzania ina idadi ya watumishi wa umma wasiozidi laki sita(kama sijakosea),kweli tumeshindwa kuhakiki idadi hiyo kwa muda mfupi mpaka program ichukue muda muda mrefu hv?Ni kheri wale wataalam wa Rwanda wake basi kutusaidia,ili haki za watumishi zipatikane haraka(Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini).

Isije kua serikali inafanya haya kiujanja ujanja pale bajeti ya kuwalipa watumishi inapokua finyu na kutumia sababu za watumishi hewa na uhakiki ili kupata muda wa kujipanga,maana kama kweli ni uhakiki zoezi lisingeenda slow hivi kama nilivyoeleza hapo juu #2.

Karibu tujadili kwa pamoja,tokwa povu ila usitukane...
Zamani tulikua tunaona ajira ya serikali ni security but siku hizi imekua sivyo kabisaaa,ni wakati sasa umefika kuangalia njia mbadala.....
 
kupekuliwa sio tatizo,
tatizo ni kusitisha watu kupanda madaraja na wengine wa ajira mpya kurudishwa nyumbani bila kujua ni lini hili zoezi linaisha.

Tunashukuru zoezi hili lirudiwe ;mara ya kwanza lilifanyika kimizengwe chini ya Wakurugenzi watiifu kwa Edo.

Tunaomba wakurugenzi wapya wahakiki upya , Chini ya Magufuri.

Tuhakikiwe vyeti na nafasi tulizonazo kama kweli zinaendana na level ya Elimu.

Ata iwe miezi 6 ; hAKI ITENDEKE

WAKURUGENZI WAHAKIKI VYEO VYA WATUMISHI NA MISHAHARA INAENDANA NA TAALUMA ZAO.

Unafaham kuwa hata hao wakurugenz baadhi yao wana mishahara mikubwa lakin elm zao ni ndogo
 
Samaki wanamezana mkubwa kabisa anammeza anayemzidi na kuendelea. Watumishi wanakwamishana wenyewe kwa sababu kila hatua inaanzia kwa mtumishi kwenda kwa watumishi wenzake!
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Unafaham kuwa hata hao wakurugenz baadhi yao wana mishahara mikubwa lakin elm zao ni ndogo
wakurugenzi wapo chini ya Raisi ; Raisi anataratibu zake ; Ukurugenzi hauna taaluma ni usimamizi
; Lakini Vitengo/ Idara za halmashauri Taaluma lazima
 
inakera sana na inaashiria ni namna gani watumishi wa uma tanadharirika na viongoz wa kisiasa wana Uhuru wa kutunyanyasha na kuvunja sheria, hivi kwan polisi sio watumishi wa uma? Mbona vyeo wamepanda!? What about us? Hivi TUCTA inafanya kazi gani maana wananitia hasira tu, hata increment jamani?? Haya mambo yanatia kichefu chefu sana
Well said
 
Back
Top Bottom