Watumishi tuache tabia ya kudai kudai tu, tuishukuru serikali

Kyambamasimbi

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
569
1,214
Mama anaupiga mwingi,

Kwanza tutambue serikali ina mengi ya kufanya hasa kuboresha huduma za kijamii ambazo husaidia wote watumishi na wasiowatumishi, mfano barabara, hosptali, shule vyuo, kilimo na mengine mengi.

Tuache ubanafsi tuwe wavumilivu Mambo yatakuwa mazuri tu kila kitu kinakwenda kwa mipango. Hongera Mama SAMIA hongera Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Mnaupiga mwingi.
 
Serikali iache kuwahadaa watumishi kulikua na haja gani kujinasibu kila siku kwenye vyombo vya habari kuwa tumeongeza mishahara ya kihistoria watu watapagawa kwa ongezeko ilo la 23.3

Mwisho wa siku mnakuja na kituko icho mfyuuuuu dadek hamna kitu huyu mama hafai kukaa pale ikulu Vinginevyo avunje genge lake la wapiga dili na abadilike
 
Unajua ni kiasi gani watumishi wanalipa kodi ktk nchi hii. !??
 
Mama anaupiga mwingi, Kwanza tutambue serikali ina mengi ya kufanya hasa kuboresha huduma za kijamii ambazo husaidia wote watumishi na wasiowatumishi, mfano barabara,hosptali,shule vyuo, kilimo na mengine mengi. Tuache ubanafsi tuwe wavumilivu Mambo yatakuwa mazuri tu kila kitu kinakwenda kwa mipango. Hongera Mama SAMIA hongera DKT. Mwigulu Lameck Nchemba Mnaupiga mwingi.
...Wewe kuanzia Leo ni BALOZI wa Sri Lanka....!
 
Unajua ni kiasi gani watumishi wanalipa kodi ktk nchi hii. !??
Kwani watumishi wanalipa Kodi kuliko wafanyabiashara wa madini?? Au makampuni?? Au Kodi gani unayoisemea na kila mtu analipa Kodi nchi hii.
 
Mama anaupiga mwingi, Kwanza tutambue serikali ina mengi ya kufanya hasa kuboresha huduma za kijamii ambazo husaidia wote watumishi na wasiowatumishi, mfano barabara,hosptali,shule vyuo, kilimo na mengine mengi. Tuache ubanafsi tuwe wavumilivu Mambo yatakuwa mazuri tu kila kitu kinakwenda kwa mipango. Hongera Mama SAMIA hongera DKT. Mwigulu Lameck Nchemba Mnaupiga mwingi.
Wewe uvccm, acha uwafanyia utani watu wenye akili zao timamu. Hawa siyo wake mnao wadanganya kwa kofia, kanga, vitenge, na vilemba wakati wa zile kampeni zenu za kuzugia huku mkiwa na matokeo yenu mfukoni.
 
Serikali iache kuwahadaa watumishi kulikua na haja gan kujinasibu kila siku kwenye vyombo vya habari kuwa tumeongeza mishahara ya kihistoria watu watapagawa kwa ongezeko ilo la 23.3

Mwisho wa siku mnakuja na kituko icho mfyuuuuu dadek hamna kitu huyu mama hafai kukaa pale ikulu Vinginevyo avunje genge lake la wapiga dili na abadilike
Ni upuuzi mtupu .
 
Kushukuru ni jambo lingine, suala ni kwanini serikali itoe tamko ambalo kuitekeleza kwake ni vigumu.
 
Mbona na ccm nayo imejaa ubinafsi. Kwa nini haikubali kushindwa kwenye uchaguzi?
Ndio maane hata wewe unapata hata nafasi ya kuchati na unalala mpaka saa nne unaamka unaenda kutafuta riziki kwa amani bila kusikia mlio wa risasi.
 
Ndio maane hata wewe unapata hata nafasi ya kuchati na unalala mpaka saa nne unaamka unaenda kutafuta riziki kwa amani bila kusikia mlio wa risasi.
Ndivyo mnavyo wadanganya Watanzania wajinga miaka nenda. Eti mkichagua upinzani, kutatokea vita!

2025 lazima mtoke madarakani. Tumeshawachoka. Nyinyi wenyewe mnaishi maisha ya anasa, halafu manata sisi tuishi maisha kama mashetani.
 
Back
Top Bottom