Watumishi majizi na wazembe Sekta ya Afya ndiyo wanaoongoza kumpinga Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima

Hizo swaga namuonaga mama mwingine wa baraza moja la kitaaluma huwa anazo sana.Sidhani kama ni rahisi kuwabadilisha ila tu kama wako kwenye haki acha wafanye tu,ndio kina mama wetu wa kiafrika.Hawaja ji edit,wako kihalisia,hawafeki mannerism zao.

Mungu awape hekima tu wasionee wala kunyanyasa mtu asiye na hatia
Bonge la comment yaani. Bigup
 
Huwezi iba dawa za GOT kibiashara. Ukiona mtumishi kaiba ujue kaiba dozi moja au mbili akatumie au ampe mshkaji wake.
Kesi zote za watu wezi huzijui? Hujasikia wale wezi wa Hospitali ya Nansio wa dawa za Milioni 200?
 
Zunguka famasi zote mjini kanunue dawa kama utapata ya GOT, hakuna mfanyabiashara mjinga anaweza uza dawa za GOT. Na ndio maana husikii serikali ikisema imekamata dawa zake zikiuzwa sehemu fulani. Na kama unafuatilia kwa makini utagundua hizi kelele za wizi wa dawa hakuna mtu anakamatwa na bado hakuna dawa hospitalini. Nimekwambia swala la dawa hospitalini ni pana zaidi ya ngonjera za kuwa watumishi wanaiba

Watu tunajua vizuri dawa nyingi mnaiba .... NYINYI NI WEZI WA DAWA MNAPELEKA PHAMACY
 
Mbona mnatumia nguvu nyingi sana?

Nyie wezi wa dawa ndio mnatumia nguvu nyingi sana kumchafua huku mitandaoni kwa kuona anawazibia mianya yenu ya wizi.
Watumishi wa afya (wale wezi na wazembe) Mungu anawaona, watu wanakufa kwa kukosa huduma wakati nyie mkijinufaisha binafsi isivyohalali kwa kutumia dhida za watu maskini. Damu za hao watu zitadaiwa mikononi mwenu.
 
Nyie wezi wa dawa ndio mnatumia nguvu nyingi sana kumchafua huku mitandaoni kwa kuona anawazibia mianya yenu ya wizi.
Watumishi wa afya (wale wezi na wazembe) Mungu anawaona, watu wanakufa kwa kukosa huduma wakati nyie mkijinufaisha binafsi isivyohalali kwa kutumia dhida za watu maskini. Damu za hao watu zitadaiwa mikononi mwenu.
Tena mikononi yao inanuka damu kabisa za watu waliokufa kwa kukosa dawa na vifaa tiba muhimu walivyo hujumu mahospitalini
 
Acha ufala watu tunajua vizuri dawa nyingi mnaiba .... NYINYI NI WEZI WA DAWA MNAPELEKA PHAMACY
Wakamate! Tueleze hapa nna hospital za serikali zinavyo nunua dawa toka MSD kwa mwaka. Isipayuke kama gwajima
 
Mahospitalini Kuna ubadhirifu wa fedha za umma kupitia WIZI wa MADAWA, kuchukua rushwa kwa Wagonjwa, kufanya uharibifu wa makusudi wa vifaa tiba ili visiwe vinafanya kazi na kisha wagonjwa waelekezwe hospitali binafsi za watumishi hao...
Hayo matatizo yapo kila sekta , na usitegemee kuwa yatamalizwa na ONE MAN SHOW!! bali ni mifumo imala, ndio maana huwa unaona kwa wazungu hakuna kutumia nguvu bali watu wanaendeshwa na mifumo imala tu!!huu ni mwaka wa sita toka awamu ya tano, iingie madarakani lakini bado changamoto, ni zile zile, licha ya kila leo watu kufukuzwa na kuingia wengine!!

Huyo waziri wa afya atatoka ataingia mwingine, madudu bado ni yale yale tu!!huko bandarini jpm amekwenda mala ngapi ametimuwa watu, waziri mkuu, hivyo hivyo, lakini hata akienda leo, lazima atakutana na madudu tu!!!vile vile angalieni na stahiki zao, miaka mitano, stahiki zao nyingi zimesimama , maisha kila leo yanapanda, utegemee ufanisi!!?dawa hakuna ni kosa la daktari?eti dawa zinaibiwa !!!mtoto chini ya miaka mitano matibabu ni bure?!!kweli hiyo huduma ipo wapi?
 
Hayo matatizo yapo kila sekta , na usitegemee kuwa yatamalizwa na ONE MAN SHOW!!bali ni mifumo imala, ndio maana huwa unaona kwa wazungu hakuna kutumia nguvu bali watu wanaendeshwa na mifumo imala tu!!huu ni mwaka wa sita toka awamu ya tano, iingie madarakani lakini bado changamoto, ni zile zile, licha ya kila leo watu kufukuzwa na kuingia wengine!!huyo waziri wa afya atatoka ataingia mwingine, madudu bado ni yale yale tu!!huko bandarini jpm amekwenda mala ngapi ametimuwa watu, waziri mkuu, hivyo hivyo, lakini hata akienda leo, lazima atakutana na madudu tu!!!vile vile angalieni na stahiki zao, miaka mitano, stahiki zao nyingi zimesimama , maisha kila leo yanapanda, utegemee ufanisi!!?dawa hakuna ni kosa la daktari?eti dawa zinaibiwa !!!mtoto chini ya miaka mitano matibabu ni bure?!!kweli hiyo huduma ipo wapi?
Sijui kwa nini tunaweka visingizio dhaifu kiasi hiki! Stahiki ndo ikufanye uibe dawa? Nchi gani inayotoa stahiki na imekomesha wizi? Wizi ni tabia tu!
 
Hatukatai anafanya kazi vizuri...Ila hiyo njia ya Uwasilishaji kama anamchamba mke mwenzie ndio hatukubaliani nao.
 
Mzani unaegemea upande mmoja mmeshindwa kuboresha maslahi why wizi usitokee? Boresheni maslahi muone kama wizi utakuwepo
 
Bajeti ya dawa kwa mtanzania mmoja bunge linapitisha shilingi ngapi? sijasikia bunge la bajeti lililopita halikuoneka kwenye tv
.
 
Mahospitalini Kuna ubadhirifu wa fedha za umma kupitia WIZI wa MADAWA, kuchukua rushwa kwa Wagonjwa, kufanya uharibifu wa makusudi wa vifaa tiba ili visiwe vinafanya kazi na kisha wagonjwa waelekezwe hospitali binafsi za watumishi hao.
Nani asiyejua namna watumishi wa Afya ( madaktari na manesi) wanavyoiibia serikali pesa kwa kuchukuwa pesa kwa wagonjwa. Mnachukua pesa kwa wagonjwa, risiti hamtoi zinaingia mifukoni mwenu halafu mnakuja piga kelele kuwa hospitali haina dawa na vitendanishi ili hali pesa ambazo hospitali ingezitumia kununulia vitu hivyo imeingia mifukoni mwenu?
Anachokifanya Dr Dorothy Gwajima ni kuwafumbua macho wananchi, kurudisha uwajibikaji kwa watumishi wa sekta ya umma ya Afya.

Wananchi mnayotendewa Hospitali za serikali siyo mnayotendewa Hospitali binafsi.
Daktari ukimkuta Hospitali ya serikali huwa hana Good customer care, lakini daktari huyo huyo mkute Private hospital hutaamini kwa ukarimu atakao kuonyesha.

Kiufupi viongozi MAHOSPITALINI huandaa taarifa nyingi za uongo anapokuja waziri husika. Sasa kumdanganya huyu waziri wa sasa lazima uwe na PhD ya uongo.
Nani asiyejua kuwa madaktari Bingwa wengi ikifika saa nne asubuhi wanaondoka kwenye hospitali za serikali wanakolipwa mishahara na wamakwenda kufanya kazi kwenye hospitali binafsi ndani ya muda wa kazi wa serikali? Kwanini waziri akiwabana mnaanza kulialia?
Hivi ni mwananchi gani asiyefahamu lugha za karaha kutoka kwa wahudumu wa Afya? Hilo nalo waziri anapolikemea mnasema anawasuta?
Vifo vingapi vinasababishwa na uzembe wa watoa huduma mahospitalini? Waziri anapotoa ujumbe kuwa madaktari wapite ward rounds zote inavyotakiwa kwanini mnanuna?
Nenda mahospitalini kipindi hiki mambo yameanza kubadilika kabisa kisa kumhofia Mheshimiwa waziri.
Ukweli ndiyo huo
Hongera kwa Field Marshal Iron lady katika uongozi wa sekta ya afya.
 
Bajeti ya dawa kwa mtanzania mmoja bunge linapitisha shilingi ngapi? sijasikia bunge la bajeti lililopita halikuoneka kwenye tv
.
hiyo bajeti ndogo au kubwa ilitumikaje ...hilo ndio swali la waziri kwetu
 
Sijui kwa nini tunaweka visingizio dhifu kiasi hiki! Stahiki ndo ikufanye uibe dawa? Nchi gani inayotoa stahiki na imekomesha wizi? Wizi ni tabia tu!
Sio kwamba wizi utaumaliza lakini njaa ni kishawishi kikubwa sana!!wala tatizo la ukosefu wa dawa mahospitalini sio wizi wa madawa!!tu bali bajeti haitosherezi kupeleka madawa, juzi nilikuwa wilaya ya tanganyika ni aibu!!viongozi wasitafute watu wa kuwatwisha mzigo!!
 
Back
Top Bottom