COARTEM
JF-Expert Member
- Nov 26, 2013
- 3,598
- 3,644
Mahospitalini Kuna ubadhirifu wa fedha za umma kupitia WIZI wa MADAWA, kuchukua rushwa kwa Wagonjwa, kufanya uharibifu wa makusudi wa vifaa tiba ili visiwe vinafanya kazi na kisha wagonjwa waelekezwe hospitali binafsi za watumishi hao.
Nani asiyejua namna watumishi wa Afya (madaktari na manesi) wanavyoiibia serikali pesa kwa kuchukuwa pesa kwa wagonjwa. Mnachukua pesa kwa wagonjwa, risiti hamtoi zinaingia mifukoni mwenu halafu mnakuja piga kelele kuwa hospitali haina dawa na vitendanishi ili hali pesa ambazo hospitali ingezitumia kununulia vitu hivyo imeingia mifukoni mwenu? Anachokifanya Dr Dorothy Gwajima ni kuwafumbua macho wananchi, kurudisha uwajibikaji kwa watumishi wa sekta ya umma ya Afya.
Wananchi mnayotendewa Hospitali za serikali siyo mnayotendewa Hospitali binafsi. Daktari ukimkuta Hospitali ya serikali huwa hana Good customer care, lakini daktari huyo huyo mkute Private hospital hutaamini kwa ukarimu atakao kuonyesha.
Kiufupi viongozi MAHOSPITALINI huandaa taarifa nyingi za uongo anapokuja waziri husika. Sasa kumdanganya huyu waziri wa sasa lazima uwe na PhD ya uongo.
Nani asiyejua kuwa madaktari Bingwa wengi ikifika saa nne asubuhi wanaondoka kwenye hospitali za serikali wanakolipwa mishahara na wamakwenda kufanya kazi kwenye hospitali binafsi ndani ya muda wa kazi wa serikali? Kwanini waziri akiwabana mnaanza kulialia?
Hivi ni mwananchi gani asiyefahamu lugha za karaha kutoka kwa wahudumu wa Afya? Hilo nalo waziri anapolikemea mnasema anawasuta?
Vifo vingapi vinasababishwa na uzembe wa watoa huduma mahospitalini? Waziri anapotoa ujumbe kuwa madaktari wapite ward rounds zote inavyotakiwa kwanini mnanuna?
Nenda mahospitalini kipindi hiki mambo yameanza kubadilika kabisa kisa kumhofia Mheshimiwa waziri.
Ukweli ndiyo huo