Watumishi hewa wasakwa serikalini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watumishi hewa wasakwa serikalini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Apr 20, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Posted on April 19, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora, Haji Omar Kheri akifanya majumuisho katika kikao cha baraza la wawakilishi

  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeahidi kuwatafuta wafanyakazi hewa ‘Gost Workers’ katika taasisi zake na mashirika ya umma na kuwachukulia hatua za kisheria watakaobainika na vitendo hivyo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora, Haji Omar Kheri amewaambie wajumbe wa baraza la wawakilishi jana wakati akifanya majumuisho ya ripoti ya kamati ya kuchunguza na kudhibiti hesabu za serikali na mashirika ya (P.A.C) ya mwaka wa 2011/2012 kuhusu ufuatiliaji hoja za ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu wa ya mwaka 2008.2009.
  Alisema zoezi la kuwatafuta wafanyakazi hewa wa serikali ilianza mwezi uliopita kwa watumishi wote kuhakikiwa upya na kutakiwa kuleta vieleelzo vyao ikiwemo kupokea mishahara yao wizarani kupitia kwa wahasibu.
  “Mheshimiwa Spika kazi ya kuwahakiki watumishi wa serikali imeanza na tunataka kujuwa idadi yao kamili na kutafuta watumishi hewa, pia tunawatafuta wale watumishi wanaopokea fedha mara mbili pamoja na wale ambao wamefariki lakini wameingizwa katika mtandao wa mishahara na wanalipwa licha ya kuwa wapo makaburini” alisema.
  Aidha Kheri alisema kazi hiyo ilianza kwa wizara ya miundombinu na mawasiliano, wizara ya elimu na mafunzo ya amali na wizara ya kazi na uwezeshaji wananchi kiuchumi na kuendelea katika wizara nyengine za serikali.
  Aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba kazi hiyo inaendelea hadi hapo serikali itakapojiridhisha na kuahidi kwamba zoezi hilo litakuwa endelevu kwa lengo la kuweka mipango mizuri ya maendeleo ya nchi na uwajibikaji.
  Kheri alisema kwa sasa zoezi la kuhakiki watumishi wa Serikali lipo katika vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar vya JKU, Vyuo vya Mafunzo, kikosi cha Zimamoto, KMKM na Valantia.
  Waziri huyo alisema lengo la serikali kuamua kufanya uhakikia huo kwa wafanyakazi ni kuona kwamba hakuna mtumishi anayepokea fedha kinyume na utaratibu wa sheria za utumishi serikalini.
  Aaliwaahidi wajumbe hao wa baraza kwamba uchunguzi zaidi wa kuweza kuwatambuwa watumishi hewa wanaochukuwa mishahara kinyume na sheria unaendelea na taarifa kamili zitatolewa mara zoezi hilo litakapomalizika.
  Alisema mafanikio hayo yamekuja baada ya Serikali kuchukuwa juhudi za makusudi kuijengea uwezo taasisi hiyo ambayo ni moja ya eneo la utawala bora katika kuendesha shunguli za Serikali.
  Mshimba aliomba radhi baraza la wawakilishi.
  HATIMAE Mwakilishi wa Jimbo la Kitope (CCM) Makame Mbarouk Mshimba jana ameliomba radhi Baraza la Wawakilishi hatua ambayo ni utekelezaji wa agizo alilopewa na Spika wa baraza hilo Pandu Ameir Kificho wiki iliyopita.
  Mbali ya kuliomba radhi baraza Mshimba pia amewaomba radhi wananchi wa Zanzibar na kumuomba radhi Spika wa baraza hilo kwa kushindwa kuwasilisha ripoti yake ya Mawasiliano na Ujenzi ya baraza la wawakilishi ambapo wakati akitajwa Mwenyekiti wa kamati hiyo kuja kuwasilisha ripoti yake hakuwepo barazani.
  Awali Spika Kificho mbele ya wajumbe wa baraza lake aliisoma barua iliyoandikwa na Mshimba akisema anawaomba radhi sana baraza na wananchi kutokana na kitendo hicho kilichotokea cha kushidnwa kuwasilisha ripoti yake kutokana na kudharurika siku hiyo.
  Mshimba alisema sababu kubwa iliyomkwamisha kufika katika kikao hicho ni kupata matatizo ya kiafya kutokaa na kuwa alikuwa akiumwa na tumbo lakini alichokosea ni kule kushindwa kuliarifu baraza na kumuarifu Spika juu ya tukio hilo.
  “Mheshimiwa Spika nilidharurika siku ile ambayo nilitakiwa kuwasilisha ripoti ya kamati yangu, kwa kweli nilikuwa nikiumwa na hivyo kushindwa kuhudhuria katika kikao nilikuwa nikiumwa na tumbo na kwa bahati mbaya nilishindwa kukuarifu na pia nilighafilika kwani sikuweza kumpa taarifa hiyo mjumbe mwengine yeyote” ilisema sehemu ya barua hiyo iliyowasilishwa kwa Spika.
  Katika barua yake Mwakilishi huyo aliahidi kwamba kitendo kilichotokea kitakuwa ni cha mwisho na hakitojirudia tena katika uhai wa Baraza la Wawakilishi.
  Spika Kificho aliwaambia wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kiwamba barua ya Mwakilishi huyo imempa matumiaoni hasa pale alipoahidi kwamba atahakikisha kitendo hicho hakitajirudia tena katika uhai wake.
  Katika kuhakikisha suala hilo halitokezei tena Spika aliwakumbusha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na mawaziri kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kuzingatia wajibu wao wa kuwawakilisha wananchi.
  Spika aliwataka wajumbe hao kuweka utaratibu mzuri na kufuata kanuni zilizowekwa na baraza hilo kwani wananchi wengi wanafuatilia vikao hivyo lakini pia umakini wa chombo hicho muhimu cha kutunga sheria kinategemea na uwajibikaji wa wajumbe wake ambao ni wawakilishi na mawaziri.
  Hivi karibuni Spika wa Baraza la Wawakilishi alikasirishwa na kitendo cha Mwenyekiti wa kamati ya Mawasiliano na Ujenzi, Makame Mshimba Mbarouk ambaye alishindwa kuwasilisha ripoti ya kamati hiyo kutokuwepo katika kikao hicho bila ya kutoa dharura kwa Spika.
  Spika alimtaka Mwakilishi huyo aliombe radhi baraza la wawakilishi na wananchi kutokana na kuwa wananchi wanafuatilia vikao hivyo na wanataka kuona uwajibikaji na umakini wa chombo hicho.
  “Waheshimwia wajumbe wa baraza la wawakilishi tunatakiwa tuwe makini sana wakati tukiendesha shunguli za baraza la wawakilishi zaidi katika kipindi hichi ambapo mijadala hii imekuwa ikirushwa hewani moja kwa moja na vyombo vya habari, wananchi wanataka kujua kila kinachoendelea hapa barazani” alisema Spika.
  Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC) na Zanzibar Cable zimekuwa zikirusha moja kwa moja matangazo ya vikao vya baraza la wawakilishi ambapo wananchi wengi wamekuwa wakifuatilia kwa umakini vikao hivyo.
  Udanganyifu wakosesha wafanyakazi fedha za likizo
  WIZARA ya Afya Zanzibar imesema udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wafanyakazi umechangia kuvuruga utaratibu wa kuwalipa wafanyakazi fedha za likizo.
  Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Duni Haji alisema hayo jana wakati akijibu maswali katika kikao kinachoendelea Chukwani Mjini hapa.
  Alisema kuwa hali hiyo ilisababisha serikali kuwa na utaratibu wa kuwalipa fedha hizo baada ya kutoka katika likizo zao.
  Duni alikuwa anajibu swali la Panya Ali Abdalla Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake (CCM) aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na serikali kulipa deni la fedha za likizo kwa wafanyakazi wa wizara ya afya.
  Mwakilishi huyo alisema kutolipa deni hilo kwa wafanyakazi kutapunguza moyo na ari kwa wafanyakazi kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
  Akijibu hilo la kutokuwepo ufanisi wa kazi Duni alisema “Wizara yangu inalielewa hilo na inaweza ikawa ni sababu moja wapo ya kupunguza ufanisi wa kazi”.
  Waziri Duni alisema chanzo ni udanganyifu miongoni mwa baadhi yao pamoja na ukosefu wa fedha kwa upande wa serikali.
  Alisema sababu za kutolipwa fedha za wafanyakazi kabla ya kwenda likizo ni huo udanganyifu unaofanywa na watumishi hao wa umma ambao wanaidanganya serikali.
  “Mheshimiwa Spika ni kweli wafanyakazi wengi hawajapata fedha za likizo, hii imetokana na kutokuwa na mpango endelevu wa malipo hayo, kubwa zaidi kuliko yote ni kulikuwa na udanganyifu wa kupindukia na ufinyu wa fedha kutoka serikalini” alisema Waziri huyo.
  Alisema upungufu huo ulisababisha utekelezaji wa haki hiyo kwa wafanyakazi kutolewa kwa misingi ya upendeleo na wengine kutolipwa kabisa.
  Katika hatua wanazozichukua kukabiliana na tatizo hilo, Waziri Duni alisema wizara yake inandaa utaratibu utakaowezesha kurugenzi ya fedha kutenga fungu kwa ajili ya malipo ya likizo badala ya kazi hiyo kupewa idara ya utumishi ya wizara hiyo.
  Akijibu suala la malipo ya sa za baada ya kazi (Overtime) Duni alisema utaratibu wa kulipa posho wafanyakazi wa afya kwa kufidia upungufu wa wafanyakazi haupo.
  Alisema posho huwa zinalipwa kwa wafanyakazi wa afya wale ambao hawaingii ‘shif’ na wanapoitwa kutoa huduma baada ya saa za kazi ndio wanaostahiki kupewa posho ‘overtime’.
  Aidha alisema katika kukabiliana na tatizo la uchache wa wafanyakazi wizara iliajiri wafanyakazi 162 mwaka 2010 amabo wamemaliza chuo cha sanyansi za afya Mbweni na asilimia 61 ya waajiriwa hao walipelekwa Pemba.
  Fedha za serikali na matumizi mabaya
  Wajumbe wa baraza la wawakilishi wameambiwa kuwa bado kumekuwepo na matumizi mabaya ya fedha za umma bila ya kuwa na vielelezo ambayo hufanywa na watu wenye mamlaka serikali.
  Akisoma muhrasari wa ripoti ya kamati ya kuchunguza na kudhibiti hesabu za serikali na mashirika (P.A.C) ya mwaka 2011/2012 Mwenyekiti wa Kamti hiyo Omar Ali Shehe alisema ripoti ya mwaka 2008/2009 imeonesha kuwa wakati wa ukaguzi wa mahesabu kwa taasisi mbali mbali, Jumla ya Tsh 5,170,000/ ambazo zilitumika kama malipo ya masurufu (Imprest) vielelezo vyake havikupatikana kuthibitisha uhalali wa malipo hayo.
  Akitaja ubadhirifu huo uliofanyika alisema Jumla ya Shilingi 29,251,380 zilitumika kununulia vifaa ambavyo havikuingizwa katika madaftari ya kuhifadhia (Store Ledger) ili kuthibitisha uhalali wa manunuzi hayo na Jumla ya Tsh 138,053,207 pamoja na Dola 94,209 zilitumika kama malipo ambayo hayakuwa na vielelezo ambapo jumla ya 103,294,571 zilitumika kama malipo ambayo hayakuwa na stakabadhi za malipo na Jumla ya shilingi 413,648,097 zilitumika katika malipo yasiyokuwa na Mikataba.
  “Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, wa Hesabu za Serikali ukaguzi unaonesha kuwa jumla ya fedha zote ambazo matumizi yake hayakuthibitika wakati wa ukaguzi ni Tsh 689,417,255” alisema Shehe.
  Akizungumzia suala la kukosekana vielelezo, Mwenyekiti huyo alisema ripoti imeonesha namna mali za Serikali zinavyokuwa hazikuwekewa kumbukumbu, kutofahamika thamani yake pamoja na kukosekana kwa hati miliki ya mali hizo. Kutokuwepo kwa mambo hayo kwa mali za umma zinazomilikiwa na Serikali, sio tu kunatoa fursa kwa wajanja wachache kujimilikisha, lakini pia tatizo hili linapelekea kuathiri sana mfumo mzima wa kimahesabu katika uchumi, pamoja na uhai wa taasisi hizo hususan taasisi za umma zinazojitegemea, kama vile Mashirika ya Umma.
  Aidha katika suala hilo kamati hiyo imependekeza serikali iandae muongozo wa utayarishaji wa daftari la kuwekea kumbukumbu za mali za Serikali kwa kila taasisi ya Umma pamoja na Serikali Kuu (Consolidated Asset Register), iaandae utaratibu wa kutathmini mali zote za Serikali hasa majengo,iandae utaratibu wa kuandaa Sera ya Ushukaji na Upandaji wa Thamani (Depreciation and Apreciation Policy), na iandae utaratibu wa kuzitoa (Disposal) mali ambazo ziko katika thamani inayokubalika kutolewa katika milki ya SerikaIi.
  “Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu imeripoti kasoro hii inayofanywa na baadhi ya Maafisa Wahasibu wa Taasisi zetu, kasoro ambayo huchangiwa zaidi na suala la kutokuwajibika na uzembe wa watendaji” alisema Mwenyeketi huyo.
  Mwenyekiti huyo aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, imeainisha mrundikano mkubwa wa madeni yanayotokana na Idara ya Nyumba kwa wananchi mbali mbali wanaoishi katika Nyumba za Maendeleo na zile zinazomilikiwa na Serikali.
  Alisema ripoti imeonyesha pia mrundikano wa madeni yanayo daiwa na Mamlaka ya Maji – ZAWA, Kama ni huduma ya maji kwa wananchi na taasisi mbali mbali za Umma na taasisi binafsi.
  “Kwa upande wa deni la Idara linalotokana na kodi za wateja wa majumbani ni shilingi 678,744,000, taasisi binafsi zinadaiwa shilingi 5,205,000 na taasisi za Serikali ni Shilingi 9,000,000 jumla ya deni lote kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti, ni shilingi 692,949,000 (Madeni haya ya Maji ni kwa upande wa Mamlaka ya Maji Pemba tu ambayo ndio Kamati iliyoifanyia kazi” alisema Mwenyekiti huyo.
  Wakati fedha za serikali zikiwa zimekosa vielelezo vinavyotakiwa pia ukosefu wa kutopatikana kwa tarifa juu ya fedha na vifaa vinavyotokana na wafadhili imeelezwa kuwa ni tatizo jengine linaloikabili serikali.
  “Katika mafunzo yaliyofanyika hivi karibuni, ambayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola- CPA yaliyofanyika Nchini Uingereza, ambayo yalihusu Kamati za PAC, suala hili liliibuka katika mjadala. Rai iliyotolewa katika mjumuiko wa wajumbe katika kutafakari namna ya kupata suluhisho la tatizo hilo linatokea baina ya wafadhili na wafadhiliwa ni kwamba, ilipendekezwa kuwa ili ionekane kuwa mikopo ama misaada hiyo inatumika vyema na inaleta faida kwa wananchi, moja kati ya masharti ya kuridhia misaada ama mikopo, iwe ni kwa kuwahusisha wakaguzi wa mahesabu wa pande zote zinazohusika kwa lengo la kupeana taarifa muhimu zinazohusiana na matumizi na ukaguzi wa fedha zilizotolewa na misaada mengine yote ya kifedha” alisema Mwenyekiti huyo.
   
Loading...