Watumiaji wa Apple (iOS) wana hatari ya kudukuliwa ikiwa hawajasasisha vifaa vyao

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Kwa muda mrefu, Apple imepongezwa kwa faragha na usalama wa watumiaji wake. Mfumo wa iOS, ulijijengea sifa ya kuwalinda watumiaji dhidi ya vitisho vya kidijitali. Hata hivyo, hakuna mfumo ambao hauwezi kushambuliwa kabisa.

Watafiti wa Citizen Lab na Kikundi cha Utafiti cha Usalama cha Google wamegundua uwezekano wa vifaa vya Apple kudukuliwa. Watafiti wamebaini udhaifu na kasoro kwenye WebKit, Safari browser, pia kwenye certificate verification, na udhaifu mwingine ulioruhusu ufikiaji mpana zaidi kwenye mfumo wa uendeshaji wa kifaa.

Hata hivyo, Apple imejibu haraka kwa kutoa sasisho za kurekebisha udhaifu huu, ikitoa njia ya kuwalinda watumiaji katika masuala ya faragha na usalama. Ikiwa una kifaa cha Apple - iwe ni Mac, iPhone, iPad, au Watch - unahimizwa kusasisha mfumo wako wa uendeshaji kwa toleo jipya la haraka.

Screenshot 2023-10-12 at 09-46-51 About Lockdown Mode.png
 
Back
Top Bottom