Mahakama ya Wilaya ya Momba, iliyopo katika Halmashauri ya Mji Tunduma, Jana imewaachia huru Watuhumiwa 34 wa uhaini, kutokana vurugu za Oktoba 29, 2025.
Kwa mujibu wa Mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Wilaya ya Momba Ndg. Simon Pelesi alisema kuwa, zoezi hili la watuhumiwa hawa kupata msamaha na kuachiwa huru ni kwa mujibu wa maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wazazi na walezi wa Watuhumiwa hawa wa vurugu za Oktoba 29, 2025 wamemshuru Mhe. Dkt. Samia kwa huruma aliyoionesha kwa vijana hawa na kutoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanakaa na vijana wao kuwaelewesha mambo yanavyo paswa kwenda.