Watuhumiwa wa mlipuko wa bomu Arusha waachiwa huru

tunduruboy

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
423
218
WATU watatu waliokuwa wakishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za urushaji bomu katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani wa CHADEMA, Juni 15 eneo la Soweto wameachiwa.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana huku uchunguzi juu ya suala hilo ukiwa bado unaendelea.

Alipotakiwa kuwataja watuhumiwa hao, Kamanda Sabas hakuwa tayari kwa kusema ni mapema mno kutaja majina ya watuhumiwa hao kwa sababu uchunguzi wa suala hilo unaendelea.

Alifafanua kuwa watuhumiwa walihojiwa na askari wa upelelezi kuangalia uhusiano wao na mlipuko wa bomu katika viwanja vya Soweto na baada ya kukamilika mahojiano hayo wameachiwa kwa dhamana.

Alisema kuwa jeshi hilo halihusiki na mpango wa kutaka kutorosha majeruhi walioko hospitali walioeleza tukio hilo na kudai ni taarifa za mitaani .

“Kuhusu propoganda zilizoenea jijini Arusha kuwa vyombo vya dola vina mpango wa kutorosha wagonjwa wanaosema ukweli hospitalini na kuwapeleka kusikojulikana si za kweli na ni upotoshaji,” alisema.

Alisema polisi au watu wa usalama wana wajibu wa kuhoji mtu yeyote pale tukio linapotokea ili kubaini ukweli wa jambo, hivyo wagonjwa hao hawana haja ya kuogopa na wasitishwe na maneno ya uongo ya mitani.

Sabas alisema hivi sasa wanaendelea na uchunguzi dhidi ya tuhuma za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Freeman Mbowe, pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wabunge wanne wengine na wafuasi wao 70.

SOURCE: Tanzania Daima
 
km upelelezi bado wana hakika gani kuwa mahojiano yao yamekamilisha uhakiki wa kutohusika hao watu?Km wamehusika kuna dhamana ya ugaidi?km hawajahusika kwanini waendelee kuwa chini ya dhamana?
 
Lazima wawaachie hawa, maana wameshajua DVR imenasa kilakitu hivyo imeshakuwa ngumu kuwabambikia sasa. Mbona Kamishna Chagonja kimya ghafla??
 
'...aagh,kumbe watuhumiwa......................mi nlidhani washtakiwa bwana'
 
Sasabasi alisema hivi sasa wanaendelea na uchunguzi dhidi ya tuhuma za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Freeman Mbowe, pamoja na Mbungewa Arusha Mjini, Godbless Lema, wabunge wanne wengine na wafuasi wao 70.

Kwahiyo wameacha kuchunguza mabomu ya kwenye mkutano yalio uwa watu, Sasa wana chunguza mkutano wa Waombolezaji.

Kweli chaginja Mweupe!
 
Muhusika wa tukio hili anaachwa kwa nini? Mwigulu ni mtuhumiwa namba moja lakini anadunda tu! Vyombo vya usalama vimepoteza hadhi ya kuwatumikia watanzania kwa usawa, na badala yake vimegeuka kuwa kitengo cha propaganda ndani ya ccm!
 
Watuhumiwa wameachiwa wakati uchunguzi unaendelea!!?????????

Well Noted!!!!!!
 
WATU watatu waliokuwa wakishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za urushaji bomu katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani wa CHADEMA, Juni 15 eneo la Soweto wameachiwa.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas, alisema watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana huku uchunguzi juu ya suala hilo ukiwa bado unaendelea.
Alipotakiwa kuwataja watuhumiwa hao, Kamanda Sabas hakuwa tayari kwa kusema ni mapema mnokutaja majina ya watuhumiwa hao kwa sababu uchunguzi wa suala hilo unaendelea.

Alifafanua kuwa watuhumiwa walihojiwa na askari wa upelelezi kuangalia uhusiano wao na mlipukowa bomu katika viwanja vya Soweto na baada ya kukamilika mahojiano hayo wameachiwa kwa dhamana.
Alisema kuwajeshi hilo halihusiki na mpango wa kutaka kutorosha majeruhi walioko hospitali walioeleza tukio hilo na kudai ni taarifa za mitaani .

“Kuhusupropoganda zilizoenea jijini Arusha kuwa vyombo vya dola vina mpango wakutorosha wagonjwa wanaosema ukweli hospitalini na kuwapeleka kusikojulikana siza kweli na ni upotoshaji,” alisema.
Alisema polisi au watu wa usalama wana wajibu wa kuhoji mtu yeyote pale tukio linapotokea ilikubaini ukweli wa jambo, hivyo wagonjwa hao hawana haja ya kuogopa nawasitishwe na maneno ya uongo ya mitani.

Sasabasi alisema hivi sasa wanaendelea na uchunguzi dhidi ya tuhuma za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Freeman Mbowe, pamoja na Mbungewa Arusha Mjini, Godbless Lema, wabunge wanne wengine na wafuasi wao 70.

Vipi tuhuma walizotoa Nape, Mwigulu na Lukavi!?
 
Kama kusingekuwa na mkanda uliorekodi mrushaji ambae ni mapolisi hao hao, hawa watatu ndio wangetolewa kafara kama Abross wa Olasiti.
.
 
Waachiwe wasiachiwe tunachomwomba Mola ni hii hali isije rudia tena wakati wowote ule hasa wakati wa uchaguzi ulioahirishwa. Na sasa wanachi na wanachama chochote kile tuwe macho wakati tukiwa kwaenye mikutana ili lolote likitokea tuwe tayari kupambano nalo na hasa hasa kuwashika live wahusika!

Wana CDM tusiogope wala kutishika na yaliyotokea, siku ya kupiga kura tujitokeze kwa wingi kabisa kuwachagua madiwani wetu. Polisi mtulinde sana siku hiyo.
 
WATU watatu waliokuwa wakishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za urushaji bomu katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani wa CHADEMA, Juni 15 eneo la Soweto wameachiwa.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas, alisema watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana huku uchunguzi juu ya suala hilo ukiwa bado unaendelea.

Alipotakiwa kuwataja watuhumiwa hao, Kamanda Sabas hakuwa tayari kwa kusema ni mapema mno kutaja majina ya watuhumiwa hao kwa sababu uchunguzi wa suala hilo unaendelea.

Alifafanua kuwa watuhumiwa walihojiwa na askari wa upelelezi kuangalia uhusiano wao na mlipuko wa bomu katika viwanja vya Soweto na baada ya kukamilika mahojiano hayo wameachiwa kwa dhamana.

Alisema kuwa jeshi hilo halihusiki na mpango wa kutaka kutorosha majeruhi walioko hospitali walioeleza tukio hilo na kudai ni taarifa za mitaani . "Kuhusu propoganda zilizoenea jijini Arusha kuwa vyombo vya dola vina mpango wa kutorosha wagonjwa wanaosema ukweli hospitalini na kuwapeleka kusikojulikana si za kweli na ni upotoshaji," alisema.

Alisema polisi au watu wa usalama wana wajibu wa kuhoji mtu yeyote pale tukio linapotokea ili kubaini ukweli wa jambo, hivyo wagonjwa hao hawana haja ya kuogopa na wasitishwe na maneno ya uongo ya mitani.

Sabas alisema hivi sasa wanaendelea na uchunguzi dhidi ya tuhuma za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Freeman Mbowe, pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema, wabunge wanne wengine nawafuasi wao 70.

Chanzo: Tanzania Daima
 
Ila wa Tindikali Igunga bado na Wale wa kanisani kimyaaaaa!!!! Ccmmm hiii jaman
 
Kuna mhubiri mmoja anasema "Watashindana lakini hawatashinda" CCM hamuwezi kushindana na watu wamesha wachoka, mabadiliko yako miyoni mwa watanzania hivi sasa, mbaya zaidi damu vinazo mwagwa ni gia yakuondoka madarakani!
 
Hii nchi sio ya magamba na siku c nyingi tutairudisha mikononi mwa watanzania!!
 
Back
Top Bottom