driller
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 1,116
- 240
imepita kama siku mbili hivi nilikua maeneo ya dit ninakula kwa wale wanaofahamu eneo ni MANGESHO sasa nikawa nimeweka bag ya laptop kwenye kiti ambacho nilikua nimekalia..! akaja jamaa mmoja hivi.., sio kwamba nawasema hawa watu vibaya ila jamaa alikua mhaya..! alikua ameshika plate imejaa wali na maharagwe na mamboga mengine..! jamaa akamwagia bag yangu maharage yani badala ya kuomba msamaha akapita tu akaja akakaa kwenye meza hiyo hiyo niliyo kaa mimi, na aliona kua amenimwagia maharage..! ikabidi nimwambie kua jamaa "hujaona umenimwagia maharage hapa..!" jamaa akasema "wewe huoni kantini ilivyobanana hivi sasa ulitegemea mimi nitafanya nini...!" dah asee nilipandwa na hasira...! ninashukuru tu nilimwambia "asee huu sio ustaarabu rafiki yangu...!"
yani jamaa aliniharibia siku...!
sio vizuri jamani..!
vipi wewe kimekutokea kipi..? na uli react vipi...?
yani jamaa aliniharibia siku...!
sio vizuri jamani..!
vipi wewe kimekutokea kipi..? na uli react vipi...?